Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo

Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo

Kama kuna jambo la muhimu na lenye kuakisi upendo wa chama kwa wanachama na viongozi wake ni hii hatua ya kuwaepusha na maambukizi. Wameongea na kutimiza waongeacho.

Bravo Chadema top leaders, bravo chadema MPs
 
Usimkufuru Muumba Kwa sababu ya tofauti za itikadi! Na hata ikibidi kukufuru, usiwatakie uzao wako laana zisizo na sababu! Kwanini ujiapize kwa mambo madogo tu haya, ambayo ni tofauti za kimtazamo tuu?!
Hahaha unaimani kali ndugu!!
Lakini ndo hivyo usiyaweke sana rohoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila chadema kama chama kina drama nyingi hiyo karantini badala ya kuwasaidia imezidi kuwagawanya mpaka wamefukuza wabunge wao ingawa utekelezaji ni mgumu wamejulikana wamechukua pesa bila kufanya kasi ambalo ni kosa kubwa kisiasa na wamewapa faida wapinzani wao
 
Hapa ndio nimeamini chadema ni kundi la wajinga na waliteleza kuondoka bungeni maana hata korona bado haijakwisha na sidhani kama wamepima kujiangalia kama wana Corona au lah!

Halafu chadema watwambie bungeni ni salama au lah? Maana mwanzo walisema siyo salama kabisa!

Wanatwambia kuwa bungeni ni salama sasa na walifanya makosa kukimbia?

Sent from my iPhone using Tapatalk
Chief unachanganya sana hapa, hatua zilizochukuliwa na chadema ni mbili muhimu;
1. Kwanza kujua hali zao kiafya, katika hili walihitaji kufuata taratibu za WHO kujitenga na umma kwa siku 14 ili kusubiri dalili za COVID-19 kudhihiri. Hili wamemaliza na sasa wanauhakika kwamba wapo salama hivyo kinacho hitajika ni kujikinga dhidi ya wagonjwa wasiojulikana.

2. Kuepuka maabukizi kwa watu wengine, kwasababu hawakujua hali zao na kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wabunge wenzao walikuwa wamefariki katika siku kadhaa nyuma hivyo hofu ya wao kuwa ni waathirika ilikuwa kubwa na hivyo kama wangeendelea kujumuika na wengine hatari ya kuwaambukiza ilikuwa kubwa sana.

Sasa wanauhakika hawana maambukizi kwa asilimia 100. Wanarudi bungeni kujumuika na wabunge ambao hawajui hali zao, kazi kwao itakuwa ni moja tu! kujilinda dhidi ya mmabukizi.
 
Ni Jambo jema japo kimsingi kuna mambo yameshawapita hasa hotuba za Kambi ya Upinzani kutokuwasilishwa, hili ndilo lilikuwa kosa kubwa sana na nasikitika kwanini mlilipuuza maana wananchi wamekosa uwakilishi ambao wengi wetu tunategemea kambi ya Upinzani wangekuwa wawakilishi wetu
Kwanza hotuba zao siku zote hukataliwa, wala hawajapoteza kitu; pia mawazo yao mazuri hupuuzwa; hadi chama cha wajinga kitoke madarakani ndo kambi ya upinzani itakuwa na maana bungeni! Ilikuwa muhimu kulinda afaya zao, haina haja kugang'ani na kuishia kufa eti unatetea wananchi! Sijui nani anawatetea wananchi waliokuwa wanatetewa na Mahiga?
 
Makene WHO wameshasema COVID-19 is here to stay! Acha ngonjera mkuu. Pia waambie hao wabunge 14 waliotajwa na Spika warudishe pesa zetu!
WHO wenyewe wanasisitiza self isolation! Alotoa hilo wazo ni mmojawapo tena kwenye twitter account yake, si official statement ya WHO! Soma na sikiliza habari kijana!
 
Kwan vpmo c vinachunguzwa au umeamka nayo ?
Hapa ndio nimeamini chadema ni kundi la wajinga na waliteleza kuondoka bungeni maana hata korona bado haijakwisha na sidhani kama wamepima kujiangalia kama wana Corona au lah!

Halafu chadema watwambie bungeni ni salama au lah? Maana mwanzo walisema siyo salama kabisa!

Wanatwambia kuwa bungeni ni salama sasa na walifanya makosa kukimbia?

