Waha tupeni majibu ya hii kauli ya Lissu; 'Kuna kijiji kinaitwa Kazura Mimba kipo Kigoma, kina watoto wengi kweli kweli'

Nakumbuka ilikuwepo camp ya wakimbizi mitaa hiyo, wale warundi wanazaliana sana kwakuwa UN inawalisha regardless of how many they are
 
Na kichocheo kikubwa cha Tanzania watu kuzaana sana nahisi ni upatikanaji wa chakula. Hii nchi watu wanakula vizuri sana tena sana.

Kuna sehemu inaitwa Matombo Morogoro aisee yaani ukienda kule mavitu ya kula ni nje nje, watu hawana fedha mfukoni ila mavyakula ni ya kumwaga.

Ndo maana pia inakuwa ngumu sana kwa raia wa nchi hii kupigania mabadiliko ya kisiasa, wanaona kwamba hayana mashiko kwenye maisha yao kwasababu wanakula wanashiba kila siku na chakula kipo tu.

Nchi kama Kenya ambayo ni semi desert pamoja na kuwa na GDP kubwa hakuna chakula, wana struggle sana huo upande, hawana misosi kama sisi ndo maana pia population growth yao sio kivile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…