MAOVU YA MAGUFULI NI SEHEMU YA HISTORIA YETU
ANDREW Jackson ni Rais wa Saba wa Marekani. Aliongoza mwaka 1829-1837. Historia ilimkweza. Mwaka 1928, sura yake ikawekwa kwenye noti ya dola 20.
Miaka 88 baadaye, Serikali iliamua kuondoa picha ya Jackson kwenye noti ya dola 20. Sababu, Jackson alikuwa mfanyabiashara ya utumwa, alionea watu weusi na kukandamiza wahindi wekundu.
Kisha, picha ya mwanamama mwanaharakati, Harriet Tubman, ikapendekezwa ichukue nafasi ya Jackson.
Ingekuwa Tanzania, wagonjwa wa Stockholm Syndrome (wenye mahaba na watesaji), wangesema wanashindana na marehemu.
Pokea habari, historia hufundishwa kwa ajili ya mwendelezo wa mema na mafundisho ya kukwepa maovu yasijirudie.
Ukiona kiongozi anatolewa mifano mingi hasi, ujue alifanya maovu yaliyovuka kiwango cha ubinadamu.
Kuna tofauti kati ya makosa (errors au mistakes) na maovu (evils). Kukosea ni ubinadamu, kutenda maovu ni ushetani.
Wafanyabiashara kudhulumiwa fedha benki. Wamiliki bureau de change kunyang'anywa na kufilisiwa kikatili. Watu kuuawa kisha miili yao kuokotwa kwenye viroba fukwe za Bahari ya Hindi, hayo hayakuwa makosa ya kibinadamu. Ni maovu.
Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi, akanyimwa mpaka matibabu, ubunge akafukuzwa, akadhulumiwa stahiki zake za ubunge akiwa kwenye kitanda cha matibabu. Haya hayakuwa makosa. Ulikuwa unyama. Ni uovu.
Kuchota fedha za umma Hazina. Sh1.5 trilioni. Sh2.4 trilioni. CAG Mussa Assad akabaini ufisadi wa Rais. Akasema Bunge ni dhaifu, halifanyi kazi ipasavyo. Rais akavunja Katiba na kumfukuza kazi. Wizi mkubwa kama huu na uvunjifu wa Katiba, sio makosa. Yalikuwa maovu.
Watu kupotea na serikali kujikausha kufanya upelelezi, sio makosa ya kibinadamu, ni ushetani. Ni uovu.
Kama ambavyo nchi nyingine hupitia historia za viongozi wao na kurekebisha, nasi hatutakaa kimya. Maovu ya Magufuli ni sehemu ya historia ya nchi yetu. Tutayasema sana. Dunia haipaswi kupotoshwa.
Miaka miwili imepita tangu alipofariki dunia. Wasiwasi umeondoka. Maovu mengi yameondoka. Ikiwemo ujambazi wa kubambikia watu kesi za uhujumu uchumi na kulazimisha watoe fedha. Pesa zikaingizwa akaunti binafsi na kufichwa China.
Ndimi Luqman MALOTO
My taķe;
Haya nadhani ndio majibu yenu sahihi watu wa yule mwovu!