Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Jamaa na likitambi lake alipata Cha mtemea kuni.. haiwezekani serikali uitanie
 
Wale ni wanajeshi sioni kosa lao,hizo ni adhabu ndg ndg za kijeshi kwanza amepewa mazoez ya kawaida tu,na hakuna aliyempiga zaid ya kupewa Yale mazoez.kwa hiyo siku hiz watuhumiwa wabembelezwe bembelezwe hata pushap wasipewe?!,siku zote ukipatikana na kosa na mjeda ,Yale mazoez niya kawaida sana.au nae alikuwa muwekezaji!?
 
Ni kweli mkuu lakini alianza kumuadhibu kwa kutumia ukabila ,kitendo cha kumuamrisha zaidi ya mara 3 anasema atamke kwa lugha ya kihaya lengo ni lipi? Kwani watanzania wote wanajua lugha ya kihaya ? Wanatakiwa kuajibishwa.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
...Kwa hiyo Mkuu unawaunga Mkono, ama ni yale mambo ya Msiba uusemee unapokuwa kwa jirani tu lakini maumivu yake utayasikia unapokuwa umetokea nyumbani kwako??? ...hebu fikiria tu kama jamaa angekuwa ni mdogo wako anayekufuata?? [emoji848]
 
Makakal angetaja hao jamaa majina ili huku mitaani tuwajue. Kwa nini kataja jina la mtuhumiwa bila kuwataja watesi wake?.
 
Walimtendea fair sana,hata hawakumtandika ila walimpa tu mazoezi ya kupunguza kitambi kile kikubwa.
Alipata adhabu iliyomstahili huyo kishoka
Hatuwezi jua alishawafanyia hivyo watu wangapi,inaelekea uhamiaji pale siku nyingi
Walikuwa wanamlia timing!

Ova
 
Habari wakuu,

Nimeona Ndugu Alex Rafael aliepigwa na Askali wa Idara ya Uhamiaji akiepelekea kusimamishwa kwa askali hao walio shiriki tukio hilo la kumpiga.

Mimi nimetafakali sana je, aliepigwa huenda huyu siyo tapeli wa kujiita ni Afisa Takukuru wala Uhamiaji, huyu ni Mtumishi wa serikali tena mzito katika idara hizo hizo nyeti maana ametia presha kubwa mpaka viongozi wamesimama kulaani tukio lile.

Kwani unahisi matapel wangapi wanakamatwa na kupingwa ila hawafukuzishi watu wala kusimamishwa watu?

Huyo tapeli ni mtu wa aina gani? Je, kuna siri gani katika tapeli?

We una maoni gani?
 
Iko hivi, kwenye hizi kazi za kuteuliwa au kazi za serikalini, kila mtu anaangalia jinsi ya kutumia fursa vizuri, sasa sometimes hio fursa inaweza ku-backfire kama ilivyotokea kwa wale askari halafu ikawa fursa kwa yule Boss wa Uhamiaji kujiuza kwenye media kuwa anatenda haki na ni msikilizaji mzuri....hicho tu.

The Gambler "Secret to survive is knowing what to throw away and what to keep, because every hand is a winner and every hand is a looser, the best you can hope for is to die in your sleep"
 
Kwa sheria zetu za kidini na kimila Hilo jamaa ni tapeli na hukumu yake ni kipigo na ikibidi ni kumpumzisha kwa amani.

Ila kwa sheria za wenzetu wa magharibi ambazo tunazifuata bila kujali kama tumefika ustaarabu kama wa kwao huyo jamaa inabidi abemberezwe hadi mahakamani, apewe wakili wa kumtetea na huku uchunguzi ukifanyika kama alikuwa anaumwa au hapana hata kama amekuwa akifanya vitendo hivyo tangu amebalehe
 
Kosa walilolifanya wale askari wa uhamiaji ni kurekodi lile tukio.

Wangemalizana nae "kihuni" tu bila kurekodi chochote. Nina uhakika yeye mwenyewe angeambiwa achague wamalizane kihuni au apelekwe mahakamani/TAKUKURU angechagua kumalizana kihuni.

Sasa hapo bado wanatambaa nae tena mambo ya mahakamani, jamaa analo pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…