Wajue wasomi hawa wenye IQ kubwa, wanaoamini kuwa Biblia ni kitabu cha kweli

Wajue wasomi hawa wenye IQ kubwa, wanaoamini kuwa Biblia ni kitabu cha kweli

Bado hathibitishi, kwangu Mimi sijaona uthibitisho hapo. Vp kama nipo India nikitoa dai Krishna amenibariki pesa nilimuomba pesa.

Labda Yoda uje umskilize huyu dada kama unamuelewa embu. Sijui samahani lakini ila Setfree unaonekan una IQ ndogo mno.
Kama sio uwepo wa Mungu, elezea sasa kilichowafanya majambazi wakakimbia kwa kusikia tu Jina la Yesu lililotamkwa na mtu ambaye hana hata wembe mkononi.
 
No. Nimekupa mifano hiyo ili usidanganyike kwamba wanaoiamini Biblia ni watu wenye IQ ndogo au ambao hawajaenda shule
IQ haina uhusiano wowote na kuamini kama vile tu ambavyo IQ haisaidii kwenye uamuzi wa mapenzi
 
IQ haina uhusiano wowote na kuamini kama vile tu ambavyo IQ haisaidii kwenye uamuzi wa mapenzi
Uhusiano upo mkubwa sana. Mtu mwenye IQ kubwa hakurupuki tu kuamua jambo. Lazima alitafakari, alifanyie utafiti na kupata uhakika. Hao wasomi sio tu kwamba waliamini. Walitoa hoja zenye mashiko zilizowafanya waamini.
By the way, kuamini ni kuwa na uhakika wa mambo yasiyoonekana. Imani sio kubahatisha.
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” — Waebrania 11:1
 
Suala la mungu hakuna uhakika kwa sababu hakuna Sheria za Sayansi zinazoweza kutumika kufanya tathmini. Mambo ya mungu hayaingii katika vipimo vya Sayansi.
 
Kama sio uwepo wa Mungu, elezea sasa kilichowafanya majambazi wakakimbia kwa kusikia tu Jina la Yesu lililotamkwa na mtu ambaye hana hata wembe mkononi.

Acha ujinga, inamaana wanaovamiwa huwa hawaga Imani eti?
 
Suala la mungu hakuna uhakika kwa sababu hakuna Sheria za Sayansi zinazoweza kutumika kufanya tathmini. Mambo ya mungu hayaingii katika vipimo vya Sayansi.
Sayansi yenyewe haijaweza mpaka leo kupima na kuelewa mambo yote ya asili. Sasa kama sayansi haijaweza kuyajua mambo yote ya asili, ndio itaweza kupima na kumjua Mungu asiye na asili. Think twice.

Isitoshe huyo msomi mmoja hapo ameishakuambia haoni mgongano wowote kati ya sayansi na uwepo wa Mungu.

Kumbuka yule kiongozi wa ile timu iliyokwenda mwezini hivi majuzi. Amebobea katika mambo ya sayansi lakini kabla ya safari alipiga magoti na kumuomba Mungu awalinde waende na kurudi salama. Hukuona mission yao ilivyokuwa successful? Wasioamini uwepo wa Mungu huwa wanajiondokea tu matokeo yake mavyombo yao yanasambaratika hewani.
 
Religion is Evolutionary Adaptation or Byproduct. Most cognitive scientists agree that the human brain evolved specific traits that make supernatural belief very easy and intuitive.
Even if evolution explains why humans are inclined toward religious belief, that does not demonstrate that the object of that belief, God, is imaginary.
 
Acha ujinga, inamaana wanaovamiwa huwa hawaga Imani eti?
Mimi siwezi kuwasemea.
Nimesema habari za imani yangu mwenyewe. Kwamba kwa kuamini nguvu ya Jina la Yesu majambazi yalishindwa na kulegea. Kwa sababu hiyo najua Mungu yupo. Maana Mungu ameniahidi kwamba akiwa upande wangu hakuna awezaye kuwa juu yangu (Warumi 8:31).

Next question?
 
