Hakuna jambo la hatari mno kama kukuta watoto wa kiume wanapiga soga za umbea-umbea na watoto wa kike, hasahasa kuhusu maisha yao binafsi ya mahusiano. Ubaya zaidi wanamtuma mtoto wa kike kuja kuwasemea. Noma sana yani....
Halafu ninyi matajiri wa Jamii-Forums huwa mnashida sana. Hapa jukwaani huwa hamuachi majigambo. Mara kuishi Marekani, Ulaya, mko ofisi kubwa ,mna elimu nzito, na mifuko yenu imetuna mapesa.
Sasa mabinti wakianza kuwafuata huko PM kuwatandika vizinga au mkashindwa kumalizana vizuri huko nje, huwa mnarudi hapa jukwaani kuchafuana na kuanikana. Kwanini mambo yenu ya faragha msiyamalizie huko huko nje au PM. Yaani kila kitu chako binafsi lazima uje ukianike humu ???
NB: Kama huu uzi una ukweli, basi watoto wa kiume wamefika pabaya mno. It smacks a bad taste...