Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

hapo covid-19 wanachotetea ni maslahi tu ya ubunge lakini wajue mwisho wa siku wao sio wanachadema tena na ubunge huo utakoma 2025
 
Unadhani CHADEMA wangeweza kufanya jambo gani zaidi ya kuwafukuza mkuu? hebu tusaidie mawazo
Kuwafukuza ni haki yao lakini ktk kuwafukuza lazima uzingatie utaratibu na si kukurupuka tu kwa hisia😀
 
Double standard haijawahi kuisha hapa Duniani na haitokuja kuisha kamwe !! People are dancing according to the tunes !!!
Jibu hoja ya msingi kwa kulinganisha na wale wa CUF. Hii double standard hata wewe inaweza kukuathiri.
 
Kwani mahakama imelitaarifu bunge kuwa kuna kesi? Ushahidi uko wapi? Kwani unapopewa adhabu ukakata rufaa, adhabu inasimamishwa kwanza kusubiri rufaa?
Maadam jambo hili limefika mahakamani, ngoja mahakama itoe maamuzi ya mwisho wasije kusema wameonewa.

It is the last kicks of a dying horse.
 
Kuna uzi wa Ushimen ulisema hili na nilicomment kuwa mwisho wa siku kisingizio kitakuwa mahakama. Hii nchi ni rahisi sana kuitabiri.
Kwenye hili linchi, ukiwa umekula na kushiba tu, inatosha kumjua streringi wa sinema hata kabla haijaanza...😂
 
Vuuup huko mahakamani wanapigwa tena na kitu kizito... Bwana Zitto akae tayari kupokea ugeni
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]
Hao unaowasema hawakwenda mahakamani ukienda mahakamani inabd usubiri
 
Kuna mambo yanahitaji kutumia busara kutatua jambo,sio kusingizia mhimili.

Ingekuwa bora mjifiche hata kwa kuwasimamisha ubunge wakisubiri hatima ya mahakama.Kama wamefukuzwa uanachama wanaingia bungeni kwa tiketi gani?

Maridhiano,maridhiano,maridhiano bila weledi wa haki.
 
Ninachojua na utabiri wangu ndivyo utakavyo kuwa

♦️ Halima ni mwanasheria na anajua kabisa ground za judicial review

♦️ Bila shaka kuna sehemu amewategeshea waka kosea procedure hasa kwenye Natural Justice ya Audi alteram partem

♦️ Mahakama itaaikiliza shauri hilo la judicial review haraka iwezekanavyo na kwa sababu suala la natural justice denial lipo wazi mahakama itaiamuru chadema kulirudia shauri lao DE NOVO

♦️ Kwa misingi hiyo litaanza upya kabisa na kama.hawataridhika tena watakata rufaa kwenye ngazi ya chama na kama watakuwa aggrieved tena wataenda mahakama kuu

♦️ Watacheza na hizo technicalities ad infinitum mpaka uchakuzi ufike
 
Swala sio mahakama ila ni uhuni wa Mbowe ....anajua kila kitu kinavyokwenda na hata mkutano mkuu ulipo kaa juzi hakuruhusu kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati kuu ila walibariki maamuzi yaliyovunja katiba yao wenyewe... akijua kabisa wataenda mahakamani na yeye kama mnufaika ataaendelea kupata fedha za kuendeshea chama na shughuli zake. So stay tune.
Tukiwaambia hiki chama ni cha kihuni muwe mnaelewa
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo?...🥺
Hao waliofukuzwa vyama vingine walienda mahakamani?
 
Back
Top Bottom