Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Walimtendea fair sana,hata hawakumtandika ila walimpa tu mazoezi ya kupunguza kitambi kile kikubwa.
 
mwizi wa kura za upinzani anapotoa ushauri wa kimalaika
Huyo Tapeli hajafanya Jambo jema Ila nao maofisa wetu wa vyombo vya dola wajifunze kutumia reasonable force ku handle mtuhumiwa....
 
Askari mnateteana kwa mambo ya kikatili...sasa mahakama zipo za kazi gani?...
Ndugu
Jaribu kufikiri kikakamavu kule ni kuidhalilisha idara...mzembe kanenepa na kitambi anamiliki kaichukulia uhamiaji oya oya...kamkokota raia mwema huko hadi dept.

Anakwepa kuvuja jasho...kuwa ustadi wa hali ya juu maafisa wamemgundua na wamemnyakua na ka-drill kidogo cha kumshusha presha basi platform zote bongo kama femist vile.

Tapeli or mwizi si watu wa kupeleka polisi ni kumchimbuachimbua na kumpa second chance akikosa ni death penalty ila ni vile sheria za kishetani ndo zinaongoza dunia!!!

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii....
Hivi ndivyo inavyotakiwa @chizimaarifa
 
Ila hao jamaa wa uhamiaji nao mafala tu.. Mtu kama huyo mnaenda kumficha porini huko mnamfanya mtakacho mpaka ayachukie maisha.. Sasa wao wanakimbilia kurecord video

Wameniudhi
Yaani wangefanya kama wale wa magogoni
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii...
Comissioner Dr. Anna, asante sana. Uhamiaji wangetenda haki mianya ya vishoka kama Ndugu yetu Alex wasingekuwepo.
Aidha mtuhumiwa anastahili kupelekwa mahakamani kwenye vyombo vya sheria na siyo kumburuzwa kwenye maji taka, kumdhihaki na nk.

Hao maofisa wafukuzwe kazi na mtuhumiwa apelekwe mahakimani. Haki huleta upendo na haki huondoa chuki, haki huondoa visasi.
 
Bwana KYAI ni tapeli sawa amepatikana na hatia ndani ya ofisi za wenye mamlaka ilifaa zaidi kumwajibisha kisheria kwa makosa yake ya utapeli/udanganyifu
Kumdhalilisha namna ile kumwogesha tope mithili ya kiboko siyo ubinadamu

Utapeli anaofanyia watu ni ubinadamu?

Mzazi mkanye mwanao jasho la mtu halitoki bure
 
Hao maafisa wangeweza kumuua huyo Alex si uliona alivyokuwa anatweta? Two wrongs dont make it a right ,sheria zichukue mikondo yake.

Kama Alex amekosa ilitakiwa wamshataki kwa mujibu wa sheria na si kuchukua sheria mkononi na kutoa adhabu.
 
Comissioner Dr. Anna, asante sana. Uhamiaji wangetenda haki mianya ya vishoka kama Ndugu yetu Alex wasingekuwepo.
Aidha mtuhumiwa anastahili kupelekwa mahakamani kwenye vyombo vya sheria na siyo kumburuzwa kwenye maji taka, kumdhihaki na nk.
Hao maofisa wafukuzwe kazi na mtuhumiwa apelekwe mahakimani. Haki huleta upendo na haki huondoa chuki, haki huondoa visasi.
Kuwafukuza kazi sio sheria mkononi?
 
God bless you Dr. Makakala..umefanya jambo jema. Kiukweli hao maofisa walifanya kitendo cha kinyama. Hujatuangusha. That's what I expected and you have delivered.
 
Wataje majina ili na wao watu wao wa karibu wajue
Umenena vema. Nilisikitika kuona afisa wa Uhamiaji anamkejeli mtuhumiwa kwa kusema hivi jibu kwa lugha yako ya Kihaya. Huyu afisa alikuwa na lengo gani. Alirudia zaidi ýa mara moja.

Watumishi waliosimamishwa watajwe majina na watu wao wa karibu wajue. Mkuki kwa nguruwe.....
 
Walimtendea fair sana,hata hawakumtandika ila walimpa tu mazoezi ya kupunguza kitambi kile kikubwa.
Mkuu hapana, 'HATA UKIFA WEWE UNA FAIDA GANI'Haya maneno wamesikifa wakitamka hao watu. Je. Kuna uhusiano gani na hayo unayoita mazoezi? Yamkini wewe na Mimi hatuna faida yoyote katika Taifa hili. Je kwa familia zetu na watoto wetu hatuna faida? Huyu baba ana mke na watoto Kama wewe ulivyo na mke/mme
 
Utapeli anaofanyia watu ni ubinadamu?

Mzazi mkanye mwanao jasho la mtu halitoki bure
Mtuhumiwa hufikishwa panapostahili kujibu tuhuma zake na kuhukumiwa anapopatwa na hatia
Kilichofanywa na maafisa siyo sahihi
 
kwa maoni yangu sioni kosa lolote walilio fanya hawa maafisa wa uhamiaji, walicho kifanya ni adhabu za kawaida kabisa za kijeshi, hakupigwa bali alipewa adhabu ya kawaida kabisa ambazo hutolewa na vyombo vyetu vingine.

Nisingeona hawa maafisa wana fukuzwa au hata kushushwa vyeo vyao, wachwe wachape kazi zao.

Hata ingekuwa mimi ndio afisa uhamiaji ningempa adhabu kama hiyo.
 
kwa maoni yangu sioni kosa lolote walilio fanya hawa maafisa wa uhamiaji, walicho kifanya ni adhabu za kawaida kabisa za kijeshi, hakupigwa bali alipewa adhabu ya kawaida kabisa ambazo hutolewa na vyombo vyetu vingine...
Maoni yako yatabaki kuwa maoni yako na ni uhuru wako.

Hatahivyo nchi hii haiongozwi kwa maoni ya mtu bali kwa sheria zinazoishi kutoka kwenye katiba ya nchi.

Raia akivunja sheria anatakiwa kufikishwa mahakamani na mahakama ndio yenye jukumu la kuamua na sio askari aliyemkamata.

Na hayo sio maoni yangu bali ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom