Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Sasa mbona wale wanajeshi wanaopigaga watu sijawahi kuskia wakisimamishwa,

Wanajeshi ndo huwa wanazingua zaidi.
Mara nyingi wakati wanapiga Wananchi huwa hawana Insignia za kuwatambulisha
 
Video ni ushahidi tosha. Uchunguzi bado mnataka kuingia tena gharama za nini?
Hapa ndipo huwa wana niacha hoi. Yaani ukweli una onekana wazi lakini ati uchunguzi.
Ndio vile vikao vya mkakati kule kwa Mwigulu.
 
Lakn matapeli wanaumiza sana watu. Watu wamekufa kwa pressure watu wamejiua, wastaafu wanatapeliwa pension zao.

Mbaya zaidi hizi kesi za kutapeli zinapoteza muda tu mara nyingi wanaachiwa..
binafsi naungana na wale askari kwa kitendo walichokifanya!!!

PONGEZI kwa askari
 
Ila wamemidia jamaa kuongea lugha ya kwao. Lugha nzuri ya kihaya
 
Hapa ndipo huwa wana niacha hoi. Yaani ukweli una onekana wazi lakini ati uchunguzi.
Ndio vile vikao vya mkakati kule kwa Mwigulu.
Kuna uchunguzi? Taratibu zinafuatwa.
 
Tapeli kaogeshwa maji na kugaragara chini ndo salama yake ingekuwa kakamatwa mtaani wangempiga vibaya hata kumuuwa.
Na huyo tapeli aache utapeli.
Kishoka yule......
Ila hao jamaa warudishwe kazini tu
Vishoka pale wamekuwa wasumbufu sana

Ova
 
Huyo kishoka alikosea kutowapa ulaji...vishoka wote wa uhamiaji wanakula na maafisa wa uhamiaji...uhamiaji kurasini vishoka kibao....ukiwapa mpunga foleni yeyote hukai ..utaitwa kupiga picha then unakabidhiwa passport..chain ipo kuanzia reception

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
ndiyo shida kubwa hiyo nchi zetu za kiafrika, maaskari wao hufikiri wapo juu ya sheria, mamlaka huubiria wananchi kutojichukulia sheria mikononi ila wao wenyew ndio wanaongoza kufanya hivyo, yaan taasisi yeyote ile serikali ambayo watumishi wake wamepitia maaskari wa aina yeyote ile hupenda sana kujchukulia sheria mikononi pale mtu anapowakosea, haya ni mambo ya zama za mawe kabisa, utatumikiaje chombo cha dola halafu hujui umuhimu wa kuheshimu sheria?
 
Ukiitazama Ile video baada ya kumtesa walimsafisha tayari Kwa kumrudisha Kwa mkuu kwamba adhabu waliyotumwa kutoa wamekwisha itekeleza.
 
Back
Top Bottom