Wabunge waliofukuzwa CHADEMA wapo Bungeni leo Juni 23, 2022, Spika kawaruhusu kuuliza maswali

Wabunge waliofukuzwa CHADEMA wapo Bungeni leo Juni 23, 2022, Spika kawaruhusu kuuliza maswali

Spika anawalia wazo, kwamba awaandikie barua watamshiki, kwamba awaambie tokeni humu ndani, kamati ya maadili itamjia juu, sasa anatafuta mwongozo nchi nyingine
 
😁😁😁
16554546876670.jpg
 
Kosa siyo lao! Kama sikumsikia vibaya Mnyika alisema Mwanasheria wa Serikali ndiye anapaswa kuwasilisha barua kwa Spika kumweleza maamuzi yaliyofikiwa na Mahakama kuhusiana na hao C-19! Baada ya hapo ndiyo Spika atachukua maamuzi.

Spika alikuwa ameshtakiwa ndio maana aliwakilkshwa na mawakili wa ofisi ya mwanasheria mkuu.

Kitendo cha mawakili wa serikali kuwepo mahakamani maana yake ni kwamba Spika alikuwepo mahakamani.

Kwa msingi huo Spika hawezi kudai hana taarifa. Ni sawa na Chadema waseme hawaba taarifa wakati mawakili wao walikuwepo mahakamani.

Pia Halima na wenzake hawapaswi kuwa bungeni baada ya mahakama baada ya mahakama kutupilia mbali kesi yao. Wanachofanya sasa ni dharau mbaya sana kwa mahakama.

NB:

Jaji anapoingia mahakamani huitisha majina ya pande zinazohusika na kesi. Msingiwa kufanya hivyo ni kuhakikisha kila upande umesikilizwa, na kila upande una taarifa maamuzi yanapotoka.
 
The judiciary has spoken the ball is firmly in Tulia's court -do nothing,do something or do the right thing. Tanzania is waiting na matumaini mapya.
 
Niliwaambia Chadema mapema leo kwamba sijaona pahala Jaji wa Mahakama kuu alilosema Halima Mdee na wenzake siyo wanachama halali wa Chadema.

Sass naona akina Halima Mdee wako bungeni kama kawa

Nchi ngumu sana
 
Nadhani ile taarifa ya maamuzi ya mahakama ya jana itakuwa haijafika kwa spika. Tu assume kuwa maamuzi yale yalisomwa jana mchana na ni Dar, na hao matapeli wanajua taarifa haijafika bungeni na ushiriki wao wa leo utawaingizia sitting allowance na night allowance ya mwisho jee kwa njaa hii wanaweza kuacha?
Kesho hawaji.

..Spika alikuwa sehemu ya washtakiwa.

..Na aliwakilishwa au alikuwa akitetewa na mawakili wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

..kwa msingi huo Spika hawezi kusema hana taarifa za hukumu iliyotolewa.

..pia mwanasheria mkuu wa serikali, ambaye ofisi yake ilituma mawakili kumtetea Spika, anashiriki vikao vyote vya bunge kutokana mamlaka yake.

..kinachoendelea hapa ni DHARAU kwa mahakama. Tunajenga tabia ambayo itakuja kutuletea matatizo.

Cc Petro E. Mselewa
 
..Spika alikuwa sehemu ya washtakiwa.

..Na aliwakilishwa au alikuwa akitetewa na mawakili wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

..kwa msingi huo Spika hawezi kusema hana taarifa za hukumu iliyotolewa.

..pia mwanasheria mkuu wa serikali, ambaye ofisi yake ilituma mawakili kumtetea Spika, anashiriki vikao vyote vya bunge kutokana mamlaka yake.

..kinachoendelea hapa ni DHARAU kwa mahakama. Tunajenga tabia ambayo itakuja kutuletea matatizo.

Cc Petro E. Mselewa
Hivi mwenyekiti atajishtaki Kwa Nan?
 
Mkuu huyu alikuwa Prof na naibu AG!

Sikiliza video anasema mahakama ikisema anatekeleza. Hiyo ilikuwa wakati wanafungua kesi
Kwa anasubiri nini? Mahakama imesema

Yaani anaongea tu utadhani ni mtu wa mitaani
Haya ni madhara ya utawala wa Magufuli ! very disturbing
 
Wabunge wa Viti Maalum, Salome Makamba na Grace Tendega wapo Bungeni, leo Alhamis Juni 23, 2022 na wameuliza maswali ya nyongeza baada ya kupewa fursa hiyo na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

Wabunge hao walifukuzwa uanachama CHADEMA na kesi waliyofungua kupinga kufukuzwa Mahakamani imetupwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam.

Pia soma - Chadema yadai kwamba iliwasilisha Kwa Spika wa Bunge Taarifa ya Mdee na wenzake kushindwa kesi mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama

Tujikumbushe Wabunge hao 19
Halima Mdee
Esther Matiko
Grace Tendega
Cecilia Pareso
Ester Bulaya
Agnes Lambart
Nusrat Hanje
Jesca Kishoa
Hawa Mwaifunga
Tunza Malapo
Asia Mohammed
Felister Njau
Naghenjwa Kaboyoka
Sophia Mwakagenda
Kunti Majala
Stella Flao
Anatropia Theonest
Salome Makamba
Conchesta Rwamlaza
Msisahau hata huyo spika ni product ya ukatili na wizi wa kura wa meko.

Mambo sio marahisi kama mnavyodhani

Hapo kanasubiri barua ya mahakama
 
Back
Top Bottom