Vyuo vikuu vyote jirekebisheni kuna namna mmepotoka kidogo.

Tatizo la Tanzania ni ubora wa elimu. Hata wakichukuwa division 1++, lakini wahitimu wengi hawana qualification za kimataifa. Elimu inabaki kwenye ''ujanja ujanja'' wa matumizi ya elimu ya kitanzania lakini hakuna wahitimu wenye viwango. Mtu hata akivuka mpaka aende Kenya anakuwa hana kiwango.
 
Lakini kibaya zaidi sikuhizi wengi wanafaulu inabidi kuchagua wachache wenye one kali kabisa zile
Japo nayo sio sawa, mtu anayepata one or two advance afu ananyimwa nafasi ya kusomea kitu ambacho angeweza kumudu ni tatizo la kisera ambalo hakuna namna serikali anaweza kulikwepa.
 
Na bado wanakurupuka tu watu waende VETA kufanyaje ikiwa hata ukimaliza hujui unaenda wapi? Mfumo unakutupa kote?

Mtu akiamua ajiajiri challenges nyingi kodi kama utitiri sasa aende wapi?

Wasomi wanakimbilia kwenye siasa
Halafu huko siasani ukimess kidogo tu, unafunguliwa kesi ya Uhaini. Dah! Fedha zetu ss walipa kodi zinaidhinishwa kirahisi-rahisi tu kuendesha kesi za mchongo zisizo na maslahi kwa Taifa.
 
Na bado wanakurupuka tu watu waende VETA kufanyaje ikiwa hata ukimaliza hujui unaenda wapi? Mfumo unakutupa kote?
Wanaotusakizia eti vijana wetu waende veta vijana wao wanawapeleka nje au kuwatengenezea koneksheni za vyuo hapa-hapa Bongo. Wao wenyewe mishahara yao usipime licha ya marupurupu kibao. Hakika aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
Mtu akiamua ajiajiri challenges nyingi kodi kama utitiri sasa aende wapi?
Hapo kjwenye kodi tatizo ni wale wataalam wanaotakiwa waibue vyanzo vya mapato kwa Serikali. Wakiketi maofisi mwao wanaona Bodaboda zinapita nao chap' wanaorodhesha kwenye list ya vyanzo vya mapato. Wakiona watu wanajisitiri pembeni mwa barabara/vichakani nao chap' wanaweka kwenye list ya vyanzo vya mapato,mkulima akivuna mazao yake na anayasafirisha kupeleka nyumbani kwa familia yake nao chap' wanaweka kwenye list ni chanzo cha mapato n.k n.k
Wasomi wanakimbilia kwenye siasa
Siasa inalipa sana. Just imagine mtu anaketi bungeni kazi ni kupiga makofi meza au kusinzia mwanzo mwisho lakini at the end of the day analipwa 500k+ isiyo na makato.
 
Japo nayo sio sawa, mtu anayepata one or two advance afu ananyimwa nafasi ya kusomea kitu ambacho angeweza kumudu ni tatizo la kisera ambalo hakuna namna serikali anaweza kulikwepa.
Kwani wenzetu wao wamewezaje?
 
Nimejaribu kukuelewa lakini nimeshindwa. Unataka vyuo viwaache baadhi ya wenye 1 kali ili vichukue pia wenye ufaulu dhaifu provided wanakidhi minimum entry requirements?

Provided hakuna anayependelewa au kuonewa, in my opinion, that’s a fair game. Kama unataka kila anayekidhi minimum entry requirements apate admission, vyuo vipya vianzishwe au vyuo vilivyopo vitekeleze expansion measures ili kuongeza admission capacities zake!
 
Quality ya hizo one hali ikoje mkuu?

Mfano mambo yetu yale ya Pure Math ya ku derive wanayapiga vilivyo au wanazuga kwenye mitihani tu?
 
Yeah. Wazo zuri - Itachangia kupunguza malalamiko.
 
Inafikirisha.
Kama wana uwezo kweli wapige SAT, wapige ACT, wapige ma essay, wachukue fursa vyuo vya kimataifa kibao vinatafuta vipanga wa ukweli scholarships kama zote.

Sio lazima kusoma Tanzania.

Hivi ninavyoongea kuna dogo katua Kazakhstan ana full scholarship, wengine wako Europe, wengine US.

Kuna dogo anafanya mtihani wa form four sasa, lakini baba yake kashaanza kumpangia mipango ya kuja kusoma MIT.

Wamuone huyu hapa mwenzao kachukua maisha kwa scholarships.


View: https://www.instagram.com/reel/Ddj7hRvo0gk/?stkn=MWxoYnZnYm4xNTg1Yg==
 
Quality ya hizo one hali ikoje mkuu?

Mfano mambo yetu yale ya Pure Math ya ku derive wanayapiga vilivyo au wanazuga kwenye mitihani tu?
Hapana math bado ni ugonjwa wa taifa

Kila mwaka inakuwa ya mwisho mkuu
 
Division 1 ni ufaulu dhaifu?
 
Sijui hawa wa kwetu ni kutokana na kuaminishwa(kunywehwa kasumba) kwamba kila kitu ni kwa connections tu au vipi.
 
Japo nayo sio sawa, mtu anayepata one or two advance afu ananyimwa nafasi ya kusomea kitu ambacho angeweza kumudu ni tatizo la kisera ambalo hakuna namna serikali anaweza kulikwepa.
Ndio tatizo linaanzia kwenye sera ya nchi kiujumla tunazalisha wasomi wengi hatujui tunawapeleka wapi
 
Mtu mjinga anafikiria kuongeza expenses kama chanzo cha mapato

Content creator nao wanalipia vibali🤣

Na hao hao wasomi ndio wameamua hayo na ukichunguza ni zao la hivi hivi vyuo vyetu na walipiga one kali hapo ndio swala la magumashi linajitokeza tena upya

Msomi kabisa na alifaulu vizuri amekuwa kiongozi anawezaje kuamua jambo la hovyo namna hiyo? Unakuja ku criticize hiyo division 1 yake tena

Unapata jibu rahisi tu
 
Sijui hawa wa kwetu ni kutokana na kuaminishwa(kunywehwa kasumba) kwamba kila kitu ni kwa connections tu au vipi.
Si unamsikia dogo anakwambia kwao Tarime ndanindani huko maana yake hata kama connection kaitafuta kwa kutoka mbali si mtoto wa Oysterbay huyo.
 
Dhaifu is a relative term! Huoni kama ufaulu wa 1.6 ni dhaifu ukilinganisha na ufaulu wa 1.3, 1.4, au 1.5, kwa mfano?
Unapotosha sasa

Division 1 hata iwe 1.9 bado sio dhaifu kwako dhaifu interm of what?

Na huku tunapoelekea nyie ndio mnafanya hizi 1 fake kuwa nyingi maana mtu anaona akipata 1.6 ni dhaifu matokeo yake vyuo vinapiga panga wengi kwa kugundua ni 1 ,a ujanja ujanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…