Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Solution ni Makao makuu ya mkoa wa Geita yahamishiwe Chato halafu mkoa wa Geita ubadilishwe jina uitwe CHATO.

Ombi la muombolezaji aitwae Bigambo litakuwa limeshatekelezwa bila ya kuwaathiri Wana KAGERA
We jamaa ni bonge la SOLVA.
 

Sasa huu mkoa mpya si utaitwa UMASIKINI
 
Sasa unachopinga ni nini. Kiburi kipo wapi hapo uliponukuu
 
Watoe hizo wilaya zinauangusha mkoa wa kagera.

Yaan biharamulo 60% wako chini ya dola
Wawapeleke wapi ndugu zenu[emoji23][emoji23] na wakiondolewa ndo mtakua matajiri ama? Mbona mnajiongopea sana? Kama ni huduma serikali ilitakiwa iwasogezee na siyo kutengeneza mkoa mpya. Hizo ni extra expenses za administration. Ujinga kbs huu. Halag kisa matakwa ya jiwe. Kumbafu kbs. Kila mahali wana haki ya kupata huduma zote. Kila mtu anastahili kupata mahitaji muhimu. Serikali iache ubabaifu. Kuunda mkoa mpya siyo solution. Kama ni huduma wasogezewe. Idiots kbs

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Wana kagera msikubali mnaamishwa chato, huko ni kuharibu historia ya mkoa wenu ilianza kumegwa biharamulo na sasa ngara, kisa interest za kiongozi mubinfasi.
Acha wajitenge maana wasubi, wahangaza, nk wamebaguliwa sana na hao akina nshomire......
Uzuri wa ubaguzi huwa hauishii kwenye "wapemba na waunguja" ndani kabisa kuna wanyambo, waziba, wahamba, wanyaihangiro, wahyoza, waendangabo, nk!
 
Jamani mi nauliza: Kama jiwe agekuwepo hao wabunge wangethubutu au hata kufikiria kupinga??
 
Sijapinga mkuu.

Cha msingi ni wamemaanisha kwamba Kagera is not for Charity. Na hii ndio kibri ya kihaya.
Sio kiburi. Mkoa huu ushatengwa hapo kabla sasa unatengwa tena kisa kuna marehemu alijenga International Airport porini na miundombinu isiyo ya lazima kusiko na uhitaji. Mikoa mikubwa Tanzania hutoweza kuikuta Kagera, kwanini isivunjwe hiyo ili kurahisisha huduma. Kwahiyo kila rais akifa wilaya yake tunaifanya mkoa?

Huyohuyo ndio alitaka Dar ivunjwe mjini ianzie wapi sijui. Ethiopia na Nigeria walianza hivi hivi kila anayechaguliwa anaangalia kwao
 
1.Kwa hiyo mkoa wa Kagera una wabunge watatu???
2. Lini hao wabunge watatu wakawa wasemaji wa wananchi wa mkoa mzima??
3. Kama vikao vya halmashauri husika za biharamulo na ngara zilipitisha wao wanatoka wapi??
4. Katika madai yao mbona hatuoni hata mbunge mmoja wa hizo wilaya??
5. Unaanzaje kusema biharamulo ndo nguzo ya uchumi wa Kagera wakati ndo wilaya maskini zaidi Tanzania???
6. Unaanzaje kusema eti biharamulo ikiondoka Kagera aanakag
 
Hawana ubavu wa kuigomea CCM kama itaamua kuipa Chato hadhi ya kuwa Mkoa (Manispaa) , kwa hiyo hata kama hoja zao zina mashiko ila chama ndicho kinaongoza Serikali na ndicho kitamuua.
 
Madini na hasa dhahabu inayochimbwa Biharamulo, nk .....wanasiasa huwa wanaangalia matumbo yao tu!
 
Mkoa ukigawanywa makao makuu yawe Lusahunga ili hizo huduma ziwe karibu na wananchi wote, Chato, Kakonko na Ngara. Kuweka makao makuu Chato ni kuwaonea wengine na mantiki ya kusogeza huduma kwa wananchi inakuwa haipo.
 
Mimi sioni mantiki ya kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya. Kwenye technologia ya kisasa ya e-government, e-banking, e-farming, e-courts nk. hoja ya ukubwa wa eneo haina mashiko kabisa. Haya sasa kama hoja ni ukbwa basi Tabora igawanywe iwe mikoa mitatu!
Mbona Marehemu Ben Mkapa (RIP) aliwahi kusema nchi hii ni kubwa sana - mbona hamkufikiria kuigawanya mkaanzisha nchi nyingine ndani ya nchi hii kubwa?.

Hoja ya Chato kuwa mkoa haina mashiko - je makao makuu yatakuwa wapi? Utasikia wana Chato wanasema tunao uwanja wa ndege, tunayo hospitali inajengwa kubwa, kwa hiyo makao makuu yawe Chato. Huyu wa Kakonko umemsaidiaje? Umbali kati ya Geita na Chato ni kiasi gani?

Rais Samia achana na watu wa aina hiyo, hizo gharama za kuanzisha mkoa mpya zitumie kujenga barabara za vijijini kwa kiwango cha lami ili mazao yasafafirishwe kwa urahisi.

Hata hii hoja ya kujenga maghorofa makubwa ya mawizara huko Dodoma, wakati vijijini barabara ni mbovu, haina mashiko. Eti mnajenga ofisi ya ghorofa sijui 6 kwa wizara - mnataka kupangisha?
 
Mm naona watu wa humu wanaotetea mkoa mpya wa CHATO kuanzishwa ni Zero brain kama wazo hili lilikuwepo muasisi alishindwa nn kuiimarisha Kagera kwanza katika miundombinu ikijumuisha stand ya mabasi ya kisasa, barabara, uwanja wa ndege na taasisi za serikali ziwe za kisasa ndio aanze program ya mkoa mpya!

Ubaguzi kwa hapo naona mhaya hana ila watu wana chuki binafsi na wahaya ila kiuhalisia mkoa wao umechoka sana. Si busara kuanza kipya cha zamani ukakitupilia mbali. Mbaguzi ni yule aliyeelekeza hela za rambirambi za tetemeko la ardhi la mkoa huo sehemu nyingine, kama angewekeza hela yote iliyopatikana kwa mkoa husika hawa watani zangu wasingekuwa wanalalama hadi sasa mana wanaonekana bado wana kinyongo sana na kuhisi kutengwa.

Pia kiusalama wana hoja hapo Kuna vinasaba vya aina mbili vitatengwa yaani warundi na waganda ule mchanganyo uliokuwepo ulikuwa na mantiki sana katika kupata taarifa sahihi ya wakazi asili wa maeneo husika.
 
Mkuu hebu ziangalie na pesa zilizopotea kwenye mchakato wa katiba mpya,mbona huzioni au ziliokotwa,au zilitoka kwenye mifuko ya watawala?
Hiyo miradi nayo ife tu,ndipo mtaona umuhimu wa katiba mpya.
Nchi inapelekwa kokote anakotaka mtawala.

Subirini,baada ya miaka mitatu mtaiona zenji ikipaa kimaendeleo

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Si alisema atahamia Kagera, ndo wajue mwenzao aliishachora ramani

Wakiamua wafute Kagera iwe Chato tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…