Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Hebu mcheki huyu jamaa anayejiita Maghayo 🙂
 
Tv kubwa nchi 65 .Umenichekesha.Mimi nikajua labda una kiwanda hata cha kutengeneza vifungashio na umeajiri watu 30.Sasa TV nayo ya kulingia jamani.
 
ok sawa
 
Ni vizuri ukaendelea kufatilia Maisha yako maana aliyekuzidi kakuzidi tu Mtu Kama wewe hata Kenya haujafika Sasa unajua Nini wewe mtoto mdogo
Ajabu hilo ndio tatizo la watanzania yupo busy kujadili maisha ya mtu badala ya kuhangaika na ya kwake, wewe upo mburahati huko maji na umeme shida , unasoma huku huna uhakika wa ajira unahangaika na mtu aliye marekani kweli?
 
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!

Kwa hio huyo ndo anapenda kuvaa miwani mikubwa kama anchomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni choon, na ndo huyu ambaye hana hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out mliokua mkimsubiri Sura yake haina nuru
 
Maisha si kushindana.Ukiishi kwa kushindana na wengine basi utaishi kwa stress .Ishi maisha kwa kushindana na wewe mwenyewe kuhusu jana ,leo na kesho yako.
Hongera. Hili la watu kujaribu kuishi maisha ya ''watu watasemaje'' ndiyo linafanya wengi wajikunyate. Halafu wengi naona wanaandika wakiwa na inferiority complex ya kujiuona wanyonge kwa watu waliwahi kuishi majuu. Nimekumbuka kijijini miaka hiyo. Kila ikifika Xmass wakati vijana wengi wanarudi likizo vijijini kulikuwa kunatokea ugomvi kati ya vijana wa kijijini na vijana wa mjini. Kisa ni vijana wa kijijini walikuwa wanadhani wanadharauliwa na vijana wa mjini. Na kejeli za ''karudi amechakaa'' zilikuwa haziishi kusemwa na vijana wa vijijini.
 
Ajabu hilo ndio tatizo la watanzania yupo busy kujadili maisha ya mtu badala ya kuhangaika na ya kwake, wewe upo mburahati huko maji na umeme shida , unasoma huku huna uhakika wa ajira unahangaika na mtu aliye marekani kweli?
Ahahaha mkuu ukweli lazima usemwe ili mbadirike muwajali wazazi wenu,acha kujifariji na hoja za kipumbavu!
 
Maisha ni popote ila kwenye za dunia ya kwanza kuna opportunities nyingi kuliko third world na living standards ni juu kuliko third world, kuna elimu nzuri, huduma nzuri za afya, na za kijamii, malipo ni makubwa kwenye kazi , kama huyo ndugu yako kashindwa itakuwa ni matatizo yake binafsi wengine walevi nakadhalika ila huwezi ukasema bongo ni bora kuliko marekani ki maisha utakuwa unajidanganya
Kwa hio huyo ndo anapenda kuvaa miwani mikubwa kama anchomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni choon, na ndo huyu ambaye hana hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out mliokua mkimsubiri Sura yake haina nur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…