Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian


Umenikumbusha kuna siku tumeenda kunywa rafiki yangu alikuja na jamaa yake (kaka) akamtambulisha anatoka marekani!!….
Khaaah ama nilishangaa jamaa bill zote hana hata mia mbovu ya kuchangia si chakula ci vinywaji anajichekesha tu…..
Had mademu wakaanza kumtania

Naunga mkono hoja hawana hela mwili mkubwa lakin hamna hata aibu kula vya wanaume tu[emoji3][emoji3]
 
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!
Mi nakuelewa kabisa mkuu.
Mfano mzuri Lembebez.
30yrs im States katurudia na gold chain tu
 
Napenda sana hizi story,😂.
Hongera sana mkuu
 
Kama ndivyo basi itakuwa mtu mwenye kudhani hivyo atakuwa na matatizo ya kiakili

Hapana.
Mafanikio ya mwenzako hayawezi kufanana na yako.
Kila mtu anavipaombele vyake.
Ukishalijua hili huwezi kuwashangaa.

Ninakuambia kuna Watu ukiwakea pesa au Pombe watachagua pombe
Kuna Watu ukiwawekea Pesa au Mungu watachagua pesa na kuacha mungu. Na wapo kinyume chao
 
Mleta mada umeongea ukweli.
80% ya walio nchi hizo ulizotaja hali zao kiuchumi si za kuridhisha
Mna ndugu na jamaa huko kama case study
Kongole. Huyu jamaa ni wale wajinga wajinga wanaonunua haya magari mtumba ya mjapana na wanaona wamemaliza kila kitu. Dunia ya leo unaona kuendesha gari ndiyo mafanikio? Kila sehemu kuna wenye mafanikio na wasiyo na mafanikio.
Bongo bana, mwana unakuta anabwata na gari ya yenye kajampia mjepo viti basi yeye anaona ananyonga mbweta mpyaaa! Umaskini waheeed huo
 
Vipi kuhusu walioenda nchi za uarabuni. Mbona hukuwataja?
 
Mkuu hivi wabongo unawajua au unawasikia?

Ni mbongo gani aliyeko Marekani ambaye hapendi Maujiko?

Sema ndiyo hivyo wanamaisha Magumu lakini si vipaumbele mkuu,Hakuna mbongo aliyesota kwenye Maisha magumu halafu uniambie afanikiwe akose Gari kali,Nyumba nzuri na demu mkali,hayupo!.
 
Nataka niende Afghanistan au Iran nikatafute maisha. Nipe connection mkuu
 

Ndio hao Wamarekani wabongo wazee wa macheni na kuslang
 
Mleta mada Yuko vizuri, hebu nyie mnaofikiri Marekani ni mbinguni leteni ushahidi wa mafanikio yenu.Hata hivyo maisha ya Marekani yapo juu kikubwa ukienda fanya KAZI Kwa malengo miaka kadhaa rudi nyumbani uwekeze, Kuna watu Huwa wakirudi likizo yaani mpaka unajiuliza huyu alikuwa Marekani au matombo morogoro
 
Ndugu yangu baada ya mama kufariki ilitumika nguvu sana kumleta msibani. Maana aliondoka tangu mwaka 97.
Baada ya msiba ilibidi atafutiwe kazi nzuri ili abaki nyumbani akafanya miezi miwili akatimka
Na kilichomuondoa alikuwa anajihisi aibu.
Nakielewa.
Wengi sana wanafiwa na.wazazi na ndugu ila hawawezi kirudi kuzika ila ukiona.swaga zao facebook na insta hutaamini.

Ila ukweli nje ukikosea step maisha yako yanaharibika mazima
 

Sikubalian na wewe, kwamba kutoboa marekani ni ngumu, Si Sahihi, watu wanaenda na Visitor Visa kama wale machalii ya R, hawarudi huwezi toboa, kazi utafanyaje mzee unaishi maisha ya "Cash Jobs" hatari

Ingia hizo nchi na vibali utatoboa asubuh kweupe sana

Mfano

Unalipwa $19(hizi ni kazi za wabeba box) kwa saa unafanya masaa 50 kwa wiki, $3800 kwa mwezi ukitoa kodi $3300 kwa mwezi unaishi chumba cha $750(included everythings) unakula $300 kwa mwezi, hivi upo peke ako unashindwaje kutoboa

ACHENI KUSAMBAZA UONGO WAZEE, hizi nchi kama unaponda bata hapa hela yao haina thaman kwao, Ukichange kwa madafu wewe TAJIRI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…