Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Mtoto anaesoma english medium anaweza kuzungumza kiingereza vizuri tu kama kajifunza tangu mdogo hadi kufikia darasa la 5 au 6 flani hivi. Kwanini? Kwasababu anajifunza lugha ya kiingereza na anafanya mazoezi jinsi ya kuongea au kuwasiliana kwa kiingereza.

Mtoto anayesoma madrasa hajifunzi lugha ya kiarabu wala hafanyi mazoezi ya kuongea au kuwasiliana kwa lugha ya kiarabu ila anajifunza aya zilizoandikwa kiarabu kwa kukaririshwa kumbuka madrasa mtoto mdogo anakaririshwa aya tu haambiwi maana ya hizo aya mpaka awe mkubwa ndio anaanza kukaririshwa tafsiri ya baadhi ya aya so anakuwa anajua aya na tafsiri zake but lugha anakuwa hajui.
 
Hakuna tatizo mkuu, kinachonishangaza ni kwamba huwa siwaoni mkizungumza kiarabu kati yenu zaidi ya salamaleko na kunukuu aya za quran tu.

Ukiona hivyo ujue ya kuwa hawana vocabularies zingine zaidi ya zile za swala 5.
Ni kama shule za kayumba, Kiingereza kinaishia mlangoni wanapotoka darasani. Nje ya pale ni kiswahili na vilugha vingine kwa kwenda mbele.
Thus, linguistic environment is not supporting the development of English. Hata kwa waislam ni vivyo hivyo, wataishia kujua kiarabu cha ndani ya madrasa. Nje ya hapo hakuna kitu.
 
Ni abrakadabra tu hakuna cha kueleweka zaidi ya kuchanganya watoto tu. Unakuta mtoto anapelekwa englishi medium akajifunze kiingereza na jioni anaenda madrasa kukaririshwa kiarabu cha dini. Huyo mtoto wa kiswahili hapo ataelewa nini kama si ujinga tu?
 
Just imagine wewe haujui lugha ya kiingereza ukapewa kijitabu kilichoandikwa kwa lugha ya kiingereza ukakariri kila kilichoandikwa kwenye hicho kitabu cha kiingereza, imagine ukakariri na tafsiri ya kila kilichoandikwa kwenye hicho kitabu kwa kusaidiwa na mtu ambaye anajua hayo maneno yanavyotamkwa na kuandikwa na tafsiri yake je kwa kufanya yote hayo utakuwa unajua lugha ya kiingereza? Tukikusimamisha mbele ya watu utaweza kuongea? Ukikutana na mzungu naweza kupiga stori?
 
Hoja yako siipingi, labda ngoja nikupe hoja yangu nadhani itakua rahisi kuona nachokilenga. Mi nakaa uswahili ukichukua sampo hata ya watoto 10 ukiwauliza wewe upo sura gani wanataja vizuri tu na kurecite but wakimaliza kila mmoja ukimuuliza ina maana gani wengi huwa wanachemka. Kuchemka kwa watu wengi maana yake haijapewa msisitizo.

Ndo maana mi binafsi naona inatakiwa kupewa kipaumbele kikubwa sana ili kueliminate hiyo unasema "kwa mwanafunzi aliyezingatia mafunzo vyema" Yani iwe yeyote anayeenda madrasa awe na uwezo wa kuelewa kile anachosoma kwa wepesi zaidi, ili hata akisikia random sura ambayo hajasoma anakua anaelewa nini kinaongelewa

HIi ni experience na mtizamo wangu kuyoka huku uswahili nilipo

Hapo imeeleza vyema kabisa. Lakini ukweli ni huu. Huwezi mpata mtu hata mmoja ambaye atakijua kiarabu kwa ufasaha kwa kusoma madrasa pekee. Lugha ina mambo mengi. Moja wapo ni mazingira ya lugha (linguisticenvironment). Mazingira ya lugha hayamfanyi mtu kujua kiarabu. Kwa maana mazingira ya kujifunza lugh ndani na nje ya madrasa ni tofauti. Ndani ya madrasa kiarabu kinafundishwa. Nje ya madrasa kiswahili kimetamalami. Katika mazingira hayo ataimarishaje uweo wake wa kiarabu? Ndiyo maana Yoda anauliza mbona mkikutana mtasalimiana vizuri tu kiarabu, lkn baada ya hapo wataendelea kiswahili. That's very fun.
 
Kweli mku, nakuunga mkono tena aibu kubwa kwa waislam wa sasa, hatusomi Kiarabu wengine tunasoma lugha za makafiri badala ya kujifunza lugha yetu. Ijapokuwa kujifunza lugha ya makafiri sio dhambi lkn vijana wengi wa kiislamu wamejikita huko

Nakwambieni enyi waislam, ni suala la muda tu kuruwan kuwa obsolete. Unajua watu wa kizazi hiki reasoning yao iko tofauti sana. Mfano mpaka sasa hamjawapa sababu za msingi kwa nini tuabudu kwa kiarabu tu, ilhali Mwenyezi Mungu ni wa wote. Uarabu kuna uasi mkubwa sana unaendelea dhidi ya uislam. Ndiyo maana wengi wanahamia nchi za makafiri badala ya nchi za kiarabu.
 
