Ugumu wa kumpeleka Nchimbi mahakamani ni kwamba atakuwa anajua mambo mengi sana ambayo yanaweza kutoka katika cross examination.
Tayari wana kesi mbaya ya Lissu, wakiiongezea hii itawapa tabu sana.
Sasa hivi wapo katika hali ngumu sana kwa sababu hawawezi kumficha daima, na hawataki kumuachia.
Na kwa kumfukuza uanachama, ukiondoa suala la uhai wake na hayo mafao yao, hana cha kupoteza. Na Nchimbi ni mbishi tangu zamani hatakaa kimya. Na amepata support kubwa sana kitoka kwa watu wengibsana wanaoona anaweza kuwasaidia kuweka wazi madudi mengi aliyoyaona ndani ya CCM.
I was kind of disappointed kuona amejiuzulu kirahisi, lakini nikaanza kufikiri kama ulivyouliza, hivi tunajuaje hata kama amejiuzulu kweli?
Ikiwa Tanzania watu huwa wanateuliwa bila kukubali kwa kusikia redioni tu, kwa nini wasiweze "kujiuzulu" kwa kusikia redioni tu hivyo hivyo?
Angalau wamuachie tumsikie akubali mwenyewe kajiuzulu, sasa hivi hata kama habari aliyoitoa Jasusi Chahali kwamba ile barua hajaandika Nchimbi si kweli, ni vigumu kumbishia Chahali ikiwa Nchimbi mwenyewe hajulikani alipo na hata simu za watu hajibu.
Ngoja nitafute networks za watoto wa Oysterbay Primary maana wale wana za ndani za familia kabisa. Naona walikuwa wananitafuta hapa ila nilikuwa busy.