Wabunge waliofukuzwa CHADEMA wapo Bungeni leo Juni 23, 2022, Spika kawaruhusu kuuliza maswali

Wabunge waliofukuzwa CHADEMA wapo Bungeni leo Juni 23, 2022, Spika kawaruhusu kuuliza maswali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FV6utnwWIAAxHuc.jpg

FV6utnwXEAQeczC.jpg
Wabunge wa Viti Maalum, Salome Makamba na Grace Tendega wapo Bungeni, leo Alhamis Juni 23, 2022 na wameuliza maswali ya nyongeza baada ya kupewa fursa hiyo na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

Wabunge hao walifukuzwa uanachama CHADEMA na kesi waliyofungua kupinga kufukuzwa Mahakamani imetupwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam.

Pia soma - Chadema yadai kwamba iliwasilisha Kwa Spika wa Bunge Taarifa ya Mdee na wenzake kushindwa kesi mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama

Tujikumbushe Wabunge hao 19
Halima Mdee
Esther Matiko
Grace Tendega
Cecilia Pareso
Ester Bulaya
Agnes Lambart
Nusrat Hanje
Jesca Kishoa
Hawa Mwaifunga
Tunza Malapo
Asia Mohammed
Felister Njau
Naghenjwa Kaboyoka
Sophia Mwakagenda
Kunti Majala
Stella Flao
Anatropia Theonest
Salome Makamba
Conchesta Rwamlaza
 
Kuna mwanasheria nilimsikia anasema kesi haijatupwa ila kuna sehemu walikosea kuandika hivyo wanaruhusiwa kufanya marekebisho na kuifungua tena
 
Wanataka sasa aibu iwakute
Nadhani ile taarifa ya maamuzi ya mahakama ya jana itakuwa haijafika kwa spika. Tu assume kuwa maamuzi yale yalisomwa jana mchana na ni Dar, na hao matapeli wanajua taarifa haijafika bungeni na ushiriki wao wa leo utawaingizia sitting allowance na night allowance ya mwisho jee kwa njaa hii wanaweza kuacha?
Kesho hawaji.
 
Sio kila Mwanasheria ni wa kumsikiliza. Akina Halima Mdee walifungua maombi ya kutaka mahakama kuu ipitie maamuzi ya CHADEMA. Mahakama imetupilia mbali maombi hayo kwa kuwa CHADEMA sio public body iliyo subject to judical review.
 
Spika bado hajapokea Maamuzi Kimaandishi.... Anasikia tu juu juu Mitandaoni...!
Wajanja kama mie hawateseki wanaendelea kumwagilia moyo na vitu bardiiiiiii..!
Hilo ni kweli kabisa kwa sababu Spika hakuwa mmoja wa washtakiwa!! Lakini ni yeye pia alisema kwa mdomo wake kuwa hatawaondoa wabunge hao kwa kuwa amepata taarifa kuwa wamefungua kesi mahakamani. Busara inamtaka awaache bungeni mpaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakapoifahamishe Tume ya Uchaguzi uamuzi wa mahakama. Au pale Chadema itakapopeleka majina ya wanachama wa kike 19 kama wateuliwa wa ubunge kwa NEC.

Kwa jinsi nchi yetu inavokwenda kwa sasa, nachelea kusema jambo hili litaingia phase mpya na ambayo haikutarajiwa - ya Spika kusubiri maamuzi ya NEC ambayo hayatakuja kwa sababu kesi iliyofunguliwa na akina Mdee ilikuwa ikiishitaki NEC pia. Ni lini NEC itasema kwa Spika viti 19 vya Chadema viko wapi? A billion dollar question!!

Endelea kunywaga hiyo kitu baridi kwa koo, mkuu!!
 
Back
Top Bottom