Wa kienyeji, mtu ameniita hivi, inamaanisha nini?

Wa kienyeji, mtu ameniita hivi, inamaanisha nini?

Kuna mtu huko inbox ameniita wa kienyeji, nimemuuliza inamanisha nini amekataa kuniambia.
Naomba mniambie hili jina linamaanisha nini? au ni tusi?

Nimejaribu kusearch humu JF nakutana na nyuzi za “kuku wa kienyeji” na “waganga wa kienyeji” tu.

View attachment 3305216
Kuna mawili hapo: la kwanza, wewe waweza kuwa ni mrembo wa asili usiyejichubua kwa mikorogo ama kutengeneza mishepu ya mchina, yaani upo natural.

Jambo la pili yaweza kuwa muonekano wako ni kama binti wa kijijini.

Zaidi ya hapo zipo maana ndogondogo za mtu kukusifia kama ushawahi kutoka naye, lakini ni matusi siwezi yaweka hapa.
 
Una hela wewe 😅?
Pesa ya kawaida TU mkuu, (ya kula hainipi shidaaa)

Mimi ni tofauti na wanajf wengine Mimi Sina gari, Mimi Sina degree, Mimi ni introvert, Mimi ninaishi uswahilini, Mimi sijawahi kwenda nchi za nje, Mimi naandika jf kupitia Tecno s1 simu zinazopigngwa na kutukanwa na Watu wa jf wengi

Nimejitahidi kuishi maisha yangu halisi hata mtandaoni
 
Kwa binadamu Wakienyeji ina maana nyingi ambazo si nzuri kwa kweli
1. Ngili (mshamba hupo hupo tu)

2. Upo local (una mambo ya kizamani)

3. Bwanyenye (upo kama kitumbua huna mbele wala nyuma)

4. Zwazwa (muda mwingi unashangaa mimacho kodo kama mkaguz wa mapato ya serikal)

5. Ili ni tusi kabisa kiukweli kakatusi mripoti TCRA
 
Back
Top Bottom