Research afanye nani? kabla ya chanjo kuruhusiwa kutumika Researh tayari, huyo kibwetele atafute vibwetele wenzake wakafanye research wao waje na majibu kua haifai
Ww haujui usemalo! Research ya kujua usalama wa dawa au chanjo unachukuaa muda mrefu kwa sababu zifuatazo:
1. Mnyama kama panya akidungwa atafuatiliwa kwa muda wa kutosha kutaka kujua kama kuna madhara ya moja kwa moja kwa mnyama husika, kama, mabadiriko hasi, ugumba, na hata kifo,
2. Kama hakuna madhara ya moja kwa moja kwa mnyama husika watataka kujiridhisha madhara kwenye uzao wake (kama atakuwa na uwezo wa kuzaa baada ya kudungwa),; kwamba watoto wake watakuwa wa kawaida au vilema, na je nao wataweza kuzaa watoto (wajukuu wa aliyechanjwa) wa kawaida, wasiokuwa na ulemavu au tabia zisizo za kawaida?
3. Hao wajukuu nao watafuatiliwa kufahamu kama kuna madhara nk
Kwa kutumia panya, ukizingatia ukuaji wao na 'metabolic rates' zao ni faster, matokeo yanaweza kuwa bayana ndani ya mwaka 1-2
4. Dawa au chanjo ikifaulu kwenye panya, hupelekwa kwenye wanyama mamalia wanaokaribiana sana na binadamu...hapa nyani , baadaye sokwe hawawezi kwepa! Huku nako yanafanyika kama ya kwenye panya. Lakini kwa kuzingatia mzunguko wa maisha wa nyani na sokwe(life cycle), matokeo kutoka kwa mnyama aliyedungwa mpaka kufikia mjukuu huchukua muda mrefu zaidi, hapa siyo chini ya miaka 5!
5. Baada ya kujiridhisha huko chini kwa wanyama wasio binadamu (takribani miaka 10) na kufaulu kuwa dawa au chanjo kweli inatibu au kukinga, na madhara haina yaliyo makubwa, huu ndio muda muafaka kufanya majaribio kwa binadamu, tena wasiozidi 100! Hawa nao watafuatiliwa kuona kama hiyo dawa 1)haina madhara makubwa 2) inatibu au kukinga ugongwa husika tena kwa kiwango kinachoridhisha?
6. Ikifaulu hapo idadi ya wakufanyiwa majaribio huongezwa, huku wakirekodi kila dhara ( side effect) na mafanikio ya dawa au chanjo husika huku wakifuatilia kiasi cha dawa vs madhara ili kuja na dosage inayo tibu huku ikipunguza madhara
7. Ni baada ya no.6 hapo juu ndio ikithibitika kuwa ni salama (safe) na inatibu/kukinga vizuri (effective in prevention/treatment) hapo ndipo inaruhusiwa kutumika kwa watu kwa kufuata miiko iliyojitokeza kuanzia panya mpaka bin adam!
Ukijaribu kuhesabu miaka hapo, kwa uchache ni 10+, hili ndio kiini cha wasiwasi wa covax (chanjo ya korona), ndani ya miezi tu hata mwaka haujaisha wanaibuka na chanjo na kuanza kushindana kuchanja watu! Ukiuliza nini madhara yake baada ya mwaka mmoja au 10, 20 ijayo, nini madhara ktk uzazi na watoto watakaozaliwa, hawana majibu! Wao wanataka tu usaini fomu ya kutomlaumu mtu endapo utapata madhara!
Kibaya zaidi haikukingi dhidi ya MAAMBUKIZI MAPYA ya corona, na kimsingi wapo wengi wamekufa kwa covid-19 huku wamechanjwa full dose ya covax! Hapa ndipo unajiuliza, unachanja watu ili iweje!?
Nimejaribu kueleza in a layman manner ili tuelewane !