Mbona katika maelezo yako inaonekana ni mtu MMOJA tu ndiye amemuita hivyo?? Lakini heading inasema Waarabu (pamoja na kwamba umeandika "Warabu") ukimaanisha ni wengi.
Kwa upande mwingine mbona humu JF baadhi ya Waislam huwa wanasema neno Kaffir siyo tusi?!!! Wanasema maana yake ni mtu ambaye hamuamini au kumuabudu Allah!!
Kwa kuwa kila mtu anamuabudu Mungu anayemuamini yeye basi kama mimi naamini Mungu Baba muumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana na mtu mwingine haamini ninayoamini mimi na yeye ni Kaffir!!! Kama wengine wanaamini Ng'ombe ndiyo Mungu, mimi ambaye siamini hivyo ni Kaffir kwa mtu huyo.
Kwa hiyo let us take things SIMPLE or EASY!!! AMINI UNACHOAMINI. Kila mtu ni Kaffir kwa mtu anayeamini tofauti na mwingine.