Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.

Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Hebu mcheki huyu jamaa anayejiita Maghayo 🙂
 
Kuna jamaa nilimuacha sehemu, sitaki kupataja sababu tulikuwa tunafanya shughuli za kialifu so mara kwa mara tulikuwa tukikamatwa
Hiyo life sikuipenda ilibidi nirudi afrika
Nikajichanga vizuri na vipesa nilivyorudi navyo kiukweli nilikuwa mtu wa furaha tofuti na uko uzunguni
Jamaa yangu alivyorudi akanikuta ninamaisha yangu poa kabisa nina kiusafiri na na tv kubwa nchi 65 nina mke wa kiswahili anamkia wa maana, na vitoto yan vifaida vya ndoa viwili
Super marker kama Ulaya
Jamaa hakuvumilia akaapa
Dah yanini kurudi kule na maisha haya mzee?!
Nami kiukweli nitafia apa apa nyumban na uzee wangu mzuri baada ya maangaiko
Samahanini mambo mengi nimeficha sababu kama nilivyokwisha ieleza hapo mwanzo, sio sifa nzuri niadithie life mbovu kufundisha vijana wenye mawazo mazuri ya kutafuta maisha ughaibuni
Tv kubwa nchi 65 .Umenichekesha.Mimi nikajua labda una kiwanda hata cha kutengeneza vifungashio na umeajiri watu 30.Sasa TV nayo ya kulingia jamani.
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.

Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
ok sawa
 
Ni vizuri ukaendelea kufatilia Maisha yako maana aliyekuzidi kakuzidi tu Mtu Kama wewe hata Kenya haujafika Sasa unajua Nini wewe mtoto mdogo
Ajabu hilo ndio tatizo la watanzania yupo busy kujadili maisha ya mtu badala ya kuhangaika na ya kwake, wewe upo mburahati huko maji na umeme shida , unasoma huku huna uhakika wa ajira unahangaika na mtu aliye marekani kweli?
 
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!

Kwa hio huyo ndo anapenda kuvaa miwani mikubwa kama anchomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni choon, na ndo huyu ambaye hana hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out mliokua mkimsubiri Sura yake haina nuru
 
Maisha si kushindana.Ukiishi kwa kushindana na wengine basi utaishi kwa stress .Ishi maisha kwa kushindana na wewe mwenyewe kuhusu jana ,leo na kesho yako.
Hongera. Hili la watu kujaribu kuishi maisha ya ''watu watasemaje'' ndiyo linafanya wengi wajikunyate. Halafu wengi naona wanaandika wakiwa na inferiority complex ya kujiuona wanyonge kwa watu waliwahi kuishi majuu. Nimekumbuka kijijini miaka hiyo. Kila ikifika Xmass wakati vijana wengi wanarudi likizo vijijini kulikuwa kunatokea ugomvi kati ya vijana wa kijijini na vijana wa mjini. Kisa ni vijana wa kijijini walikuwa wanadhani wanadharauliwa na vijana wa mjini. Na kejeli za ''karudi amechakaa'' zilikuwa haziishi kusemwa na vijana wa vijijini.
 
Ajabu hilo ndio tatizo la watanzania yupo busy kujadili maisha ya mtu badala ya kuhangaika na ya kwake, wewe upo mburahati huko maji na umeme shida , unasoma huku huna uhakika wa ajira unahangaika na mtu aliye marekani kweli?
Ahahaha mkuu ukweli lazima usemwe ili mbadirike muwajali wazazi wenu,acha kujifariji na hoja za kipumbavu!
 
Maisha ni popote ila kwenye za dunia ya kwanza kuna opportunities nyingi kuliko third world na living standards ni juu kuliko third world, kuna elimu nzuri, huduma nzuri za afya, na za kijamii, malipo ni makubwa kwenye kazi , kama huyo ndugu yako kashindwa itakuwa ni matatizo yake binafsi wengine walevi nakadhalika ila huwezi ukasema bongo ni bora kuliko marekani ki maisha utakuwa unajidanganya
Kwa hio huyo ndo anapenda kuvaa miwani mikubwa kama anchomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni choon, na ndo huyu ambaye hana hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out mliokua mkimsubiri Sura yake haina nur
 
Back
Top Bottom