Waislamu kwenye ndoa na mazishi wametuacha mbali sana Wakristo

Waislamu kwenye ndoa na mazishi wametuacha mbali sana Wakristo

Nilitaka niolewe nyumbani wakataja mahari jamaa akasema ngoja ajipange. Alirudi baada ya mwaka nikawa nimebadili mawazo. Ningekuwa muislamu ningeshaolewa. Ila daah jamani hizi mahari zetu za kikristo sio fair. Yani wenzio wamemla buuure na wataendelea kumla tu bila kulipa hiyo mahari. Halafu wewe unaenda kutoa milioni kadhaa? Dah poleni wanaume.
Sasa kwanini ulimtolea nje jamaa mara ya pili!
 
Nilitaka niolewe nyumbani wakataja mahari jamaa akasema ngoja ajipange. Alirudi baada ya mwaka nikawa nimebadili mawazo. Ningekuwa muislamu ningeshaolewa. Ila daah jamani hizi mahari zetu za kikristo sio fair. Yani wenzio wamemla buuure na wataendelea kumla tu bila kulipa hiyo mahari. Halafu wewe unaenda kutoa milioni kadhaa? Dah poleni wanaume.
Na wewe unagawa uroda bure,??

Kama unalijua hilo kwann basi usimtunzie mumeo??
 
Kitu kikiwa kirahisi pia kina gharama yake.Mfano kwa waislam mtu akimchoka mke hakuna kuvimiliana ni either talaka au analetwa mwenzio.Nikimchoka mume naomba talaka chap nawahi penye manufaa.Hii ya mazishi hivi mzazi kafa let's nipo Dar yeye yuko Tabora haina haja ya kusubiri ni anazikwa tu.Binafsi uislamu dini nzuri ila ndoa na mazishi hapana jmn

annatee Swala la kuoa msingi wake ni kuhalarishwa na kusitirika pia kutambuana ili isije watu wakaingiliana kimapenzi na wakati ni ndugu au unaweza mpenda mtu kumbe alikua mume au mke wa mzazi wako ama kaka yako, kabla yako mwisho ukalaanika na mungu ndo maana tukakatazwa kuzini hadi ndoa kwanza, kwaiyo swala la kufanya ndoa kua na ugumu au mizunguko kwenye kuoa halina uhusiano wowote kwenye swala la kudum kwa ndoa, kwasisi waislam mtu akitangaza nia ya kuoa na ikiwa mchumba wake ameridhia kuolewa nae af mtu katikati ulete mizinguko isiyokua na maana bas iyo ndoa ikishindikana na hao wakaenda kuzini huko kwingine nawe utakua mwenye dhambi kama wao.

Issue ya kuoa kuacha, kuolewa kuachika, au kuongeza mke ni swala la mtu binafsi na wala sio dini iwe kwa wakristu ama waislam, kumbuka ni ndoa nyingi zinavunjika na zipo nyingi zinadumu pia kwa pande zote wakristo na waislam chamsingi nikujitambua, ukifuata na kuheshimu miiko na maadili ya dini yenu wewe na mwenza wako mtadumu sana kwenye ndoa ila mmoja wenu au nyote akiwa na dhamila tofauti na malengo ya mungu kwenye ndoa basi hamtadumu hata muwe mmezungushwa kias gani na hata viapo vyadamu.

“Nasisitiza waislam tumeruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja ila hatujalazimishwa” pia kuna taratibu zake, hii ulosema kua ukimchoka mtu unaoa mke mwingine ni swala la mtu binafsi sio mafundisho ya dini wala mtume kipenzi chetu hakuwahi kufanya ivo kwa wake zake ndo maana ilo swala likawa hiari mtu kama unaweza fanya kama huwezi acha, ukiforce kuoa mke zaidi ya mmoja na ukamfanya mwingine ndoa kwake ikawa msiba kilasiku unamtesa ni unapata dhambi na utadhibiwa siku ya mwisho.

Mwisho swala la kuzika kama ilivyo kwenye ndoa sisi hua hakuna cha nini wala nini japo hekma inaweza tumika kulingana na uhusika wa kifo chenyewe wala sio cheo au ukubwa wa marehemu tofauti na apo inakua sio sawa kidini, mtu akishakufa amekufa ni watu mnaweka hisia tuu na mnaacha uhalisia ndo maana wengine wamefikia hatua ya kupiga picha maiti na picha zingine misibani sio sawa, mambo yakusubiriana kwanza mnaweka msiba kua mkubwa pasipo na maana watu wanaprint tshirt za picha za marehemu end etc MTU AKISHAKUFA AMEKUFA haki yake ni kuzikwa tuu ayo mengine ni mbwembwe kwenye macho ya watu wala mungu hayaitaji ayo.

Tusamehane huandishi wangu sio mzuri.
 
Aisee hkn muislam anatakiwa afanye nje ya dini yake kuacha ni halal na kuongeza mke ni halal isipokuwa lazima asbb ziwepo sio tu una mkera mwenzio ndo umuache unaweza ukawa huna mapenz naye ukamuacha ni ruksa kbs
 
Ni mwanamke wa kiislamu. Tena ilikuwa hivi.
Tupo kwenye basi tunatoka Arusha sasa njiani basi likasimama kupisha watu waliokuwa wamebeba mwili wa ustadhi wanaupeleke mkisikitini kuuswalia na wapo wanaume tu.
Ndiyo mtu mmoja akauliza, kwanini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika? Likatoka hilo jibu

[mention]Hoffenheim [/mention] kabla ya yote kwanza fahamu ni makosa kwenye matukio yoyote ya kiislam mwanaume kuchanganyana na mwanamke kuna sababu nyingi ndani yake ntakupa ukihitaji, kuzika ni tukio na ndani yake kuna ibada na ibada inahitaji utakatifu na utulivu ili isije badara ya kumtukuza mungu tukawa tunamkufuru, wanawake hawajakatazwa kuzika ila makatazo yao yapo kwenye vitu kabla ya tukio kama kuchanganyika na wanaume ila kama hakutokua na wanaume wa kumsitiri marehemu basi wanawake wanaruhusiwa kufanya ivyo jambo ambalo sio rahisi kutokea.

Pia nje ya mada rasmi wanawake hawana kazi kwenye ilo zoezi ukizingatia nature ya maumbile yao, hasa ukianza na kuchimba kaburi, kubeba mwili/jeneza, kuswalia maiti (wanawake hawaruhusiwi kuongoza swala yotote ikiwa wanaume wapo), tatu kuzika yani kuingia kaburini na kushusha mwili ndani ya kaburi hadi kufukia na kuombea mwili ila wanaruhusiwa kushiriki kumwombea dua marehemu baada ya kuzika.

Kwa iyo hata wewe unaweza kuona hakuna haja ya wao kufanya izo ikiwa ni nzito kidgo kwao na mwisho ndo ilo unalosema kwasisi waislam sio swala zuri kulia kwa kuanguka kugaragara kurukaruka ama kupiga yowe ama kutoa sauti kwa kulalamika na ukingalia wanawake wengi hua hawawezi kuhimili kuzika bila ayo mambo ndo maana ikawa ivo ili kutomkufuru mwenyezi mungu maana swala la kifo nilakumshukuru mungu kama alivokupa ndo amechukua kwaiyo kwanini umlaumu as if mungu kafanya makosa makubwa na kuna wengine ufikia hatua mbaya ya kukufuru utasikia mtu anapiga yowe anasema MIMI NITAISHIJE JAMANI FULANI UMEONDOKA na mengineyo utazani uyo aliyekufa ndo alikua mungu wake.
 
Back
Top Bottom