Wadau wa JF tujuane kwa kazi zetu, na dharau zitapungua

Wadau wa JF tujuane kwa kazi zetu, na dharau zitapungua

Wakuu

Humu kumekuwepo na dharau za hapa na pale humu jukwaani.unakuta mtu anakushambulia,anakutukana kwamba mnalingana umri, cheo, au mali.

Unakuta mtu anadharaulika mtaani kwake lakini jukwaani anajiona mtemi,anafoka na kuwadharau wengine

Leo nataka tukate mzizi wa fitna, tujuane kwa umri na vyeo vyetu,heshima itarejea na ustaarabu utarejea jukwaani

Mimi ni mmachinga wa kuuza maji,karanga,soda na vitu vidogovidogo vya wasafiri katika stand X na mkoa X (utani)

Karibuni
CIA-Tz special mission
 
kuna picha ulinitumia, mdada mmoja mrembo sana,yupo mbugani,ni eidha anang`oa mbegu za mpunga ama anapanda,na badae akawa amesimama nyuma ya magunia ya mpunga,kwa kweli nilizipenda hizo picha. Mkuu vipi hali ya mvua hapo misungwi.
Aaaah! Unamzungumzia Reyna. Naam! Yeye kaamua kujikita katika kilimo na ufugaji. Na anafanya vizuri sana. Ni mfano wa kuigwa maana angeweza kubinua matako mitandaoni humu akapata akitakacho lakini kaamua kuwa tofauti. Kazi hii ya kilimo na ufugaji imemheshimisha sana. Mungu ambariki binti yule 🙏🏿

Mvua Misungwi, kama zilivyo sehemu nyingine nyingi, ndiyo zinajaribu kuanza anza. Tunazisubiria kwa hamu!

-257344394.jpg
1757611123.jpg
-1160861866.jpg
-662668144.jpg

-1739838790.jpg
 
Mimi ni mfanyabiashara mkubwa nchini, chai nakunywa china chakula cha mchana nakula Dubai.
Shoo kitandani napiga bao kuanzia tano, Nina PhD

Jf raha sana 🤣🤣🤣
 
Aaaah! Unamzungumzia Reyna. Naam! Yeye kaamua kujikita katika kilimo na ufugaji. Na anafanya vizuri sana. Ni mfano wa kuigwa maana angeweza kubinua matako mitandaoni humu akapata akitakacho lakini kaamua kuwa tofauti. Mungu ambariki binti yule
reyna ni nani mkuu?
 
Mnatoa comment zenu kwa masiala sana utadhan mmelazimishwa jmn. Masiala n mengi kweny hii thread
Masiala ni nini mkuu?

Wewe comment yako isiyo ya masiala iko wapi?

Acha watu wajifurahishe maana mada yenyewe haina kichwa wala miguu. Ni masiala tupu! 😁
 
Mimi ni mzee wa tenda za kufyeka barabara za TANROADS na kuzibua Kalavati. Huwa nnawachora mnavyopita na magari yenu.

Lakin niwape maua yenu madereva wa malori na mabasi huwa mnatusalimia kwa honi.

Naomba siku mojamoja mkuwe mnatirushia mikate na maji kama mnavyowarushiaga wale nyani wa kitonga.
 
Back
Top Bottom