Ni abrakadabra tu hakuna cha kueleweka zaidi ya kuchanganya watoto tu. Unakuta mtoto anapelekwa englishi medium akajifunze kiingereza na jioni anaenda madrasa kukaririshwa kiarabu cha dini. Huyo mtoto wa kiswahili hapo ataelewa nini kama si ujinga tu?
Mafunzo ya dini ni zaidi ya kusoma Quran ukiona watoto wanaenda madrassa kuna mengi wanajifunza
 
Nakwambieni enyi waislam, ni suala la muda tu kuruwan kuwa obsolete. Unajua watu wa kizazi hiki reasoning yao iko tofauti sana. Mfano mpaka sasa hamjawapa sababu za msingi kwa nini tuabudu kwa kiarabu tu, ilhali Mwenyezi Mungu ni wa wote. Uarabu kuna uasi mkubwa sana unaendelea dhidi ya uislam. Ndiyo maana wengi wanahamia nchi za makafiri badala ya nchi za kiarabu.
uasi wa waarabu haufanyi kiarabu kiwe haram brother , na kutumia kiarabu kwenye swala haimaanishi kuwakuza waarabu , dini kukua au kufifia hilo halitakuongezea wala kukupunguzia kitu kwenye maisha yako , sisi ndo tunatakiwa kujishughulisha na hilo
 
Nakwambieni enyi waislam, ni suala la muda tu kuruwan kuwa obsolete. Unajua watu wa kizazi hiki reasoning yao iko tofauti sana. Mfano mpaka sasa hamjawapa sababu za msingi kwa nini tuabudu kwa kiarabu tu, ilhali Mwenyezi Mungu ni wa wote. Uarabu kuna uasi mkubwa sana unaendelea dhidi ya uislam. Ndiyo maana wengi wanahamia nchi za makafiri badala ya nchi za kiarabu.
Muislam tofauti na Wakiristo. Hata wewe ukisilimu mawazo mgando hayo hutakuwa nayo
 
Muislam tofauti na Wakiristo. Hata wewe ukisilimu mawazo mgando hayo hutakuwa nayo

Mawazo mgando ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu anakubali sala kwa lugha moja tu. Ilhali watu na Lugha zao ni malia Yake
 
Hapo imeeleza vyema kabisa. Lakini ukweli ni huu. Huwezi mpata mtu hata mmoja ambaye atakijua kiarabu kwa ufasaha kwa kusoma madrasa pekee. Lugha ina mambo mengi. Moja wapo ni mazingira ya lugha (linguisticenvironment). Mazingira ya lugha hayamfanyi mtu kujua kiarabu. Kwa maana mazingira ya kujifunza lugh ndani na nje ya madrasa ni tofauti. Ndani ya madrasa kiarabu kinafundishwa. Nje ya madrasa kiswahili kimetamalami. Katika mazingira hayo ataimarishaje uweo wake wa kiarabu? Ndiyo maana Yoda anauliza mbona mkikutana mtasalimiana vizuri tu kiarabu, lkn baada ya hapo wataendelea kiswahili. That's very fun.
hoja yako ya mazingira wezeshi nakubaliana nayo ndo vitu kama jamii vya kuamua na kuangalia solution ni nini.
point ya "mkikutana mtasalimiana" sjajua kwanini umeniuliza mimi hilo swali maana hakuna sehemu nilitaja mimi ni muumini wa sehemu fulani. ila kama unataka maoni yangu mi naonaga wazee wangu wakikutana wanasalimiana kilugha baada ya hapo wanatwanga stori za hapa na pale kwa kiswahili.

kucement hoja ya muda mrefu muslim community kujifunza lugha iwe msisitizo kwenye jamii zetu
 
Mawazo mgando ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu anakubali sala kwa lugha moja tu. Ilhali watu na Lugha zao ni malia Yake
Kama waislam wenyewe wameridhika na mfumo wao wa maisha inatosha ,kama ambavyo sisi hatuhoji wale manabii wanaonena kwa lugha zisizoeleweka coz nyi wenyewe mmeridhika sisi haituhusu
 
Quran imeandikwa kiarabu ila kiarabu si Quran maandishi ya kiarabu yanatofautiana na ya kwenye Quran kwa kuwa huwa hayana irabu(aeiou) kwa hyo anaesoma Quran tupu hawez kusoma kiarabu unless amesoma kiarabu ama kwa lugha nyingine kiarabu kinasomwa kwa kujua maana na muundo wa maneno.
Qu'ran imejengwa juu ya herufi 28 za hijaa ambazo kwa hizo ndo kiarabu chote kimejengwa hapo, hakuna herufi zaidi ya hizo sasa maneno yako kiasi kama sijayaelewa.
 
Mawazo mgando ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu anakubali sala kwa lugha moja tu. Ilhali watu na Lugha zao ni malia
Kwanini wakiristo waende makanisani na wasiabudu majumbani? MUNGU hayupo majumbani?
 
Nakwambieni enyi waislam, ni suala la muda tu kuruwan kuwa obsolete. Unajua watu wa kizazi hiki reasoning yao iko tofauti sana. Mfano mpaka sasa hamjawapa sababu za msingi kwa nini tuabudu kwa kiarabu tu, ilhali Mwenyezi Mungu ni wa wote. Uarabu kuna uasi mkubwa sana unaendelea dhidi ya uislam. Ndiyo maana wengi wanahamia nchi za makafiri badala ya nchi za kiarabu.
nchi za makafiri ni zipi mkuu? nitajie kama tano ili tujifunze mkuu
 
Mawazo mgando ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu anakubali sala kwa lugha moja tu. Ilhali watu na Lugha zao ni malia Yake
Kwanini wakiristo mnaenda kuabudu makanisani? Majumbani mungu hayupo? Kwanini upoteze muda wakati hata Mungu J2 nyumbani yupo?
 
Bro kama naleta siasa. Jifanye jeuri au jitoe ufahamu kwa kuswali swala 5 kwa lugha yako ya kiswahili au ya kabila lako.
Mungu anasema kwenye hiyo Quran , kuwa anasikia maombi ya mtu yoyote yule . Hata ukiswali kwa lugha yoyote anasikia.
 
Back
Top Bottom