Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Huwa nakereka sana hawa jamaa wanaochambua soka la bongo wanavyopambana kufa na kupona kuongea kiingereza. Hivi hawawezi kuchambua mpira bila kuingiza hivyo viingereza vyao vya ugoko?

Badala ya kusema "Value" kwa nini wasiseme thamani?

Badala ya kusema "Flanks" kwa nini wasiseme eneo la kulia au kushoto?

Badala ya kusema "assists" kwa nini wasiseme amesaidia wengine kufunga?

Na vingereza vingine vingiiiiiiiii!!
 
Hii ni moja ya sababu za mimi kuacha kusikiliza vipindi vya michezo
Wanatumia nguvu kubwa sana kuongea lugha ambayo dhahiri shayiri, inaonekana hawaiwezi. Hata kama wanaiweza inasaidia ni kwa watazamaji wengi ambao ni watumiaji wakubwa wa Kiswahili?

Wale wa kwenye Redio ndiyo balaa. Sasa unakuta watu kama Maulidi Kitenge na Shaffii Dauda wameshindwa kutafsiri Kiingereza cha kawaida kabisa, wanatakaje kutumia kiingereza kigumu kuelezea mchezo wa mpira?
 
Hii ni moja ya sababu za mimi kuacha kusikiliza vipindi vya michezo
Mimi kama ni mechi kubwa let's say Simba na Yanga ama yale mashindano ya AFCON huwa nabonyeza audio pale nabadilisha lugha. Kwa maana yaani hata kutangaza mpira kwa ufasaha wa kiswahili hawawezi wanaruka ruka tu na masimulizi hadi ya ukoo anakotoka mchezaji mara ni nne kuzaliwa mara wanakusimilia kwanini anavaa jezi imeandikwa Jr ama jina la mama....bila kufahamu kuwa kutangaza kunaendana na kuchambua mchezo husika na sio mambo yasiyo husiana

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Code mix hizo na chanzo chake kikubwa ni kuto kuwa na lugha moja ya mawasiliano na kujifunzia hasa wakati wanasoma mashuleni kwahyo inapelekea mtu kuwa affected wakati wakutumia lugha kwahyo usiwalamu bari toa lawama kweny mfumo wako wa elimu na lugha ndio kweny Tatizo
 
Mtu anayechanganya Lugha bila ya sababu, hajui hizo lugha zote mbili bali alizikariri'

Kwa mfano neno "kupelekea" siyo neno sahihi bali "kusababisha" ndiyo neno sahihi. Kwa mfano ungeandika "...hasa wakati wanasoma mashuleni kwa hiyo inasababisha mtu kuathirika wakati wa kutumia lugha..."
 
Back
Top Bottom