pye Chang shen
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 11,422
- 6,108
Hapo uhamiaji watu wanalizwa sana na hao jamaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo Tapeli hajafanya Jambo jema Ila nao maofisa wetu wa vyombo vya dola wajifunze kutumia reasonable force ku handle mtuhumiwa....
NduguAskari mnateteana kwa mambo ya kikatili...sasa mahakama zipo za kazi gani?...
Hivi ndivyo inavyotakiwa @chizimaarifaWIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii....
Ila hao jamaa wa uhamiaji nao mafala tu.. Mtu kama huyo mnaenda kumficha porini huko mnamfanya mtakacho mpaka ayachukie maisha.. Sasa wao wanakimbilia kurecord video
Comissioner Dr. Anna, asante sana. Uhamiaji wangetenda haki mianya ya vishoka kama Ndugu yetu Alex wasingekuwepo.WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii...
Bwana KYAI ni tapeli sawa amepatikana na hatia ndani ya ofisi za wenye mamlaka ilifaa zaidi kumwajibisha kisheria kwa makosa yake ya utapeli/udanganyifu
Kumdhalilisha namna ile kumwogesha tope mithili ya kiboko siyo ubinadamu
Kuwafukuza kazi sio sheria mkononi?Comissioner Dr. Anna, asante sana. Uhamiaji wangetenda haki mianya ya vishoka kama Ndugu yetu Alex wasingekuwepo.
Aidha mtuhumiwa anastahili kupelekwa mahakamani kwenye vyombo vya sheria na siyo kumburuzwa kwenye maji taka, kumdhihaki na nk.
Hao maofisa wafukuzwe kazi na mtuhumiwa apelekwe mahakimani. Haki huleta upendo na haki huondoa chuki, haki huondoa visasi.
Umenena vema. Nilisikitika kuona afisa wa Uhamiaji anamkejeli mtuhumiwa kwa kusema hivi jibu kwa lugha yako ya Kihaya. Huyu afisa alikuwa na lengo gani. Alirudia zaidi ýa mara moja.Wataje majina ili na wao watu wao wa karibu wajue
Mkuu hapana, 'HATA UKIFA WEWE UNA FAIDA GANI'Haya maneno wamesikifa wakitamka hao watu. Je. Kuna uhusiano gani na hayo unayoita mazoezi? Yamkini wewe na Mimi hatuna faida yoyote katika Taifa hili. Je kwa familia zetu na watoto wetu hatuna faida? Huyu baba ana mke na watoto Kama wewe ulivyo na mke/mmeWalimtendea fair sana,hata hawakumtandika ila walimpa tu mazoezi ya kupunguza kitambi kile kikubwa.
Mtuhumiwa hufikishwa panapostahili kujibu tuhuma zake na kuhukumiwa anapopatwa na hatiaUtapeli anaofanyia watu ni ubinadamu?
Mzazi mkanye mwanao jasho la mtu halitoki bure
Wewe ndio uko nje ya mstari kweli! Nani kafukuzwa kazi?Kuwafukuza kazi sio sheria mkononi?
Maoni yako yatabaki kuwa maoni yako na ni uhuru wako.kwa maoni yangu sioni kosa lolote walilio fanya hawa maafisa wa uhamiaji, walicho kifanya ni adhabu za kawaida kabisa za kijeshi, hakupigwa bali alipewa adhabu ya kawaida kabisa ambazo hutolewa na vyombo vyetu vingine...
Upo sahihiJinai haiwezi kuhalalisha mtu mwingine kufanya jinai