Sent from my iPhone using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu chadema watwambie bungeni ni salama au lah? Maana mwanzo walisema siyo salama kabisa!
haya chadema jibuni swali bunge sasa ni salama kuliko kabla hamjaondoka? kama mnaliona kwa sasa ni salama ni kwa vigezo vipi mumetumia? leteni jibu
 
Hapo na mimi ndo nashangaa. Kwanini waende kujumuika nawabunge wengine mjengoni ambao bado hawajapima? Sasa hapo utakuwa umefanya nini?
mkuu katika chama wa upinzani pumbavu kuliko vyote dunia chadema inaongoza ikiwa chini ya Mbowe sio chama hiki ni kundi la wajinga fulani waliorundikana kwa mwavuli wa chama.Tatizo mwenyekiti na katibu mkuu elimu hawana .ujuaji bila elimu una mwisho.Hayo ndio matokeo yake
 
Keyword kwenye hotuba ya Mnyika :“Wabunge wetu wote waliotekeleza makubaliano na uamuzi wa Chama na Wabunge wa kujitenga kwa siku 14 ambayo yanatokana na maelekezo na ushauri wa Wataalamu wa afya ikiwemo WHO,” Yaani huo ni utetezi tosha mbele ya dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
WHO iliwahi toa maagizo kwa nchi gani au chama gani kwenda karantini? ??
 
Nasubiri kuona Chadema ina nguvu na mamlaka gani yakutoa amri kwa muhimili huru kama wa Bunge.

Zaidi ya yote hawa ni wa kutengwa sababu tangu wameondoka hakuna maambukizi mapya bungeni.
 
Wabunge wote wa Chadema ambao hatimae wamehitimisha siku 14 za kujitenga (self isolation) kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli za Bunge, vikiwemo vikao vya Bunge, ndani ya ukumbi na kamati zake katika maeneo mengine ya mhimili huo, leo Ijumaa, wanatarajiwa kurejea bungeni kuendelea na majukumu yao, baada ya kuwa na uhakika kuwa hawana maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19.

Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika (Mb) amesema kuwa Wabunge wa Chadema waliotekeleza uamuzi wa makubaliano ya Chama na wabunge, ya kujitenga kwa kutofika maeneo yote ya Bunge, walitekeleza masharti na ushauri unaotolewa na wataalam wa masuala ya afya kuhusu namna bora ya kujikinga au kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona, miongoni mwa watu hasa inapotokea mahali walipo zipo taarifa kuwa kati yao kuna maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID19.

"Wabunge wetu wote waliotekeleza makubaliano na uamuzi wa Chama na Wabunge wa kujitenga kwa siku 14, ambayo yanatokana na maelekezo na ushauri wa wataalam wa afya, likiwemo Shirika la Afya Duniani, kwa sasa, kuanzia leo, watarejea bungeni kuendelea na shughuli za kuwawakilisha wananchi, huku wakiendelea kuzingatia tahadhari zote za kujikinga wao na kuwakinga wengine wakiwemo wabunge wengine, Watumishi wa Bunge na wananchi wetu," amesema Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Mnyika.

Itakumbukwa kuwa Wabunge wa Chadema walianza kutekeleza makubaliano hayo tarehe 1 Mei, mwaka huu, baada ya kuwepo kwa taarifa za maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19 katika maeneo ya Bunge, hususan miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo siku hizo 14 zinazoelekezwa na wataalam wa afya zimemalizika jana na sasa wana uhakika na afya zao dhidi ya maambukizi ya COVID19.

Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Mnyika ameongeza kusema kuwa msingi wa makubaliano hayo, unatokana na maelekezo na ushauri wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo yamethibitisha kuwa, kujitenga (self isolation) ni mojawapo ya njia muhimu zilizothibitishwa kisayansi katika kuzuia au kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa sababu inasaidia kuvunja au kupunguza muingiliano wa watu.

Imetolewa leo Ijumaa, Mei 15, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

View attachment 1450788
View attachment 1450789
Kwani korona imeisha mpaka warudi
 
Kichekesho walikimbia bungeni kwa madai ya kwenda kukaa karantini Sasa wanarudi bungeni kwenye bunge lile lile ambalo asilimia kubwa karibia wote hawajakaa karantini ukiondoa hao 15 wa chadema je huoni Ni utoto na usanii tu walio ufanya? Kama walikimbia maambukizo mbona wanarudi Tena wakati wabunge walio baki hawakuacha bunge Wala hawajapimwa Wala hajakaa karantini swali si wataambukizwa Corona Sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom