Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ni vilaka vipya kwenye nguo chakavu.Kwa kifupi;
1. Matokeo ya urais kuruhusiwa kupingwa mahakamani.
2. Mfumo kuruhusu Mgombea binafsi.
3. Kuwepo kigezo cha 50 + 1 kwa mshindi.
4. Kuwe na uwakilishi sawa wa 50/50 kwa jinsia zote.
5. Jeshi la polisi kutoingilia shughuli za vyama vya siasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
6. Tume ya uchaguzi iwe na watumishi wake.
7. Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi.
8. Mkurugenzi wa Uchaguzi, Mwenyekiti wa tume na Makamishina wapatikane kwa kuomba kazi ambazo zitatangazwa hadharani.
9. Uteuzi wa wajumbe wa tume uzingatie uwakilishi wa vyama vikubwa vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wanataaluma.
10. Kigezo cha kupita bila kupingwa kiondolewe.
11. Pamoja na kuzingatia jinsia jamii ya walemavu izingatiwe wakati wa uteuzi.
12. Mikutano ya vyama vya siasa ifanyike kwa usawa na nafasi ya Msajili wa vyama vya siasa itangazwe hadharani.
NB: Mimi naongeza 13. Atakayebainika kutangaza matokeo ya uongo ashitakiwe kwa makosa ya Uhujumu Uchumi, kwa sababu kalihujumu taifa zima lililotumia gharama kubwa kuandaa uchaguzi.
View attachment 2161685Hii sana imenitafakarisha siasa za Tanzania, Putin na tank ni Rais na CCM na Ukraine ni katiba mpya.
Simple. CCM hayawezi kukubali.
Haijawahi kuwa hivyo, kumbuka yaliyomtokea mzee Mwinyi huko Kigoma wakati wa uchaguzi baada ya kushuka kwenye ndege, rubani mmoja alipiga picha mapokezi hayo.Nakumbuka zamani vyama vyenye wagombea urais vilikuwa vinapewa ruzuku kwa ajili ya kampeni sikumbuki kiasi, pamoja na posho za mawakala wao.
1. Matokeo ya urais kuruhusiwa kupingwa mahakamani- Itahitaji mabadiliko ya Katiba
2. Mfumo kuruhusu Mgombea binafsi- Itahitaji mabadiliko ya Katiba ya sasa
3. Kuwepo kigezo cha 50 + 1 kwa mshindi- Itahitaji mabadiliko ya Katiba ya sasa
4. Kuwe na uwakilishi sawa wa 50/50 kwa jinsia zote- Sio muhimu, watu wachaguliwe kwa uwezo wao
5. Jeshi la polisi kutoingilia shughuli za vyama vya siasa kabla, wakati n
6. Tume ya uchaguzi iwe na watumishi wake - Kwa ngazi za chini kuhesabu kura wakitumika walimu ni sawa. Hii iwe upande wa wakurugenzi na wasimamizi wakuu.
7. Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi - Ilitakiwa kuwa hivi miaka mingi sana.
8. Mkurugenzi wa Uchaguzi, Mwenyekiti wa tume na Makamishina wapatikane kwa kuomba kazi ambazo zitatangazwa hadharani - Itahitaji mabadiliko katika Katiba ya sasa
9. Uteuzi wa wajumbe wa tume uzingatie uwakilishi wa vyama vikubwa vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wanataaluma - Taasisi za Kidini watakuwa na kazi gani kwenye tume? Au kufanya maombi?
10. Kigezo cha kupita bila kupingwa kiondolewa- Hakuna Kigezo Kikatiba
11. Pamoja na kuzingatia jinsia jamii ya walemavu izingatiwe wakati wa uteuzi - Watu wachaguliwe na kuteuliwa kwa uwezo wao
Ndio maana hiyo ruzuku ikafutwa, lkn lengo lilikuwa kuwawezesha ili wasirubuniwe na mabeberu wa nje.Hii haitakiwi kila mtu si ataamua kuwa na chama cha msimu wa uchaguzi Ili apate pesa?
Acha warubuniwe tuu si kuna sheria ya ku track matumizi yao na source ya pesa?Ndio maana hiyo ruzuku ikafutwa, lkn lengo lilikuwa kuwawezesha ili wasirubuniwe na mabeberu wa nje.
Ana uwezo gani mzuri!!!?50/50 ndio nini? Hivi kuna nchi yoyote duniani ina 50/50, mmeona wapi? Iko wazi, wanawake wengi uwezo wao bado mdogo sana kuongoza, sasa nchi inataka maendeleo, 50/50 sioni maana yake, sio nawachukia wanawake, la harsha, ukweli uko hivyo, naturally most women uongozi hawawezi, sasa maendeleo yatatoka wapi. Jamani, sielewi kama naeleweka, wanawake type ya Mama Samia ni 1 in 100 mil nasema kweli kabisa, na Mama Samia kajifunza mengi kwa JPM ndio maana amekuwa na uwezo mzuri.
Mm sioni hoja kabisa ya 50/50, na hakuna duniani mfano huo.
Hata matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani inahitaji mabadiliko ya katiba maana katiba ndo inazuia hilo jamboKati ya yote hapo ,hilo la mgombea binafsi halina tija ,litahitaji mabadiliko makubwa zaidi ya Katiba na sheria.
Basi hilo halitakubaliwaHata matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani inahitaji mabadiliko ya katiba maana katiba ndo inazuia hilo jambo
Matokeo ya urais kuruhusiwa kupingwa mahakamani.