Waishio milimani Jijini Mwanza watakiwa kuondoka kupisha mwekezaji

Waishio milimani Jijini Mwanza watakiwa kuondoka kupisha mwekezaji

habari njema kwa watu wa Mwanza, mwanza inakwenda kubadilika
 
Nimezaliwa Njombe naishi Mbeya na nini shughuli za uzalishaji mali kwenye mikoa 3 tofauti..

Una swali jingine? Unadhani kila anaemsapoti Rais ni mkabila kama yule zwazwa wenu?
Lakini mkuu, sio vyema kuita nyumba za wenzio uchafu, hata hio nyumba yako nzuri kwa wengine ni choo tena cha kujisaidia wageni, tembea uone.
 
Mbona hii kitu ilikuwepo toka awamu ya nne jameni? Kigoto kuliwekwa beacon, Kiseke mlima wa Hali ya hewa, Igogo na Isamilo.Mwenda zake alijua huu mchongo na ndio uliompa kura Kanda ya Ziwa 2015 kwa kuchukua tatizo Hilo kuwa fursa kwake nakumbuka tukiwa CCM Kirumba ktk kampeni Wananchi wa maeneo husika walizirai na kulia akasema hakuna mtu kuguswa, so it's just a matter of time waje na Buzuruga
Wanafufua miradi yote ya awamu ya nne.

Awamu ya sita ni replica ya awamu ya nne.
 
#HABARI WAKAZI wa Jiji la Mwanza waliojenga maeneo ya milimani wanatarajiwa kuondolewa ili kupisha wawekezaji kutoka nchini Brazil./https://t.co/QD6YHUbiF5 https://t.co/8CILpXP7qFView attachment 2260361
Muondoke huko Milimani ila mlipwe au mjengewe apartments. Nyumba bila barabara? Hivi waafrika tutaelimika lini? Tunaongeza slums kwenye miji yetu...Hakuna mpangilio, muondoke haraka sana.
 
Hii mambo ya kuuza nchi vipande vipande tunapata hasara, kama vipi tuuze jumla kila mtu apewe chake asepe.

Lakini hiyo familia ya Brazil itajenga kwenye milima yote ya Mwanza Mabatini, Kirumba, Igogo, Mahina mpaka Ibanda huko?
nadhani umeishia kusoma kichwa cha habari tu kwa uvivu wako
 
Ulivyo Soma ni sahihi kabisa wala hujakosea. Ndo habari ya mjini, zile nyumba zote zilizopo kwenye mountain inabidi zitoke jamaa wa Brazil aje ajenge na Familia yake.

--------

Wawekezaji hao wanatarajia kuwekeza kwenye sekta ya miundombinu, viwanda na utalii katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegeto.

Akizungumza na Nipashe ofisini kwake hivi karibuni, Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine, alisema mpango huo unalenga kuboresha miundombinu pamoja na kukuza sekta ya utalii utakaogharimu Sh. bilioni 150.

Alisema makubaliano hayo yanahusisha wawekezaji kutoka nchini Brazil katika Jiji la Rio de Janeiro, ambao walifika jijini humo, kuangalia fursa za uwekezaji katika miundombinu, viwanda na utalii.

Costantine alisema maeneo mengine ambayo wawekezaji hao wanayalenga ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha pembejeo za kilimo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Kanda ya Ziwa.

“Sehemu zingine ni ujenzi wa barabara pamoja na nyumba za ghorofa katika milima mbalimbali ambayo inaangalia ufukwe wa Ziwa Victoria,” alisema.

Alitaja sehemu zingine watakazozigusa kuwa ni pamoja na kutengeneza eneo la ufukwe wa Ziwa Victoria sehemu ya kliniki, Nera jirani na kituo cha polisi wa majini ambalo litatengenezwa na kuwa sehemu za uwekezaji na utalii.

Constantine alisema mpango huo utasaidia ukuaji wa uchumi wa Jiji la Mwanza na mtu mmoja mmoja.

Alisema wawekezaji hao wana umoja wao nchini Brazil unaojulikana kama ‘Africa Unity’ na mpaka sasa wamewekeza nchini Dubai na Ethiopia.

