Wajue wasomi hawa wenye IQ kubwa, wanaoamini kuwa Biblia ni kitabu cha kweli

Wajue wasomi hawa wenye IQ kubwa, wanaoamini kuwa Biblia ni kitabu cha kweli

Weka hapa academic credentials zako ili tujue kama kweli unawazidi hao wasomi unaowaita wajinga.
Biblia ina majibu mengi kwanini mvua hazinyeshi kwa wakati au mahali panapohitajika mvua. Ila kwakuwa huiamini hata kukuwekea hapa vifungu ntakuwa napoteza muda
Lete hivyo vifungu vyako, kwanini mvua hazinyeshi kwa wakati
 
Bible ni vipande kutoka kwenye torati na injili,pia kuna baadhi ya mistari iliyotungwa tu na waandishi kwaajili ya watawala wa zama zao.
Hakuna mkiristo anaeijua torati au injili.
Torati kilikuwa kitabu kimoja na injili kilikuwa kitabu kimoja
Lakin ajabu leo utakuta torat na injili kwenye biblia.
Mkuu, Torati sio “kitabu kimoja.” Torati (Pentateuch) inajumuisha vitabu vitano: Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati.

“Injili” nayo sio kitabu kimoja. Katika Agano Jipya kuna Injili nne: Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Neno injili linamaanisha “habari njema,” na vitabu hivyo vinne vinatoa ushuhuda kuhusu maisha, huduma, kifo na ufufuo wa Yesu.

Kusema Biblia ni “vipande vya Torati na Injili” sio sahihi. Biblia ya Kikristo ina Agano la Kale na Agano Jipya, na ndani yake kuna aina mbalimbali za vitabu: Vya historia, mashairi, hekima, manabii, Injili, Matendo, nyaraka na Ufunuo.

Kwahiyo usishangae kukuta Torati na Injili kwenye Biblia. Huo ndio muundo wa Biblia ya Kikristo: Torati ni sehemu ya Agano la Kale, na Injili ni sehemu ya Agano Jipya.

Leta ushahidi wa dai lako kwamba baadhi ya mistari “ilitungwa tu kwa ajili ya watawala wa zama zao”
 
Wasomi, viongozi, wasanii anyone claiming he know God and he can prove he is lying. And believe ya hawa watu haibadilishi ukweli kuwa hatujui?
 
Psalm 27:1

"The Lord is my light and salvation, who shall I fear? The Lord is stronghold of my life, of whom shall I be afraid?"

🐒
Wow! Keep sharing the Word, and may it also continually guide our lives and choices.
 
Wasomi, viongozi, wasanii anyone claiming he know God and he can prove he is lying. And believe ya hawa watu haibadilishi ukweli kuwa hatujui?
Samahani mkuu. Nimesoma na kurudia comment yako ila sijakupata. Hebu chagua lugha mojawapo kati ya hizo mbili uielezee hoja yako vizuri labda ntakuelewa
 
No. Nimekupa mifano hiyo ili usidanganyike kwamba wanaoiamini Biblia ni watu wenye IQ ndogo au ambao hawajaenda shule


Hivi inatokea vp mtu mwenye IQ kubwa, Logician na Philosopher mzuri anaamini kwenye ujinga ulioandkiwa kwa bible?
 
Samahani mkuu. Nimesoma na kurudia comment yako ila sijakupata. Hebu chagua lugha mojawapo kati ya hizo mbili uielezee hoja yako vizuri labda ntakuelewa


Kwa lugha rahisi mtu yeyote kiongozi mkubwa, msanii, wasomi wanaotoa dai Mungu yupo na Wana uthibitisho wote hao ni waongo. Na Imani ya hawa watu haibadilishi ukweli ulipo.
 
Hivi inatokea vp mtu mwenye IQ kubwa, Logician na Philosopher mzuri anaamini kwenye ujinga ulioandkiwa kwa bible?
Ungetulia kwanza ukatafakari hoja zilizowafanya wasomi hao wenye IQ kubwa wakaiamini Biblia.
Kwa mfano, Francis Collins anasema, "the moral law he saw in himself was difficult to explain purely through evolution and materialism."

Hivyo alipopata maelezo mazuri ya moral law katika Biblia, aliikubali.
 
Samahani kuna kitu huwa kinanichanganya naomba unisaidie kufafanua "Mimi Niko ambaye Niko"..
Yohana 8:58.
Yesu akawaambia kabla Ibrahim hajakuwako mimi NIKO....

Kwa uelewa wangu Hili ni jina la MUNGU alilojitambulisha kwa Mussa baada ya miaka 400.

