Kitu kikiwa kirahisi pia kina gharama yake.Mfano kwa waislam mtu akimchoka mke hakuna kuvimiliana ni either talaka au analetwa mwenzio.Nikimchoka mume naomba talaka chap nawahi penye manufaa.Hii ya mazishi hivi mzazi kafa let's nipo Dar yeye yuko Tabora haina haja ya kusubiri ni anazikwa tu.Binafsi uislamu dini nzuri ila ndoa na mazishi hapana jmn
annatee Swala la kuoa msingi wake ni kuhalarishwa na kusitirika pia kutambuana ili isije watu wakaingiliana kimapenzi na wakati ni ndugu au unaweza mpenda mtu kumbe alikua mume au mke wa mzazi wako ama kaka yako, kabla yako mwisho ukalaanika na mungu ndo maana tukakatazwa kuzini hadi ndoa kwanza, kwaiyo swala la kufanya ndoa kua na ugumu au mizunguko kwenye kuoa halina uhusiano wowote kwenye swala la kudum kwa ndoa, kwasisi waislam mtu akitangaza nia ya kuoa na ikiwa mchumba wake ameridhia kuolewa nae af mtu katikati ulete mizinguko isiyokua na maana bas iyo ndoa ikishindikana na hao wakaenda kuzini huko kwingine nawe utakua mwenye dhambi kama wao.
Issue ya kuoa kuacha, kuolewa kuachika, au kuongeza mke ni swala la mtu binafsi na wala sio dini iwe kwa wakristu ama waislam, kumbuka ni ndoa nyingi zinavunjika na zipo nyingi zinadumu pia kwa pande zote wakristo na waislam chamsingi nikujitambua, ukifuata na kuheshimu miiko na maadili ya dini yenu wewe na mwenza wako mtadumu sana kwenye ndoa ila mmoja wenu au nyote akiwa na dhamila tofauti na malengo ya mungu kwenye ndoa basi hamtadumu hata muwe mmezungushwa kias gani na hata viapo vyadamu.
“Nasisitiza waislam tumeruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja ila hatujalazimishwa” pia kuna taratibu zake, hii ulosema kua ukimchoka mtu unaoa mke mwingine ni swala la mtu binafsi sio mafundisho ya dini wala mtume kipenzi chetu hakuwahi kufanya ivo kwa wake zake ndo maana ilo swala likawa hiari mtu kama unaweza fanya kama huwezi acha, ukiforce kuoa mke zaidi ya mmoja na ukamfanya mwingine ndoa kwake ikawa msiba kilasiku unamtesa ni unapata dhambi na utadhibiwa siku ya mwisho.
Mwisho swala la kuzika kama ilivyo kwenye ndoa sisi hua hakuna cha nini wala nini japo hekma inaweza tumika kulingana na uhusika wa kifo chenyewe wala sio cheo au ukubwa wa marehemu tofauti na apo inakua sio sawa kidini, mtu akishakufa amekufa ni watu mnaweka hisia tuu na mnaacha uhalisia ndo maana wengine wamefikia hatua ya kupiga picha maiti na picha zingine misibani sio sawa, mambo yakusubiriana kwanza mnaweka msiba kua mkubwa pasipo na maana watu wanaprint tshirt za picha za marehemu end etc MTU AKISHAKUFA AMEKUFA haki yake ni kuzikwa tuu ayo mengine ni mbwembwe kwenye macho ya watu wala mungu hayaitaji ayo.
Tusamehane huandishi wangu sio mzuri.