Vyuo vikuu vyote jirekebisheni kuna namna mmepotoka kidogo.

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Competition kubwa sasahivi wanafunzi kwenda kusoma UNI private na one yako kali limekuwa jambo la kawaida , sasa mtu unakuta ana div 1 ya 7 au 8 from PCB naye anataka akasome udaktari ,sasa hivi hata div ya 5 tu kupata MD kipengele labda wakutupe UDSM ya mbeya huko au UDOM kwa mbinde au kama unajiweza ukalipe mil 7-9 KIUT
 
Badala yake eti waende VETA wakati yeye mwenyewe hapo majuzi kati kamaliza UD

Kweli uchawi muombee mwenzako🀣
Aende chuo kwa Jasho lake mwenyewe sio kwa michongo-michongo na connections za maGod fathers. Hebu fikiria; "Amefaulu" F6 kwa michongo-michongo na sasa anataka aende chuo kwa michongo-michongo.
 
Badala yake eti waende VETA wakati yeye mwenyewe hapo majuzi kati kamaliza UD

Kweli uchawi muombee mwenzako🀣
Niwe mkweli, kwa ufaulu wangu wa Advance, ingekua ni wakati huu nisingeingia hapo UDSM, sio kwamba ni mbaya ila hiyo competition, ingenikataa mapema sana.

Ila sasa wakati ule, ni kugusa tu UD ikajibu, wee coca fanya ku confirm, na mie bila kuchelewa ni kubofya tu twichiiiii.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, coca huyo ndani ya main campus.
Alooooh.
 
Lakini mbaya zaidi now wanafunzi wameshakuwa wengi sana na bado cutting points ni hizo hizo tu
Sasa washushe cutting point mkuu wakati siku hizi one ya 3 ni kawaida. Mimi binafsi nikiangalia matokeo ya shule yangu niliyomaliza form six nashangaa maana watoto wanafaulu haswaa, mwenye two ndo kafeli wakati enzi zetu one zilikuwa chache two ndo nyingi.
 
Mie sitaki nacheka km mwehu hapa, eti KIUT.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ukisoma comment yangu mwisho kuwa labda ukasomee "Beekeeping" na jibu lako utajikuta unarudi pale pale kuungana na mimi kuwa labda cousre isiyo na competition
 
Tunapoelekea kama huna one ya 3 kupata MD chuo cha serikali sahau. Nawaonea huruma vijana wa kesho.
 
Mie sitaki nacheka km mwehu hapa, eti KIUT.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
We acha tu πŸ˜‚,madogo kila wakikaa wanawaza UDSM,MUHAS NA UDOM hawajui kwamba kule kuingia ni mtiti kwa sasahivi ,tena usiombe umesoma advance Science combπŸ˜‚
 
Safi sana mkuu nimependa analysis yako kisomi sana

Lakini unadhani VETA ni solution ikiwa system yetu haijaandaa mazingira rafiki kwa vijana wanaoenda huko kusoma technical skills?

Tumeshuhudia wengi wao wamesoma huko VETA lakini uwezeshwaji umekuwa duni.

Nchi za wenzetu wametengeneza system nzuri ya kuwawezesha vijana kama hao huku hakuna.

Pia.mashinikizo kutoka kwa family
Hakuna mzazi atakubali mwanaye mwenye 1.7 anende VETA mkuu sidhani.

Natambua kozi za afya zinahitaji watu competent sana maana afya ya mtu ni muhimu .

Ina maana kuwa ufaulu huu wa sasa ni feki mkuu?.
Mimi naona bado tunaforce kuishi dunia ya kale ambapo
Teaching materials zilikuwa chache
Shule zilikuwa chache zaidi
Walimu walikuwa wachache pia

Moreover online materials nazo zilikuwa chache tofauti na sasa hapo lazima wafaulu mkuu au unasemaje?

