Waligusa Nini Yarabi Toba...
 
Tangu ripoti ya CAG iwekwe hadharani, maafisa wawili wa CAG wamefariki huku vifo vyao vikizunguka sana mitandaoni kana kwamba kuna jambo sio la kawaida/

Mbaya zaidi wanatajwa baadhi ya watu, kwanini tamko rasmi lisitolewe kuhusu sintofahamu hii...Je hadi kufikia Novemba ripoti ya CAG itakaporuhusiwa na Tulia kujadiliwa bungeni ushahidi mwingi kiasi gani utakaokuwa umepotea..

Tutakuja kuambiwa vielelezo fulani alikuwa navyo aliyefariki.
 
Wewe unasubiri mpaka wakanushe ndiyo ujue ni uongo?
 
Hata kama wanasema kifo ni fumbo, lakini kimsingi panapotokea vifo viwili vinavyofuatana, vya watumishi wawili tofauti, toka ofisi moja, waliohusika kuibua uozo kwenye ofisi za serikali uliooneshwa kwenye ripoti ya CAG, wanaojielewa lazima wajiulize maswali.

Panahitajika majibu ya kina kuhusu vifo hivi, ili kama kuna mchezo ulichezwa, basi watumishi wengine kwenye ofisi husika wawe makini, na uchunguzi wa kina ufanyike.
 
Kuna ombwe kubwa la vyombo vya habari Tanzania. Haya ni mambo ya media kuafanya uchunguzi na siyo kusubiri matamko ya serikali kama anavyodai mchangiaji mmoja.
 
Acha wacheleweshe tatizo kwa muda kwa kuua wasio na hatia,iko siku watalipia udhalimu wao
 
Kuuliza ndio uchonganishi?
Ukizama kwenye bandiko lake hakuna kiulizo. Ni mwemdo wa serious and kind of heinous allegations !!! Tuhuma kama hizi zinatakiwa kuwa na vielelezo vinavyojitosheleza. Mleta mada katunyima vielelezo hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…