Rais kuwa na mamlaka sio kuyatumia kwa faida zake binafsi za kisiasa. Unadhani rais kupewa mamlaka, kapewa ili awakomoe mahasimu wake kisiasa? Nyie ndio wale mnadhani kila afanyalo rais ni sahihi, kisa kapewa mamlaka ya kuongoza nchi. Sio bure unaona anasaka kinga za kutokushitakiwa akiwa madarakani, ni kwa sababu anajua kuna mambo anafanya kinyume cha madaraka aliyopewa, na viazi kama nyie mnaona hayo ndio matumizi ya madaraka.
Hapa ndio tunaposema kuwa katiba hii mbovu inatoa madaraka makubwa kwa rais kupita kiasi, mpaka anafikia mahali pa kutumia madaraka yake vibaya kwa faida yake binafsi. Lisu ni msaliti kwa tafsiri ya ccm, na ukitaka kujua ww ni kiazi fuata upepo, kamfungulie kesi mahakamani udhibitishe huo usaliti wake.