Siwezi kuthibitisha uongo and logically it's impossible to prove negative claim. Lakini naweza kuonesha migongano iliopo kwenye hicho kitabu.
Ukiokoka na kujazwa Roho Mtakatifu, huwezi kuona hiyo unayodai ni migongano. Kama umejazwa Roho Mtakatifu, unapoisoma Biblia Roho Mtakatifu anakusaidia na kukuongoza kuielewa. Biblia sio kitabu cha kawaida, kimeandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu.
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote.." (Yn 16:13)
 
Samahani dada, hv umeolewa?
Usitafute mke mtandaoni. Piga magoti, uombe Mungu atakupa mke mwenye busara
Mithali 19:14
"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA"
 
Mimi siwezi kuwasemea.
Nimesema habari za imani yangu mwenyewe. Kwamba kwa kuamini nguvu ya Jina la Yesu majambazi yalishindwa na kulegea. Kwa sababu hiyo najua Mungu yupo. Maana Mungu ameniahidi kwamba akiwa upande wangu hakuna awezaye kuwa juu yangu (Warumi 8:31).

Next question?

Kama ni Imani yako mbona Sasa unatumia kama uthibitisho wa uwepo wa Mungu?
 
Ukiokoka na kujazwa Roho Mtakatifu, huwezi kuona hiyo unayodai ni migongano. Kama umejazwa Roho Mtakatifu, unapoisoma Biblia Roho Mtakatifu anakusaidia na kukuongoza kuielewa. Biblia sio kitabu cha kawaida, kimeandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu.
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote.." (Yn 16:13)

Thibitisha Genesis 1 and 2 hazina mgongano, thibitisha hadithi ya Nuhu ni kweli. Wanatheolojia wenyewe wanakubali uwepo wa hizi contradiction Sijui wewe ni nani unayeelewa zaidi watu wengine.
 
Yohana 8:58.
Yesu akawaambia kabla Ibrahim hajakuwako mimi NIKO....

Kwa uelewa wangu Hili ni jina la MUNGU alilojitambulisha kwa Mussa baada ya miaka 400.

Na YESU anakuja kulitumia hilo jina pia, baada ya wayahudi kusema kipindi cha Ibrahim YESU hakuwepo ndio akawaambia mimi NIKO.
Sawa shukrani.
 
Usitafute mke mtandaoni. Piga magoti, uombe Mungu atakupa mke mwenye busara
Mithali 19:14
"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA"
Jibu swali mdada, acha kurukaruka kama popcorn
 
Thibitisha hadithi ya Nuhu ni kweli. Wanatheolojia wenyewe wanakubali uwepo wa hizi contradiction Sijui wewe ni nani unayeelewa zaidi watu wengine.
Bado tu una mashaka na yaliyotokea wakati wa Nuhu?
Soma uzi huu:
 
Bado tu una mashaka na yaliyotokea wakati wa Nuhu?
Soma uzi huu:

Leta ushahidi hapa sio stori, maana hoja zako Setfree bado zinaonesha upeo mdogo sana wa kufikiri kwa kina. Your still making Circular logical fallacy kupitia namna unavyodadavua mambo pia hoja zako ni illogical hazina uthibitisho wowote zaidi ya kelele.

Be direct leta ushahidi wa gharika wakati wa Nuhu. Elezea wachina, wahindi, wamisri wakale, watu weusi walitoka wapi baada ya gharika kubakiza watu 8 kwenye safina. Pia toa uthibitisho wa namna wanyama wote duniani walivyoenea kwenye chombo Cha mita 130 na namna wanyama walivyotoka Australia, Artic hadi middle east kwenye safina.
 
Uwezo wako wakutafakari ni mdogo ndugu mwandishi kwa maana kuna wanasayansi wengi tu hawaamini Mungu wala uwo ukristo wako, mfano
Jerry Coyne — evolutionary geneticist na professor wa University of Chicago.

Brian Cox — physicist wa University of Manchester; ameeleza msimamo wake wa kutokuwa na imani ya Mungu.

Bertrand Russell — mwanafalsafa, mwanahisabati na mshindi wa Nobel Prize in Literature;

Francis Crick — mmoja wa waliogundua muundo wa DNA na mshindi wa Nobel Prize.
Soma vizuri kichwa cha mada na mada yenyewe. Mimi sijasema kwamba wanasayansi wote wanamwamini Mungu.
 
Back
Top Bottom