Wadhamini wa Lissu waiomba Mahakama kutoa hati ya kumkamata Tundu Lissu

Wadhamini wa Lissu waiomba Mahakama kutoa hati ya kumkamata Tundu Lissu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani na maombi ya wadhamini Ibrahim Ahmed na Robart Katula wa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Julai 14, mwaka huu.
53c6d139d9a7137727f38e708e275cc6

Wadhamini hao amefungua maombi wakiiomba itoe hati ya kumkamata kwa kuwa wameshindwa kumpata na kumfikisha mahakamani hapo.

Maombi hayo yalipangwa kusikilizwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini upande wa Jamhuri haujawasilisha majibu ya kiapo kinzani.

Hakimu Simba alisema mahakama yake itasikiliza maombi hayo Julai 14, mwaka huu na kesi ya msingi itatajwa siku hiyo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba amri za awali kuhusu mshtakiwa Lissu zinaendelea.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni Wahariri Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Katika kesi ya msingi kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016, jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13, 2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
 
Matundu yameanza kubainika Sasa..😅
 
Angeachwa ili aje, ajipime ubavu na JPM tuone Nani Baba Lao,

Magufuli hajawahi kushindana kwa box la kura na akashinda. Fuatilia hata alipokuwa mbunge mara 4, ni mara ngapi aliwahi kushinda kwa box la kura? Niliposikia tu Lissu ametangaza kugombea, mara moja nilijua kesi yake itaanza haraka. Na kwa taarifa yako, hukumu yake tayari magu ameshapanga Lissu afungwe.
 
Kanunue kesi ufungwe wewe, nadhani madeni huwa yananunuliwa kwa mara ya kwanza wewe utanunua kesi.
 
Magufuli hajawahi kushindana kwa box la kura na akashinda. Fuatilia hata alipokuwa mbunge mara 4, ni mara ngapi aliwahi kushinda kwa box la kura? Niliposikia tu Lissu ametangaza kugombea, mara moja nilijua kesi yake itaanza haraka. Na kwa taarifa yako, hukumu yake tayari magu ameshapanga Lissu afungwe.
Akifungwa si atakuwa kashapoteza sifa ya kugombea urais jumla hata kwa miaka ya mbeleni?
 
Back
Top Bottom