GE2025 Wabunge wa sasa waliokatwa kugombea CCM hawa hapa

GE2025 Wabunge wa sasa waliokatwa kugombea CCM hawa hapa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Geoffrey Mwambe ni mwamba ila kakatwa jamani,alikuwa waziri mchapakazi kipindi cha jiwe, alikuwa wizara ya uwekezaji kama sikosei.
 
Hivi Makamba ana kimavi gani mbona huwa hana damu ya kibali hata akibebwa anamwaga?....anawakosea wapi bosses?
Japo mimi sio mwanahabari wa uchunguzi ila ninaweza kuunganisha visa kadhaa kuhusu makamba Jr....na uchambuzi mfanye nyie.....mimi natoa assist tu....
Samahani hivi visa havina mtiririko.

1.kwanza Magufuli alimpa wizara ndogo ambayo Makamba hakuridhika nayo.

2. Magufuli akamtumbua akawa mbunge wa kawaida.

3. Makamba, Nape, Ngereja, na Kinana wakadukuliwa sauti zao wakipanga mikakati ya kukabiliana na Magufuli ndani ya Ccm.

4. Samia anaingia madarakani na falsafa ya kurejesha Umoja na mshikamano ndani ya CCM....anawateua Pro-Magufuli na Ant-Magufuli serikalini wafanye kazi pamoja ili kuleta harmony.

5. Makamba na Nape wanarejeshwa kuwa mawaziri..Ridhiwani naye ndani...Kinana anarudishwa CCM.
Mama aliamini hawa vijana walionewa tu.

6.Makamba na naibu wake Byabato wanahamishiwa foreign affairs.

7.Mkumbuke Makamba, Nape na kinana ni inseparable...wanaelewana sana hawa....ukaribu ule ukaanza kumuingiza Byabato ndani mdogomdogo.

8. Nape anaonekana Bukoba mjini akiwa na Byabato Naibu wa rafiki yake Makamba wakiwa Kashai, Nape anamuhakikishia Byabato atamsaidia kushinda uchaguzi hapo Bukoba.

9. President Samia anafanya mabadiliko madogo ya mawaziri usiku....anawatema Makamba, na rafiki yake Nape hata Byabato anaunganishwa humohumo.

10.Baada ya Makamba na Nape kutemwa Haikuchukua muda kinana nae anaomba kujiuzuru.

Kuna untold story nyingi za makamba nyingi ikiwemo kufanya mikakati ya siri ili apendekezwe kuwa mrithi wa Philip mpango...akiamini kuwa akiwa makamu wa rais kwake itakuwa rahisi kuupata urais kwa njia za kimjini mjini kabla ya 2030.
 
Hawa ni wabunge wa sasa ambao CCM imewapumzisha.

1. Mrisho Gambo - Arusha Mjini
2. Stephen Byabato - Bukoba Mjini
3. Luhanga Mpina - Kisesa
4. Ndaisaba Ruhoro - Ngara
5. Josephat Gwajima - Kawe (Hakuchukua fomu)
6.Yusuph Makamba - Bumbuli
7. Nicodemus Maganga - Mbogwe
8. Christopher Ole Sendeka - Simanjiro
9. Pauline Gekuli - Babati Mjini
10. Angelina Mabula - Ilemela
11. Seif Gulamali - Manonga
12. Justine Lazaro Nyamoga - Kilolo
13. Vedastus manyinyi mathayo - Musoma Mjini
14. Cecil Mwambe - Ndanda
15. Geoffrey Mwambe - Masasi mjini
16. Godwin Kunambi-Mlimba
17.

update

Unaweza kutazama orodha nzima katika uzi huu hapa - LIVE - Kamati Kuu CCM yafanya maamuzi, majina ya watia nia Ubunge yanatangazwa muda huu
No 6. Nadhani ulimaanisha January Makamba.
 
Back
Top Bottom