Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Kabisa mkuu, hapa cha muhimu kama mtu unataka uchomoke haraka uwe na wale marafiki ambao wao tunaweza kuwaita 'wanafiki' au 'wajanja' lkn wa maendeleo. Kuna marafiki mnakula bata wote ila ikifikia saa fln yeye humuoni, au anakunywa kdg kachangamka lkn saa nne tu huyooo ashaondoka, wewe unabaki unafukuzia madem, dem kakukalisha anaagiza tu, saa saba anakwambia anaenda kulala kwake, unaanza kutafuta malaya mwingine, hapo kuja kushtuka kesho yake ushamwaga kama 300k, ndo unakutana na mchizi wako 'mnaaa'. Hao wachizi wanasaidia sana kukufanya ushtuke na ujione mjinga kisha unakua na hasira ya kutoka huko
Sure thing mkuu,

Mimi nilijifunza in hard ways, kwanza kuna kampani nilipiga chiiniii, then ikawa nakunywa sio kwa sababu wana wanakunywa ila nakunywa nikiona mimi nahitaji kufanya hivyo tena kwa budget na kiwango ninachoona mimi kinafaa.

Muda mwingi pia nakunywa kwangu, kutoka ni kwa machale sanaa 😂😂,

Lazima ukae kimalengo.
 
Uko sawa, tunapopishania ni hapo tu kunywea bia nyumban, mimi nilishashindwa kabisa.

Mie kipindi nataka kuchomoka miaka hio nilijiwekea plan kwamba mm ndo niwe wa kwanza kuondoka kila siku, sabab mie kunywa yangu ilikua ya kampan, then tunasaka madem, nliitolea toka kipindi nipo UDSM na machalii. Sasa nikistukia mshkaj anaanza kukusanya kusanya tu 'blackberry' yake (enzi hizo ndo zimeingia, malaya akikuta ipo mezani anakukonyeza aje so tulikuaga tunaziweka mezani), mimi naaga naenda toilet, nikiwa huko naaga kwa message tunakutana mitaani kesho yake. Hvohvo hadi nikachomoka, hii kunywa na wana ndo mbaya sababu unanywea sifa na kuwapa offa wadau inakukamua balaa
 
Mimi siyo tajiri bado lakini wakati naanza kuzoea kushika million 1 ikapanda tano mpaka sasa siri yangu sijawahi kuongeza kiwango cha matumizi eti kwa sababu hela nimeipata kwa jasho.

Wewe kijana unayetumbua kipato chako madai hela umeipata kwa jasho unapaswa ujue hakuna hela isiyopatikana kwa jasho hata huyo malaya mwenyewe anayejiuza ili hela yake aifurahie lazima jasho limtoke japo anasikia raha.

Mleta mada umewashauri vizuri vijana.
 
hii kunywa na wana ndo mbaya sababu unanywea sifa na kuwapa offa wadau inakukamua balaa
Hii ishaniponza sanaa 😂😂, ndio sababu ya kunifanya nijinywie zangu nyumbani.

Kuna ile feelings upo na wadau alafu waleti imevimba hutaki kuona wanao wanajisikia unyonge, basi kabla mezani hakujakauka ushamwita muhudumu adouble round,

Mara umeenda toilet, basi unapitia na jikoni ushaagizishia kilo mbili ya nyama choma wana wanashangaa meza inapendeza tu.
Kumbe pale unajiumiza mwenyewe tu 😂, asubuhi wana wanaishia kukupigia simu kukuuliza “vipi chief umeamka salama???” hapo ukikumbuka ya jana unazidi kuchafukwa na simu unaizimila mbali 😂😂
 
Ulichowaambia ni ukweli mtupu.

Nina vijana wangu nikiwaambia mimi nilikuwa naosha magari,lakini nilikuwa natunza hela kidogo kidogo kwa malengo na pombe ilikuwa mbali nami kwa kipindi hicho,labda tudemu kwa mbali kwa kipindi hicho. Nikafungua duka. Nikanunulia gari la kwanza miaka miwili baadae,hapo nina uwanja,najenga taratibuuu.

Kikubwa malengo. Hawa madogo wa siku hizi kila kitu wanaona wanachelewa. Wanafikiri zipo hela za kudondoka moja kwa moja nyingi,halafu afanye mambo yote kwa mkupuo.

Ndani ya mada,kipindi mimi nina mtaji wa milioni 40. Mjombaangu akawa anastafu anapata kiinua mgongo cha milioni 250. Nikampa plan hizo pesa afanyie nini,akaona kama nazimendea hela zake. Nikamwambia mimi sina shida hata na senti 5 yako ila nakusaidia ksbb nawajua nyie wastaafu,utarudi kunisumbua muda si mrefu.

Nikamwambia mimi nina milioni 40 tu,lakini ninazo nyingi kuliko zako milioni 250. Kwani miaka miwili mingi?. Nikawa na mtaji wa kama milioni 90+,anakuja kukumbuka yale maneno yangu na anaona aibu hata kunisalimia. Kachokaa hatari
 
Hii ishaniponza sanaa 😂😂, ndio sababu ya kunifanya nijinywie zangu nyumbani.

Kuna ile feelings upo na wadau alafu waleti imevimba hutaki kuona wanao wanajisikia unyonge, basi kabla mezani hakujakauka ushamwita muhudumu adouble round,

Mara umeenda toilet, basi unapitia na jikoni ushaagishia kilo mbili ya nyama choma wana wanashangaa meza inapendeza tu.
Kumbe pale unajiumiza mwenyewe tu 😂, asubuhi wana wanaishia kukupigia simu kukuuliza “vipi chief umeamka salama???” hapo ukikumbuka ya jana unazidi kuchafukwa na simu unaizimila mbali 😂😂
Hii inaambatana na kufukuzia kale ka heshima ka kuwa 'wewe ndo mkuu wa meza, jemedari mwenyewe AKA Suleimani wao'

Ikukute unapenda sifa af kuna rafiki yako mmoja anajua kutoa sifa zile za kichawa chawa, mzee utarudi home pocket ina vumbi tu na ile harufu ya ten ten
 
Umenikumbusha fundi wangu mmoja alikuwa akinijengea kibanda mahali fulani, ilikuwa nikimlipa maybe 350k basi atakuja kazini tena baada ya siku tatu hadi nne hela zikimwishia.

Kuna siku nimemlipa 700k baada ya siku mbili anasema anaumwa hana hata mia ya kwenda Hospitali, kumbe jana yake alikesha Kitambaa Cheupe na wale slay queens.

Yaani totozi na gambe ndiyo moto wa kuchomea hela za wengi
 
Kikubwa malengo. Hawa madogo wa siku hizi kila kitu wanaona wanachelewa. Wanafikiri zipo hela za kudondoka moja kwa moja nyingi,halafu afanye mambo yote kwa mkupuo.
Ndo tatizo kubwa, mtu anataka kitu cha milion, hataki kutunza 50k anayopata hadi ifikie huko, akipata 50k chap anafikiri kuitumia tu.

Ukitaka hasira fikiria kuna watu wana maduka na faida yao kwa baadi ya bidhaa ni shillingi mia, hizo mia mia zikiwa kumi ni buku, zikiwa mia ni 10k, anajiwekeza ndo anakuza mtaji.

Madogo hawajui hilo wanasubiri waje waipata yote 1m, huo ujinga unawachelewesha wengi saaana, wanabaki kusema wamerogwa kumbe wanajiroga wenyewe
 
Back
Top Bottom