Waafrika uongozi umetushinda; huo ndo ukweli hatakama hatuupendi

Hahaha daah
 
We ulishasikia wapi Tanzania rais anawajibishwa baada ya uongozi mbovu kwenye awamu yake? Utasikia South Africa na nchi zingine ulimwengu wa kwanza ndio wanafanya hivyo.
Ndio maana S.Africa imefikia viwango vikubwa vya maendeleo ktk nyanja mbali mbali.
 

Suala la umeme halijawahi kuboreka ndani ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 30, ni kweli mgao kwa sasa ni mkali, lakini haimaanishi tatizo liliwahi kuisha. Usidhani hatuna kumbukumbu vizuri boss. Hata kipindi Cha dhalimu magu mgao ulikuwepo na ushahidi upo. Ww kama ni muumini wa viongozi walevi wa madaraka hiyo ni kimpango wako, lakini huwezi kutulazimisha kuona ulevi wa madaraka ndio utawala sahihi.
 
Mgao hata South Africa na Nigeria upo we unashangaa nini wakati wa JPM kuwepo na mgao baadhi ya maeneo na ilikuwa si mara kwa mara, pia alijitahidi sana kwa muda mchache vile kuzima mgao ikizingatiwa nchi ilikuwa inanuka shida.
Sasa hivi mgao huu haijawahi tokea, hii ni kali.

Angeendelea awamu nyingine mgao ingekuwa historia.

Mtakataa lakini ukweli mnaujua, JPM alikuwa kiboko, vimbeni mpasuke lakini yule mzee respect.
 
JPM pekee ndiye aliiweza hii nchi.
Aliivuruga nchi na ikavuruguka kweli kweli. Ndiye mwanzilisha mpaka wa vikundi vya kufanya uovu na watu wasiyojulikana, chanzo cha kuwepo watu kama Bashite
 
Aliivuruga nchi na ikavuruguka kweli kweli. Ndiye mwanzilisha mpaka wa vikundi vya kufanya uovu na watu wasiyojulikana, chanzo cha kuwepo watu kama Bashite
Sio vikundi vya kufanya uovu, sema vikundi vya kurekebisha tabia.
 
Ngozi nyeusi haiwezi kujitawala. Ndio maana miaka 60 sasa hata sukari tu imetushinda!
Ukikaa na kuitegemea serikali hasa kwa nchi za kiafrika jua utakufa masikini. Fanya yako na jiangalie wewe kama wewe
 
We ulishasikia wapi Tanzania rais anawajibishwa baada ya uongozi mbovu kwenye awamu yake? Utasikia South Africa na nchi zingine ulimwengu wa kwanza ndio wanafanya hivyo.
Huyo Magufuli na Bunge lake la Chama kimoja angeweza kuwaondolea Immunity na kuwaweka Jela ila yeye mwenyewe alikuwa ni Kiongozi mbovu.
 
Tunajilimbikizia mimali kwanza ili tukiacha kazi tusichekwe !
Pia kazi na Bata kama kawaida !
Mimi nimefanya yangu na wengine watakuja nao watafanya yao. !!
Hayo ndio mawazo yetu !!
 
Huyo Magufuli na Bunge lake la Chama kimoja angeweza kuwaondolea Immunity na kuwaweka Jela ila yeye mwenyewe alikuwa ni Kiongozi mbovu.
Nadhani nia yake ilikuwa hiyo ila bahati mbaya ikawa too late !
 
Hii nchi tunahtaji wat wenye akili
Hiv unajua ni Kwa nn mikoa ya Kanda ya ziwa ilikuwa haina maji na ziwa Victoria lipo
Ila
Gas imeweza kutoka mtwara mpaka dar bila shida yeyote
 
Wizi ndio mmeona dili la maana, yaani kila mahali wizi, rushwa, dhulma na hata vifo
Kweli mmetumia 3b na ushee kwa ajili ya hifadhi wakati mnazo kibao
Huu sio umasikini bali mmeamua kuwaachia baadhi wawaibie tu
 
kazi inaendelea vizuri sana karibu kile eneo hususani katika jijini la dar es salaam nadhani unaona huko uliko.....
 
Nadhani nia yake ilikuwa hiyo ila bahati mbaya ikawa too late !
Sikuiona hiyo NIA ila nilichoona ni NIA yake ya kuifanya CCM iwe na nguvu (ktk mtazamo wake) iwe kama Zama za Mwalimu Nyerere, wakati wa sera ZILIZOFELI za UJAMAA na KUJITEGEMEA .

Pamoja na kuwa na PhD lakini alikuwa na uelewa mdogo sana haswa kuhusu SIASA na NYAKATI.

Ile kauli mbiu yake ya MATAJIRI WATAISHI KAMA MASHETANI alikua anataka "kuigiza" lile AZIMIO LA ARUSHA LA MWALIMU NA KAWAWA WAKE.

Mimi nilimpigia Kampeni Magufuli sana Kitaani na hata humu JF lakini nilipogundua kuwa huyu ni CHIZI anaerusha Ngumi hewani itakayompiga ni huyo huyo nilijitenga nae mbali nikawa ni Critic wake na hatimae nikakihama na Chama Cha Mapinduzi alichokigeuza kuwa kuwa Genge la Kimafia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…