Waislamu kwenye ndoa na mazishi wametuacha mbali sana Wakristo

Waislamu kwenye ndoa na mazishi wametuacha mbali sana Wakristo

Nilitaka niolewe nyumbani wakataja mahari jamaa akasema ngoja ajipange. Alirudi baada ya mwaka nikawa nimebadili mawazo. Ningekuwa muislamu ningeshaolewa. Ila daah jamani hizi mahari zetu za kikristo sio fair. Yani wenzio wamemla buuure na wataendelea kumla tu bila kulipa hiyo mahari. Halafu wewe unaenda kutoa milioni kadhaa? Dah poleni wanaume.

Shida kubwa ipo hapa; kwa Wakristo mahari ni pesa/mali wanayolipwa Wazazi wa binti wakati kwa Waisilamu mahari ni pesa/mali ya binti anayeolewa hivyo kwa Waisilamu binti ndiye anayetaja thamani ya mahari yake mwenyewe, na jambo hili linatoa heshima kwa muolewaji kwani yeye akitaja mahari yake na ikiwa ni yake mwenyewe huyo binti anakuwa sio kama Bidhaa inayouzwa kwa mume tofauti na wazazi wakitaja na kupokea mahari ya binti yao ambapo inakuwa ni sawa wamemuuza binti yao kama Mbuzi kwa mume kitu ambacho wakati mwingine hupelekea mabinti kunyanyasika vibaya katika ndoa zao kwani unaweza kumsikia mume akimtamkia mkewe; "Mimi usinichezee unajua nimetoa kwa wazazi wako ngombe 100 kwa ajili yako??!"--- tena hapo mwanaume kafura kwa hasira kali kisa labda mkewe alijisahau kumtengea maji ya kuoga bafuni, 😀😀
 
Nilitaka niolewe nyumbani wakataja mahari jamaa akasema ngoja ajipange. Alirudi baada ya mwaka nikawa nimebadili mawazo. Ningekuwa muislamu ningeshaolewa. Ila daah jamani hizi mahari zetu za kikristo sio fair. Yani wenzio wamemla buuure na wataendelea kumla tu bila kulipa hiyo mahari. Halafu wewe unaenda kutoa milioni kadhaa? Dah poleni wanaume.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilitaka niolewe nyumbani wakataja mahari jamaa akasema ngoja ajipange. Alirudi baada ya mwaka nikawa nimebadili mawazo. Ningekuwa muislamu ningeshaolewa. Ila daah jamani hizi mahari zetu za kikristo sio fair. Yani wenzio wamemla buuure na wataendelea kumla tu bila kulipa hiyo mahari. Halafu wewe unaenda kutoa milioni kadhaa? Dah poleni wanaume.
Ndugu zangu japo mimi ni mkristo ila hawa ndugu zetu waislamu linapokuja suala la ndoa na mazishi huwa hawana mambo mengi.

Mtu anafariki leo kesho mapema tu anazikwa kama hakutokuwa na safari ya kumsafirisha.

Kwenye ndoa nako hakuna kuremba watu wamependana wakatambulishana kijana wa kiume akaridhia mahari dhidi ya binti ni fasta to ndoa inafungwa.

Mahari zenyewe ni kawaida tu si kama huku kwetu, wanachojali wao ni watu waowane na ndio maana ni ngumu sana kukuta jamii nyingi za waislamu wanaishi pamoja bila ndoa.
Siku zote huwa nasema kuwa, Wakristo ni njia nyembamba inayoonwa na kupitwa na wachache, wengi wenu mma majina ya Kikristo au mnaupenda Ukristo au mmerithishwa Ukristo au na Mashabikintu na wapenzi wa Ukristo lakini kamwe si Wakristo na hamjawahi kuwa.

Ni wapi katika Ukristo mliapangiwa au mlifundishwa kiasi cha mahari mnachotakiwa kutoa? Ni wapi mlifundishwa mfanye sherehe kubwa za kufahari?
Ni wapi mlifundishwa kufanya misiba na maziko ya kifahari?
Watu mnajiamulia wenyewe kuishi mifumo yenu ya kimaisha halafu mnasingizia dini.

Mbona Wakristo wa huko Ulaya, Marekani na kwingineko nje ya Afrika hawafanyi mambo ya ndoa na maziko kifahari? Wengine hata mahari hazitolewi?
Mfumo wa ufungishaji ndoa wa bomani ulitumiwa ma wakoloni wakiuleta kutoka huko kwao. Mbona ndoa za Bomani leo hii huwa hatuzioni zikiwa na hizi mbwembwe?

Mkubali tu kwamba wengi huwa mnajidhania kuwa ni Wakristo ila kiuhalisia mpo nje kabisa ya Ukristo.
Ukristo unapaswa uutafute, unakuhitaji ujikane kweli, sasa dini inayokutaka ujikane na uichague yenyewe dhidi ya mali itakufundishaje kuishi maisha ya kifahari? Kwa uwezo na mali zipi ulizo nazo?
 
