Umarufu wa siasa za Tanzania, hutafutwa kwenye vitu vya Kipumbavu Sana,
Lengo la hili nalo, ni kujitafutia umarufu, ambapo ni Ujinga Tu,
Mfano, Nchi nzima hakuna aliyeko lockdown, Wakati raia wa kawaida wakiendelea na majukumu bila uwoga, wakikwepana na vitu vya hatari, wakihatarisha uhai wao na ili tu, walipe Kodi, Kodi ambazo zinaenda kuwalipa hao viongozi wetu na wabunge ambao wanakimbia kazi za wananchi,
Hii Mimi nimetafakari Sana, akiri yangu ikanifundisha vitu vingi na vingine vya kunitia hasira kama mwananchi na mpiga Kura,
Wakati wabunge walipochukua hatua ya kwenda kujifungia, Je, walikuwa ni waathirika kama ambavyo wengine wamekuwa wakitengwa Kwa sababu wameambukizwa na Corona?
Na kama haikuwa hivyo! Je walikwenda lockdown ya namna gani hiyo?
Maana yake, Ni kuwaambia hasa wananchi ambao wamewachagua na wakiendelea kufanya kazi ktk mazingira hayo ambayo wao wameyakimbia na huku wakiendelea kulipa Kodi ili wabunge hao wapupule mishahara minono kwamba, Wao ndio wanaostahili kufa Kwa sababu maisha Yao hawana uwezo wa kujikarantini kama wao siyo?
Okey, Hilo tuliache,
Je sasa Corona imekwisha sasa?
Wanarudi bungeni kulekule walikokukimbia kwamba kule kumejaa maambukizi, kumebadirka nini huko leo?
Ni kweli tunapendana na kuwapenda wawakilishi wetu, lakini kunamambo wanafanya ambayo kiujumla yanahitaji tuwaulize na pengine waone misimamo yetu, si kila watakalolitengeneza wakalifanyia kazi linahitaji kuungwa mkono, no! Natamani tufikie kwenye level ya juu kabisa ya siasa zetu, za kutokuogopana na kupeana sifa tu Kwa kila kitu,
Tukifikia hapo, tutakuwa tumejikomboa Sana,
Na mwisho, Tunataka Katiba mpya ya wananchi wote, na sio ya viongozi na kulinda Vyama,
Tunataka wabunge tuwe tunawaadhibu na kuwakataa Sisi wananchi na si Vyama vyao kuwafukuza wabunge wetu hata kipindi Ambacho wananchi Tunawapenda na tunawahitaji
Wananchi ndio tuwe majaji Kwa wabunge wetu, tuwatimue hata katikati ya mihula Yao, Vyama kutimua wabunge wetu bila lidhaa yetu tuliowachagua ni unyanyasaji wa wawazi kabisa