TCU wanapiga chujio kali sana kwa vyuo vya sasa lakini swali linabaki kuwa ni wote wenye 1 ni ufaulu feki?

Kama wapo waliofaulu kiuhalali wakakosa nafasi na wakapata ambao walifaulu ufaulu "fake" tunaosemea inakuwa kosa la nani?

Asante
 
Mie sitaki nacheka km mwehu hapa, eti KIUT.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna dog alifaulu vzr tu akaomba zake UDSM tu ,akaja kushangaa hao hao UDSM wamemtupia Iringa kwenye kabranch kao ka MUCE kamekaa kama shule ya sekondari atleast sasahivi ndo wanakajenga jenga πŸ˜‚.

Na nasikia kuna MUHAS inajengwa Kigoma kuna UDOM inajengwa Njombe πŸ˜‚πŸ™Œ na kuna UDSM inajengwa Ruangwa Lindi πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nilichoona inategemea ameomba chuo gani na kozi anazoomba amezipanga vipi. Mimi binti yangu alipata D. 1. Lakini awamu ya kwanza aliomba UDOM, Mzumbe na UDSM na vyote akakosa. Na shida kubwa ni namna alivyokuwa amepanga zile kozi.Nilichofanya niliingia mzigo mwenyewe. Kozi option number 2 nikifanya kozi option namba 1. Amepata vyuo vyote vitatu.
 
Kuna mlipuko mkubwa sana wa idadi ya watu, hatakama div I zingekuwa ngumu kupata bado vyuo vingelemewa tu.

Tunazaa zaidi ya watoto 2.3m kwa mwaka. Hii ni zaidi ya idadi za ujerumani, ufaransa, uhispania, ubelgiji, uholanzi, uswizi, sweden na norway zikiunganishwa kwa pamoja!

Tuweke madaraja ya vyuo kama wenzetu. Vyuo vitofautiane kihadhi.

Kuwe na vyuo vya hadhi ya juu vinavyopokea wanafunzi wenye ule ufaulu wa juu kabisa. Serikali iwekeze huko kwenye mambo ya utafiti na ubobezi, kama kipaumbele.

Halafu vyuo vingine ndo vipambane na hao waliobaki.

Elimu ya lazima iwe mpaka form 6, baada ya hapo mtu achague aende kwenye taaluma ama ufundi. Sio lazima kila mmoja atoboe kwenye taaluma.

Shule ni mfumo! Sio kila mtu anaweza kutulia darasani na kusikiliza muda mrefu. Mifumo huwatema baadhi ya watu. Waende jeshini na kwenye ufundi.

US wana ivy league and peers, UK wana russell group and oxbridge, China wana C9, Korea Kusini wana SKY, Ufaransa wana Les Grandes Ecoles, Australia wana Group Eight nk, nk. Haya ni makundi yao ya vyuo vya hadhi ambapo wanapelekwa vipanga na kunolewa kwa manufaa ya taifa.

Ndio maana nchi za wenzetu haziishiwi wavumbuzi muhimu. Pia tutuoe motisha kwa vyuo binafsi na tuvikuze.
 
Yes. Lazima vyeti vya baadhi ya vyuo viheshimikeipasavyo. Chuo gani mwanafunzi yupo at large mpaka anakwenda kugawa utamu huko Mwanza??
Enzi hizo SUA kulala ilikuwa ni bidhaa adimu.
 
Jomba huoni jinsi watoto walivyopasua mitihani yao? Halafu kumbuka pia watoto wengi wana F za Basic Maths form four ndo maana wanatemwa kozi nyingi pamoja na kugonga One form 6
 
We acha tu πŸ˜‚,madogo kila wakikaa wanawaza UDSM,MUHAS NA UDOM hawajui kwamba kule kuingia ni mtiti kwa sasahivi ,tena usiombe umesoma advance Science combπŸ˜‚
Hatariii sanaa. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mie mnanichekesha hapa kwa kweli, wataenda huko huko hakuna namna.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…