Shida kubwa ipo hapa; kwa Wakristo mahari ni pesa/mali wanayolipwa Wazazi wa binti wakati kwa Waisilamu mahari ni pesa/mali ya binti anayeolewa hivyo kwa Waisilamu binti ndiye anayetaja thamani ya mahari yake mwenyewe, na jambo hili linatoa heshima kwa muolewaji kwani yeye akitaja mahari yake na ikiwa ni yake mwenyewe huyo binti anakuwa sio kama Bidhaa inayouzwa kwa mume tofauti na wazazi wakitaja na kupokea mahari ya binti yao ambapo inakuwa ni sawa wamemuuza binti yao kama Mbuzi kwa mume kitu ambacho wakati mwingine hupelekea mabinti kunyanyasika vibaya katika ndoa zao kwani unaweza kumsikia mume akimtamkia mkewe; "Mimi usinichezee unajua nimetoa kwa wazazi wako ngombe 100 kwa ajili yako??!"--- tena hapo mwanaume kafura kwa hasira kali kisa labda mkewe alijisahau kumtengea maji ya kuoga bafuni, [emoji3][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatareee sanaaaa.
 
Mbona kila siku ni matangazo ya kuunadi tu Uislamu ukilinganishwa na Ukristo, inamaana Uislamu wenyewe umeshindwa kujitangaza kwa maudhui safi na matendo mema popote pale duniani?

Nina wasiwasi sana juu ya hii dini isijekuwa hivi [emoji117] "Kizuri huwa chajiuza bali kibaya hujitangaza".

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Wakiachana vipi kuhusu watoto watalelewa na Nani?

Na kwa Wakristo wakiachana kwa kosa la uzinifu watoto watalelewa na nani??-- watalelewa na hao hao wazazi kwani kuachana ni kifo??!

Kumbuka sio kila kosa kwa Mume au mke katika uisilam dawa yake ni talaka, katika maisha ya ndoa kunaweza kutokea kutoelewana kati ya mume na mke kiasi kwamba hatari ya kutoana roho ikajitokeza, sasa katika hali hiyo busara ni kuacha watoane roho au kutengana kisheria kupitia talaka??, bila shaka kuachana kwa talaka ni busara kwani kama mmoja akimtoa roho mwenzake na huyo aliyemtoa roho naye akafungwa maisha nk, huoni watoto watabaki katika UYATIMA mkubwa??!!, ni bora talaka na watoto watalelewa na hao hao wazazi japokuwa maisha yao hayatakuwa ya malezi ya pamoja lakini hiyo ni bora sana kuliko kulelewa na Wazazi wasiolewana na pengine kutoelewana huko kukavuka mipaka na kusabisha irreparable danger.
 
Nilitaka niolewe nyumbani wakataja mahari jamaa akasema ngoja ajipange. Alirudi baada ya mwaka nikawa nimebadili mawazo. Ningekuwa muislamu ningeshaolewa. Ila daah jamani hizi mahari zetu za kikristo sio fair. Yani wenzio wamemla buuure na wataendelea kumla tu bila kulipa hiyo mahari. Halafu wewe unaenda kutoa milioni kadhaa? Dah poleni wanaume.
Una maanisha aliporudi baada ya mwaka hukukubali akuoe tena?
 
Hamia kwao
Kila dini na taratibu zake
Mbona sisi tumewaacha mbali kwenye umiliki wa shule hospital vyuo

Hapo hujilinganishi nao

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumiliki shule na hospital ni utashi wa watu mwenyewe. Lkn ukiristo hakuna sehemu unasema mmiliki hivyo vitu.
Uislam ndio unasema ndoa, kislim, kuzika vifanyike haraka Sana
 
Mbona kila siku ni matangazo ya kuunadi tu Uislamu ukilinganishwa na Ukristo, inamaana Uislamu wenyewe umeshindwa kujitangaza kwa maudhui safi na matendo mema popote pale duniani?

Nina wasiwasi sana juu ya hii dini isijekuwa hivi [emoji117] "Kizuri huwa chajiuza bali kibaya hujitangaza".

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app

Wewe ni mkristo kweli??, je unajua kauli ya Yesu alipowaambia wanafunzi wake kwamba Waende duniani kote kuitangaza injili kwa kila kiumbe??-- kutangaza injili kwa kila kiumbe (hata kwa panya, mende nk) huko sikokutangaza Ukristo??, je nako huko utakuitaje??, kibaya chajiuza---?? I doubt with your christianity..

Read, Marko 16:15.
 
Ndugu zangu japo mimi ni mkristo ila hawa ndugu zetu waislamu linapokuja suala la ndoa na mazishi huwa hawana mambo mengi.

Mtu anafariki leo kesho mapema tu anazikwa kama hakutokuwa na safari ya kumsafirisha.

Kwenye ndoa nako hakuna kuremba watu wamependana wakatambulishana kijana wa kiume akaridhia mahari dhidi ya binti ni fasta to ndoa inafungwa.

Mahari zenyewe ni kawaida tu si kama huku kwetu, wanachojali wao ni watu waowane na ndio maana ni ngumu sana kukuta jamii nyingi za waislamu wanaishi pamoja bila ndoa.
Mbusu jiwe unapojifanya mkristo
 
Kuna watu huwa wanafanya dhihaka kuwa waislamu mahari ndogo na bla bla kibao,hawajui lengo ni kufanya ndoa iwe nyepesi ili watu wafunge ndoa waepuke zinaa,lkn upande wa pili kwakuwa hamuogopi dhambi huwa mnadunda Tu!
Hii nimeipenda watu waepuke zinaa ,hivi na kuachana ikoje ,ama ndio Ile kuwa muishi ndani mwezi bila kusemeshana ndio urudi kuwa bado nahitaji kumpati talaka.

Kuna mmoja alishatoa kadi akadai minimum iwe 100k mchango
 
Back
Top Bottom