Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Ile tafsiri ya "katiba yetu ni nzuri" aliyoitoa bi Kidude tafsiri yake ni katiba nzuri kwa kufanya uhuni na maamuzi yoyote bila kuwa na wasiwasi wa kuhojiwa au kushtakiwa .

Kwa kifupi katiba ile mwananchi si lolote bali wanaotawala ndio wanaweza kuamua hata kesho mtu apotee na wasihojiwe popote.

Haswaaaa.
 
Hivi kuna sehemu yeyote kwenye KATIBA imetamkwa Barua ya VP kujiuzulu ipelekwe kwa nani?View attachment 3660111

Na kwanini Rais aridhie kujiuzulu kwa mtu ambaye alipigiwa kura kama mate na sio kwa teuzi ya barua?

Sasa mbona Ndejembi kapendekezwa na CCM, na sio Rais Kumteua? Katiba inachezewa wazi wazi.
 
Wakati wa rafiki yangu, mimi naamini hakuyafanya yeye bali waliyawanya wao, yeye akawa Bangusilo na hii ilifanyika ili watu kama nyie mumchukie yeye.

Chukulia utekwaji wa Mo Dewji! isitoshe. Ukimsikiliza kwa makini sana Polepole utanielewa, japo kuna watu wamesha aminishwa kuwa utekaji na mauaji ilikuwa kazi ya Magufuli. Kwa wanamojua Magufuli kwenye IMANI ya KIROHO watakwambia sii mtu anayeweza fanya mambo yale.

MAGUFULI alikuwa Gaddafi wa Tanzania (Magufulification) ukimkosea, ukimuudhi anakuchana mbele za watu hafichi kutumbua mtu yeyote hadharani na hili liliwachukiza wengi ati udhalilishaji kwa nini isiwe siri

Niishie hapa, maana kama Polepole aliweza kupotezwa hata Makamu wa rais anaweza kupotezwa! Mimi nani wa kusimama kidume mbele ya mfumo kandamizi.
Kwenye kumtetea magufuli hapo unataka kudanganya na mimi sikubali unidanganye....Magufuli kwa kinywa chake alimtaka ndugai awashughulikie wabunge wenye mawazo mbadala huko ndani bungeni na wakitoka nje atawashughulikia yeye....magufuli huyohuyo aliwahi kuwashangaa wakurugenzi wanaowatangaza wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi....Magufuli huyohuyo lissu kapigwa risasi alikaa kimya bila kulizungumzia lile tukio hata kwa kulaani alishindwa....Magufuli huyohuyo aliunajisi uchaguzi wa serikali ya mitaa 2019
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wanasifia "Katiba yetu nzuri"
Wanasema wameridhia EN ajiuzulu
Wakafanya kikao na kupendekeza mtu mwingine
Wakampitisha Bungeni
Wakaenda kumuapisha Ikulu
Wakahamisha vimulimuli, ving'ora na saluti

Wenye kupiga makofi na vigelegele wakapiga...

Siku tano baadaye...

Aliyesemwa kajiuzulu hajaonekana... Wanaosifia Katiba nzuri hawatuambii kama hiyo Katiba imemlinda aliye"jiuzulu"...

Hakuna aliyeonesha hadi leo EN akisema amejiuzulu kwa hiari yake au hata kuonekana akikabidhi barua au ofisi kwa makamu mpya! Sasa ikitokea wanatuonesha mwili wake marehemu... na kujitokeza kutoa poleee... si bado watatuambia "Bwana ametoa, Bwana ametwaa"?

Kama Katiba hii ni nzuri sana... kuna ubaya gani EN aelezee bila mtutu wa bunduki sikioni alivyojiuzulu?

Maana kama VP anaweza kuondolewa tukaletewa mwingine... itakuwaje tuone Rais anatoweka, hatujui aliko, siku chache baadaye tunaambiwa "inna illahi wa inna lillahi rajioun", mwingine anaapishwa....

Inakukumbusha kitu chochote?

Swali: Ikitokea Nchimbi anaibuka na kusema hajajiuzulu Umakamu je, Ndejembi atakuwa bado halali?
Jaji Waliyoba Alimpigia simu akathibitisha Dr. Nchimbi mwenyewe kwamba "Nimeandika Barua ya kujiudhuru"

Kwa hoja kwamba vipi Kama ajajiudhuru ni hoja dhaifu.
 
Kosa kubwa la magufuli nipale aliweza kuikamata nchi na kila mtu akatulia, sasa yeye angetakiwa kuamrisha katiba mpya ipatikane na hili kwa uwezo wake angeweza kabisa, sasa yeye alihangaika na miradi mingi na vile sijui alijua atakaa milele?!. Angalia sasa miradi yake aliyobudi watesi wetu ndiyo wanatamba nayo.
 
Ni wakati sasa katiba mpya ilazimishe kujiuzulu kufanyike hadharani wakati tunamuona live mtu anayejiuzulu na ajieleze kwa wananchi sababu zake za kujiuzulu, ikiwezekana bungeni kabisa.

Hii habari ya kujiuzulu kisirisiri kwa barua za Twitter mtu anaweza kupandishiwa habari ya kujiuzulu na yeye akaiona Twitter tu.
Na hili liwe kwa Speaker pia. Hii mambo ya kufanyika (kufanyiana) gizani na pengine under mtutu wa bastola ni uhuni tu.
 
Unajichoshaga na maswali yasiyo na kichwa wala miguu. Mbona barua yake ya kujiuzulu ilisambaa mitandaoni. Suala la kutoonekana hadharani inawezekana ni uamuzi wake binafsi. Kwani we ulishawahi kuonekana hdharani? Nenda nyumbani kwake au waulize ndg zake
Nchimbi ni mali ya Umma , public lazima iwe concerned na whereabout zake
Makamu wa Rais haonekani a week huku tunaaminishwa kajiuzulu

How do you find it mzee especially kwa figure kama ile

Ujue CCM ni dumbs mkuu na hawana akili huwa movement zao ni kama zinafanywa na very low class people

Hiki walichofanya kina impact kubwa sana baadae
 
Nchimbi ni mali ya Umma , public lazima iwe concerned na whereabout zake
Makamu wa Rais haonekani a week huku tunaaminishwa kajiuzulu

How do you find it mzee especially kwa figure kama ile

Ujue CCM ni dumbs mkuu na hawana akili huwa movement zao ni kama zinafanywa na very low class people

Hiki walichofanya kina impact kubwa sana baadae
Bahati mbaya aliingia kwenye madaraka katika mazingira yenye utata yaliyoacha uchungu na maumivu kwa wengi. Kupata wengi wa kumlilia labda ubinadamu (na ile aliyosema ni kauli yake ya mwisho) uchukue mkondo wake, ila hiki cha MO29 ndiyo kinaweza kuwapa nguvu na upenyo watesi wake.
 
Back
Top Bottom