Sio mzee Ndugai; ni Canon Ndugai.Wamrudishe Mshauri wa Askofu mkuu wa Canterbury mzee Job Ndugai
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio mzee Ndugai; ni Canon Ndugai.Wamrudishe Mshauri wa Askofu mkuu wa Canterbury mzee Job Ndugai
Kitu kikiharibika kinatakiwa kirekebishwe haraka sio kukiharibu zaidi ilhali Mamlaka yote ya kukirekebisha unayo !! Ukiona huwezi unawapisha wanaoweza !! Wazungu Wanasemaga To fall down is an accident but to stay down is a choice !! Acheni visingizio watu waadhibiwe wanaoiba mali za Umma !!Jiwe kaiharibu sana hii nchi, sijui tulikosea wapi
Nakubaliana na wewe mkuuYule spika alishasema Rais halazimishwi kufuata ushauri wa bunge. Sasa wananchi maslahi yao yatalindwaje?. Huyo spika ni kibaraka wa Ikulu bungeni.
Kweli kabsa hata nje ya chama tutawatema tu hakuna wanalofanya, wanadhani sisi hatuoniHiyo jeuri hawana! Kwanza 95% next uchaguzi wanatupwa nje maana walibebwa na JPM. Bora wajijengee heshima wapiganiwe na wananchi lakini kwenye chama hawatoboi.
Mazoea hujenga tabia.Huyo spika alizoea bunge lenye wapinzani, na akawa kazi yake ni kuwakomoa kwenye kila hoja yao. Matokeo yake tabia ile imegeuka kilema kwake, hivyo kila mwenye hoja kinzani na serekali kwake ni kumzuia tu. CCM vumilieni upuuzi mlioulea kugeuza bunge kuwa chombo cha kuikinga serekali, badala ya kuisimamia na kuiwajibisha.
Tatizo sio Spika tatizo lipo kwenye Katiba !! Rais ndio kila kitu ! Atakachoamua ndicho kitakachokua hata Spika mstaafu anajua hivyo !!Kwanini wapoteze muda...badala waendelee na kujadili bajeti za wizara, mm binafsi naona speaker wetu yupo sahihi
ni tanzania sio kenyaLabda kama ni wabunge wa Kenya au Zambia,lakini hapa kwetu ni ndoto ya mchana,amka unaweza kukojoa kitandani.
Hoja hizi nyepesi sana, sio za kumng'oa spika. Anyway, ngoja tuone. Nitaamini tu endapo akitolewa uspika.Kuna tetesi kuwa baadhi ya wabunge wamejipanga kuwasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya kuonekana wazi kushindwa kuuongoza mhimili huo kwa manufaa ya watanzania.
Hatua ya wabunge hao inakuja baada ya Spika kuzima ajenda za wananchi ambapo baadhi ya wabunge walitaka masuala hayo yajadiliwe bungeni yeye akayazuia yote wengine wakimlaumu kuwa ana mgongano wa maslahi na ya kifamilia kutokana na mumewe kuwa boss wa ewura
(i) Hoja ya kujadili Ripoti ya CAG (Mhe. Ole Sendeka)
(ii) Hoja ya kujadili uvamizi wa tembo kwa wananchi( Mhe. Bahati)
(iii)Hoja ya tatizo la mbolea na kufutiwa leseni mawakala wa mbolea( Mhe. Msambatavangu)
(iv)Hoja ya ajira kutolewa kwa upendeleo (Mh. Mwita Waitara)
Hili si bunge la wananchi ni bunge la Chama Cha Mapinduzi.Spika anapozuia bila kutoa maelezo ya maana huwa ana maana gani? Yeye anasimamia bunge la wananchi wa Nchi ya Wapi?
Aka la mwenda zakeHili si bunge la wananchi ni bunge la Chama Cha Mapinduzi.
Kwa CCM ni kuishia hadithi za alinachaKuna tetesi kuwa baadhi ya wabunge wamejipanga kuwasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya kuonekana wazi kushindwa kuuongoza mhimili huo kwa manufaa ya watanzania.
Hatua ya wabunge hao inakuja baada ya Spika kuzima ajenda za wananchi ambapo baadhi ya wabunge walitaka masuala hayo yajadiliwe bungeni yeye akayazuia yote wengine wakimlaumu kuwa ana mgongano wa maslahi na ya kifamilia kutokana na mumewe kuwa boss wa ewura
(i) Hoja ya kujadili Ripoti ya CAG (Mhe. Ole Sendeka)
(ii) Hoja ya kujadili uvamizi wa tembo kwa wananchi( Mhe. Bahati)
(iii)Hoja ya tatizo la mbolea na kufutiwa leseni mawakala wa mbolea( Mhe. Msambatavangu)
(iv)Hoja ya ajira kutolewa kwa upendeleo (Mh. Mwita Waitara)
Walitaka bunge la aina hiyoAka la mwenda zake
Kabisa mambo yanazidi kuwa magumuKiukweli yanayoendelea bungeni yanasikitisha sana.
Natamani Watanzania waamke kutoka usingizi wa pono tuwavue UWAZIRI mawaziri wote kudadeki.
Yaani jinsi Ndalichako alivyotetea KIKOKOTOO na Jenista Mhagama alivyotetea ajira ambayo ilikuwa hoja ya Esther Matiko INAUMIZA SANA.
Bunge kaputi haliwezi kukohoa kitu kama hichoWabunge wa ccm hakuna kitu kama hicho