Wafanyabiashara walioporwa mabilioni na Mwendazake kurejeshewa fedha hizo na Rais Samia

Yes ni wakwepa Kodi lakini hupaswi kuchukua Hela kwenye akaunti ya mtu inapaswa umpe ratiba ya kulipa au mpige fine Ili afanye biashara huku anakulipa hata kama itachukua miaka 5. Ila hii ya kuzoa Kila kitu hapana maana biashara inakufa kabisa.

Ni kama yule mzungu alivyodaka ndege zetu ulidhani ni ustaarabu? Sasa ndege isiporuka Mapato ya kulipa yatatoka wapi? Au imagine China waje kuchomoa pesa zetu zote BOT kisa wanatudai mikopo kadhaa unadhani itakuaje?

Hakuna mtu asiyekwepa Kodi au kudaiwa mkopo Cha msingi mbane akulipe ila sio kukomba pesa kwa akaunti bila utaratibu.
 
Ingekuwa bora zaidi kuelezwa kwanza zilikoenda hizo pesa
 
Ingekuwa bora zaidi kuelezwa kwanza zilikoenda hizo pesa
Hizo fedha zilijenga uwanja wa ndege Chato, Kivuko cha wasafiri Chato, ndege za serikali Chato, mbuga ya wanyama Chato, hospitali ya rufaa Chato, VETA chato na barabara za Chato.
 
Hizo hela anazorudisha anazitoa wapi?.

Na hizo hela zilizoporwa zilikwenda wapi?.
Hata wale wa uhujumu uchumi usishangae wakarudishiwa. Maana walilipishwa mabilion Tena cash kwa kukiri kosa ila cha kushangaza hakukua na Sheria iliyokua inaelekeza Ile pesa iende wapi!!! So ikajenga mwanya kwa wahuni kugawana.

Nia ya JPM ilikua nzuri sikatai ila Kuna wahuni walinufaika na huu mpango. Yaani badala ya Hela kurudi serikalini wakajikuta inatoka kwa mkwepa Kodi inaenda kwenye tumbo la fisadi mwingine serikalini waliojificha kwenye kichaka cha uzalendo!!
 
Hawo wahuni ni Mwendazke na genge lake. Unadhani yale mabulungutu aliyokuwa anagawa ovyo kwenye ziara zake yalikuwa yanatoka wapi?
 
niongeze na mimi tuwe wawili kwenye kuamini mwishoni kuwa walionewa.
Obviously hayajakukuta ndio maana!! Hivi si juzi hapa serikali imekiri trillion 400 waliodai Acacia ilikua feki Ili kuwaita mezani!! So usiwe mwepesi wa kuamini kuwa serikali Iko sahihi muda wote.

Ukitaka kuona ni uhuni mliposikia China inapora bandari ya Sri Lanka Ili kufidia deni mlijiskiaje?? Au mliposikia Mzungu kakamata ndege yetu kula South Africa Ili arudishiwe deni Kuna mtu alipongeza??

So kama mlivyoona mzungu kawaonea basi hata hao wakwepa Kodi walionewa. Kama mtu ana kesi ya Kodi kwanini asiburuzwe kortini au kwenye TRAB na TRAT why uibe Hela zake kimya kimya kinyume na Sheria?

Nia ilikua njema ila utekelezaji mbovu sana ndio umetufikisha huku
 
Zilienda wapi hizo hela? Isije ikawa walikula wengine halafu Kodi za wa wananchi wavuja jasho ndio ziwalipe
Fedha hizi zilizoporwa kwa matajiri kupitia ofisi ya mganga, zilikuwa zikilipwa cash, hawakutaka kabisa zipitia mfumo wa kibenki ili zijulikane zilitoka wapi na kuishia wapi.

Kuna tetesi kwamba pesa hizi ziliporwa na marehemu na kuzifanya kuwa pesa zake binafsi. Pesa hizi ziliwekwa kwenye chumba maalum chenye uimara mkubwa wa kuta na milango kule kijijini kwake, na kulindwa wakati wote. Kuna tetesi pia kuwa mara baada ya kifo chake, watu wake wa karibu walienda, wakazichukua na kuzitorosha.

Habari hizi zinatiwa nguvu zaidi na taarifa ya mkaguzi kuwa pesa hiyo iliyoporwa na marehemu kutoka kwa aliowabambikizia kesi haionekane mahali popote.

Pesa hii itafutwe, ili waliodhulumiwa warudishiwe pesa yao. Litakuwa kosa kubwa walioiba waendelee kuitumbua hii pesa, halafu pesa za walipa kodi zukafudie pesa iliyoporwa na marehemu wakati wa uhaiwake.
 

Nakazia.
 

Ana miezi 20 hayupo, mbona hakuna mtu ameenda kushtaki?
Kwanini tunakubali kuchezeshwa huu mziki?
 
Nashauri twende mbali kidog. Katika fedha zilizoporwa kuna asililia kubwa iliingia kwenye vikosi kazi kama 3 vya kupora mali za waliokuwa targeted . Kulikuwa kile cha TRA na kulikuwa kile kilichokuwa chini ya DPP Biswalo na cha tatu ndiyo hicho cha Makonda na Sabaya. Isiishie kuwarudishia fedha walioporwa bali wale waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ili tuweze ku-recover baadhi ya fedha walizojigawia.
 

Na mimi hapo ndo nitaendelea kumkubali JPM mpaka kesho, the courage to do what’s necessary, mfano mtu kama Chen.ge kila mtu anajua ameiba ila huwezi kumpeleka kokote ukamfunga kwa namna alivokua anasuka dili zake, why mtu kama huyu upoteze nae muda kwenye kesi wakati ukimtaiti kwenye mifumo mbadala anaweza kutema kila alichoiba?
 
Mh, ni jambo jema lakini hayo asiyafanye kama yeye hakuwemo kwenye ile serikali na yeye alikuwemo na alishiriki
Sa100 alishiriki dhuluma hiyo kwa vp? Au inaposemwa jiwe alikuwa dikteta huelewi maana yake? Kama ni collective responsibility, sawa, maana wote- jiwe na S100 ni ukoo mmoja uliolaaniwa wa ccm.
 

Please do not take offense, wewe kichwani zinakutosha?
 
au kama zilitumika kununua wapinzani kwa manufaa ya CCM, basi CCM wenyewe wajue namna ya kuzirudisha kwa wenyewe.
Slow slow aje hapa kwa upoleupupole atujuze kwenye yale manununzi aliyosimamia pesa iltoka wapi!
 
Bado mnaendelea kuaminisha watu kua mlikua sawa na mlionewa, nyie mlikwepa Kodi majizi makubwa nyie, na kusababisha wanyonge kuendelea kukosa dawa, madawati, zahanati, maji na mengineyo, mlipotemeshwa fedha bado mmeendelea kutetea wizi wenu ili muonekane mlikua sawa, mtahukimiwa mbaya kabisa washenzi nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…