Tetesi: Waarabu wa Dubai Port kuwang'oa TICTS bandarini

Tetesi: Waarabu wa Dubai Port kuwang'oa TICTS bandarini

Kwa hiyo unakiri unabwabwaja tu bila uthibitisho!!?
Tafsiri ya kukuuliza hilo swali ni kwamba kitu kinaitwa uthibitisho huwa ni geresha ya kukwepa ukweli uliopo. Ndio maana nikakueleza na wewe uthibitishe, ulichosema ni kweli Ila kwenye kuthibitisha utashindwa.

Ni sawa na mtu akuambie thibitisha kuwa wakristo hawataenda peponi.
 
Kwa technolojia yao ilivyo kubwa, si ajabu watu wakapunguzwa sana hapo Bandarini. Na wale wenzangu na mimi waliozoea mseleleko, wajipange tu kurudi mashambani.
Ama kwa hakika.maana wao ndio the leader on the port industrial worldwide
 
Ni kwa nn anaposemwa mwarabu huwa mnahusisha dini? Kipindi cha JK kulikuwa na story za Marekani kutaka kupewa kigamboni, mbona sikuona mtu/watu wakihusisha dini? Bali nilichoona ni kuhusisha mambo ya kijeshi na unyang'anyi?

Hata sasa kumeibuka story ya Marekani kutaka kupewa bandari ya Bagamoyo, sijaona mtu akihusisha dini bali inahusishwa military base na unyang'anyi mwingine.

China pia hivyohivyo akitaka kupewa sehemu kuendesha watu hukosoa sana, Ila sioni wakihusisha dini.

Kwa nn wakisemwa waarabu mnakimbilia dini?
Kwasababu hayo mataifa hayaendekezi udini tofauti na mataifa ya Kiarabu
 
Tafsiri ya kukuuliza hilo swali ni kwamba kitu kinaitwa uthibitisho huwa ni geresha ya kukwepa ukweli uliopo. Ndio maana nikakueleza na wewe uthibitishe, ulichosema ni kweli Ila kwenye kuthibitisha utashindwa.

Ni sawa na mtu akuambie thibitisha kuwa wakristo hawataenda peponi.
Huna uthibitisho,na mtoa mada Hana uthibitisho,kasukumwa tu chuki mnazofundishana ukwata,ycs nk
 
Hawa waarabu ni waharibifu wataharibu nchi yetu
Angalia mfano wa loliondo,ukifika loliondo ni kama upo uarabuni

Nakuhurumia nchi yangu hawa waarabu ni watu wa hovyo kabisa tuombe Mungu apatkane kiongozi atakaewafurusha
Acha fikra potofu mkuu,hao dp wanaendesha bandari nyingi tu europe,kama sikosei hata greece na cyprus hao dp ndio waendeshaji wa hizo bandari,hata holland wana sehemu ya bandari iko chini yao,hao ni wazoefu wa hayo mambo hawana uswahili kama wa akina karamagi,kikubwa wapewe space wafanye kazi yao,naamini hamna container vessel itakayokaa bandari masaa 24 au kule nangani wiki 2 kusubiria kuingia bandarini,hao jamaa ni proffesional sio unga unga mwana
 
Ticts ni kampuni ya kizalendo issue Ni kuwawweesha kufikia target au kuwaondoa ?
Ticts wanapiga pesa mizgo kibao kwa nn wasiimprove kununua mashine nzuri..Ni kampuni nzuri sema hawana huduma mbovu na pale bandari kitu kidogo mzigo ukichelewa kutoka ndani ya siku 7 unapata storage ..

Kuna watu wanacontainer labda Tano unafika unakuta zimeshushwa 2 kwa ukaguzi ila zitoke nyingine zimebaki! Zikikaa sana zinaingia storage
 
Back
Top Bottom