Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Yap ni kwel hapa bora nimefungua JF maana nilikuwa na mpango wa kujilioua kufanya kufuru ya matumizi.

Umasikin mbaya sana, yaan unatufanya kile tulichokitafuta mwezi mzima tunakimaliza ndani ya siku3 which Is Nonsense.

Tujitahidi kuzingatia matumizi mazuri ya Pesa, watu wengi wana matumiz mabaya ya pesa hasa pale unapopita kipindi kigumu alafu ukazipata pesa, chap unakimbilia kuumwagilia moyo na kuupa pole mwili kwa starehe, unasahau kuwa shida haziishi na huwezi kuulizisha mwili hata ufanye nini.

La msingi tujitahidi kusave matumizi.
Na ikawe kumbukumbu kwa vijana wote watafutaji, natumaini kila mara mtu akifungua huu uzi kabla ya kufanya mlipuko wa starehe itasaidia kumkumbusha kidogo umuhimu wa hizo fedha kipindi akiwa na shida
 
Nidhamu ya pesa ni mtihani mzito shekh!

Imagine umehangaika zako mara umepiga “mshindo” wako alafu ukiangalia ndio weekend imeingia kila mahali ukipita unamsikia mariooo

“Shiiiiiiii badiiiii”
“nilikuwa na wanangu kina chinooo”
“niseme nsisemee, semaaaa” X 2

Ukizidi kusogea unamsikia jux nae ,
“huyuuu demu ake naniiii, anpandisha midadiii, anitafutia lawama,……….”

Ukisema uzame ndaniii tu kwisha habari yako, unakuta watoto wamepanda juu ya meza wanacheza na wamependeza balaaa!

Unaendaje kulala mkuu, au tukuulize,

we kuwezaaa???

Nyie achenii banaa starehe ni tamuuu [emoji23][emoji23]

Tukiamka asubuhi ndio majuto huanza.
[emoji23][emoji23]Ukipata pesa jambo la kwanza iweke mbali na wew, ikiwezekana itie ktk Benk Account then ATM card mkabidhi mtu alafu kaa nae mbali, jipe muda ishi kama hauna pesa, after several days Moyo utazoea hiyo hali ya kujihisi huitaji pesa and automatic utarudi ktk akili ya Kiungwana ya kutumia pesa kiungwana na kibajeti zaidi.

Ubaya wetu ni kupanga matumizi tukiwa na pesa mkonon badala ya kupanga matumizi ndipo pesa iyafuate hayo matumizi ili kuepuka lawama zisizo tarajiwa[emoji23].
 
Lengo lako la kushusha uzi ni hiyo paragraph ya mwisho.
Kwingine umeji brand tu kua unatoa dili za vijisenti.
 
Uzuri wa uber/bolt sio lazima ukariri plate number, kila mtu akinunua gari madereva wa uber/bolt watakula wapi??
 
Lengo lako la kushusha uzi ni hiyo paragraph ya mwisho.
Kwingine umeji brand tu kua unatoa dili za vijisenti.
Yaani na utu uzima wako ndicho ulichokiona?

Pitia comments za watu waloelewa lengo langu la kuweka huu uzi.

Hio inbox yenyewe nmeshagapiga lock toka muda sana hao madem watanifikiaje?, kilikua kibwagizo cha story tu hicho.

JIONGEZE
 
Ulicho andika ni kweli kabisa... Lakini hata ambao hatupigi Nyagi, bado pesa ni changamoto. Sijui tunazipeleka wap yani..?
 
Ulicho andika ni kweli kabisa... Lakini hata ambao hatupigi Nyagi, bado pesa ni changamoto. Sijui tunazipeleka wap yani..?
This is serious trouble then, kuna na kina 'CHUMA ULETE', nadhan washakuweka pin hapo
 
Sasa unafanya nini na hela zilizoongezeka
Hela haziongezeki mkuu zingekuwa zinaongezeka zikaonekana kweli zimetosha huyo Bahakresa tunayemsikia asingekuwa anashindana kununua Scania na HOWO series mpya ili aweze kuhimili soko.

Kila siku unakutana na chuma mpya hapo road yaani anaona kama zilizopo hazifikishi mzigo mapema ili akusanye hela.
 
Nasoma uzi WA kinabii, ukinikumbusha mambo niyafanyayo na ubaya wake

Wakuu,.mengi mnayoeleza kwa mliyokuwa mkipitia...yako kamili kabisa na ninayopitia....yaani ni mule mule

Kaka Mla Bata , ulitoka vipi kwenye hiki kifungo?
OP Teslarati ameeleza vizuri sana mkuu, kikubwa kujitathmini tu kipi unataka, furaha ya muda mfupi with a bunch of regrets au uwe na discipline kwa ajili ya kesho yako, we both know that isn’t easy at all 😂, ila unakubali kusacrifice tu kwaajili yako na future yako.

Na effects zake ndio kama ivyo, kama ulikuwa ni mtu wa kutoka sana na wana means sasa inabidi uanze kujipunguza kidogo kidogo.
 
Kaskazini wote tutakua na kikao Rombo Hotel mwezi huu wa 7 tarehe 7,Agenda za makubaliano.

1.Agenda za Maandalizi ya Christmas
2.Usajili wa wanachama wapya
3.Namna ya kupata pesa
4.Ujasiriamali endelevu.
NB Makubaliano ni kwamba disemba kila mtu atachinja alicholisha disemba.Kwa wale mnaolisha Layama chips mjini disemba mtachinja mlicholisha hakutakua na huruma
 
"wewe wiki 2 zilizopita si umepata hela ambayo mwalimu anatumia mwezi mzima kuipata" ,

Daah serikal iongezee mishahara ya walimu mana sio kwa dharau na matusi wanayopata. Yan mtoa mada unaamin kla mwlm anasubr lak tano ya salary kuna walm wanafanya makubwa na wana investiment zao,
 
Bora kijana abet kuliko mzee na wanapoteana vibaya, mzee hajamaliza majukumu analiwa unamuonea huruma sana
Hao watakuwa Wazee wa hovyo, Wazee wenye busara zao huwakuti wakifanya mambo ya hovyo hata siku moja
 
Hao watakuwa Wazee wa hovyo, Wazee wenye busara zao huwakuti wakifanya mambo ya hovyo hata siku moja
Ile kitu ni uraibu mkuu, mazoea yakizidi ngumu kuacha, ingawa unajua madhara yake ila ngumu kuacha.
 
Ile kitu ni uraibu mkuu, mazoea yakizidi ngumu kuacha, ingawa unajua madhara yake ila ngumu kuacha.
Mungu anisaidie nisiwe na huo uraibu.

Sijawahi Kubet

Sinywi pombe

Sivuti sigara/bange

Sijui nainjoi nini maisha haya 😅🙌
 
Out of topic, Mtoto mkali mmoja wa JF aliepo karibu na mikocheni anaependa bata anicheki, nipo mitaa hii weekend nzima
Maneno meengi ...kumbe point ndo hii ..

So you are financially free!!?
Wewee..!!😒
 
Back
Top Bottom