Aliongeza kuwa katika makubaliano ya mpango huo, Jiji la Mwanza litatoa ardhi na wawekezaji watatoa mtaji, teknolojia na mradi huo utakapokamilika utanufaisha pande zote mbili.

ULIPAJI FIDIA
Akizungumzia uwekezaji wa maeneo ya milimani, Constantine alisema, jiji limepewa jukumu la kulipa fidia katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegoto ambayo yapo mlimani ili kupisha uwekezaji huo.

Constantine alisema wawekezaji hao wamekubaliana na jiji litafute ardhi na kukamilisha mipango yote ndani ya miezi mitatu kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu kabla ya kazi hiyo kuanza.

Aliongeza kuwa wawekezaji hao wanaendelea kutafuta maeneo mengine ya kuwekeza ikiwamo mikoa ya Dodoma na Arusha.

Chanzo: Nipashe
Haya, tukitoka huko tunaingia Posta,Dar es Salaam.
 
Mimi kwetu Igogo, Naunga mkono wahamishwe.

Ukiangalia vizuri pale igogo ni karibu kabisa na mjini kati ambapo ni eneo zuri sana kibiashara pia limepakana na ziwa ambapo zinaweza jengwa hotels n.k

Ujenzi wa kwenye mawe ni gharama ndomana wakazi wengi wa igogo wanishi kwenye nyumba za zamani ambazo nyingi zimechakaa sana.

Wakazi wa igogo hawana uwezo wa kupaendeleza pale.

Kuna baadhi ya matajiri wao waliona fursa mapema igogo wakawa wanawaamisha watu.
 
Hasara gani? Anauziwa nani? China wangeendelea kuwachekea wajinga kama nyie isingekuwepo pale ilipo..

Maendeleo yana gharama ikiwemo kufyeka wajinga kama nyie,MKapa aliwafukia kule kwenye migodi walipoleta ubishi wa kitoto.
Mkapa wako sasa hivi ana tofauti gani na hao aliowafukia si, tena bora aliowafukia maana yeye anaoza huko kuzimu.

Unasifia ujinga wa kuuza nchi kwa mikataba isiyo na masilahi na taifa.

Walifukia watu kwenye migodi ili wawekeze kwenye dhahabu mpaka Jiwe ndio akaja kutusanua kwamba jamaa wanasomba dhahabu bure. Kusifia upuuzi kama huu ndio kuwa na akili wewe punguani?

Mikataba ya miaka kibao watu wanachukua rasilimali za nchi bure ndio maendeleo?

Sijawahi kuona chawa mpumbavu kama wewe.
 
Mkapa wako sasa hivi ana tofauti gani na hao aliowafukia si, tena bora aliowafukia maana yeye anaoza huko kuzimu.

Unasifia ujinga wa kuuza nchi kwa mikataba isiyo na masilahi na taifa.

Walifukia watu kwenye migodi mpaka Jiwe ndio akaja kutusanua kwamba jamaa wanasomba dhahabu bure. Kusifia upuuzi kama huu ndio kuwa na akili wewe punguani?

Mikataba ya miaka kibao watu wanachukua rasilimali za nchi bure ndio maendeleo?

Sijawahi kuona chawa mpumbavu kama wewe.
Tofauti ipo yeye kaacha familia yake kwenye neema
 
Lakini mkuu, sio vyema kuita nyumba za wenzio uchafu, hata hio nyumba yako nzuri kwa wengine ni choo tena cha kujisaidia wageni, tembea uone.
Hizi sio nyumba ni mabanda hata pa kuweka kimba zao hakuna..

Au maana ya Nyumba siku hizi imebadilika? Acha unafiki,Hizi ni nyumba? 👇
 

Attachments

  • IMG-20220509-WA0008.jpg
    IMG-20220509-WA0008.jpg
    44.5 KB · Views: 3
Vile vibanda pale mlimani vibomolewe tu,ile sehemu kama tunapata muwekezaji ni sehemu nzuri sana kwa utalii
 
Back
Top Bottom