Na YESU anakuja kulitumia hilo jina pia, baada ya wayahudi kusema kipindi cha Ibrahim YESU hakuwepo ndio akawaambia mimi NIKO.
 
Kwa lugha rahisi mtu yeyote kiongozi mkubwa, msanii, wasomi wanaotoa dai Mungu yupo na Wana uthibitisho wote hao ni waongo. Na Imani ya hawa watu haibadilishi ukweli ulipo.
Okay, thibitisha uongo wao
 
Ungetulia kwanza ukatafakari hoja zilizowafanya wasomi hao wenye IQ kubwa wakaiamini Biblia.
Kwa mfano, Francis Collins anasema, "the moral law he saw in himself was difficult to explain purely through evolution and materialism."

Hivyo alipopata maelezo mazuri ya moral law katika Biblia, aliikubali.

Sababu gani?

Embu mama elezea point yako vizuri ueleweke. Unatuthibishia aje Mungu yupo hapa pamejaa watu wasio amini macho yanakutazama tupate neno kutoka kwako.
 
Hawa ni wasomi/wanasayansi walio hai ambao wamekiri wazi imani yao katika Kristo:
Francis S. Collins — PhD in Physical Chemistry; MD in Medicine
Huyu aliongoza Human Genome Project. Human Genome Project (HGP) ulikuwa mradi mkubwa wa kimataifa wa kisayansi wa kuchora na kubaini mpangilio wa DNA ya binadamu.

Francis alikuwa atheist kijana lakini alipofikia umri wa miaka 27 alibadilika akawa Mkristo baada ya kuchunguza suala la imani kwa kina. Huyu amesema wazi kwamba haoni mgongano wa lazima kati ya kuwa mwanasayansi makini na kuwa Mkristo.

John C. Lennox — DPhil (PhD) in Mathematics; DSc in Mathematics
Huyu ni Emeritus Professor of Mathematics, University of Oxford. Ana zaidi ya machapisho 70 ya hisabati na ameshiriki mijadala ya wazi na Richard Dawkins, Christopher Hitchens na wengine kuhusu Mungu, sayansi na imani. Yeye mwenyewe anaeleza kwamba aliweka imani yake katika Kristo tangu akiwa mdogo na baadaye akawa na conviction kwamba ujumbe wa Kikristo ni wa kweli.

Alister McGrath — DPhil (PhD) in Molecular Biophysics; DPhil (PhD) in Intellectual History.
Alisoma Chemistry Oxford na akapata doctorate katika molecular biophysics. Huyu pia alikuwa atheist, lakini baadaye akabadilika na kuwa Mkristo. Oxford yenyewe inaeleza safari yake hiyo.

Wewe unayeupinga Ukristo na kusema eti Biblia ni kitabu cha riwaya, umeandika vitabu vingapi vya kisomi/kisayansi au una PhDs ngapi? Labda tuanzie mjadala wetu hapo.

Mkatae shetani anayepofusha fikra zako ili nuru ya Kristo isikuangazie.

2 Kor 4:4
"ambao ndani yao mungu wa dunia hii(shetani) amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."
Mimi nani hata ni Katae?

Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Biblia ni kitabu cha kweli na YESU KRISTO ni BWANA na Mwokozi.
Na yeye ndiye njia, kweli na uzima.
 
Okay, thibitisha uongo wao



 
Sababu gani?

Embu mama elezea point yako vizuri ueleweke. Unatuthibishia aje Mungu yupo hapa pamejaa watu wasio amini macho yanakutazama tupate neno kutoka kwako.
OK, ngoja nikupe points chache. Nimeishashuhudia humu sio mara moja jinsi nilivyopona magonjwa mengi kwa muujiza baada ya kutamka jina la Yesu Kristo ambaye ni Mungu pamoja nasi.

Nimeshuhudia sio mara moja jinsi ambavyo niliwasambaratisha majambazi waliokuwa wanataka kunidhuru, just by rebuking them in Jesus name. Nimeishashuhudia humu jinsi nilivyopata miujiza ya pesa baada ya kumuomba Mungu. Yote hayo yamefanyika baada ya kusoma na kuiamini Biblia hii hii iliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu.

Nimeeleza katika huo uzi wa dalili za kuja kwa Yesu kwamba hizo dalili zilitajwa na Yesu mwenyewe, ambaye ni Mungu, zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, na leo zinatimia mbele ya macho yetu. Huo si ni ushahidi tosha kwamba Mungu yupo na aliyosema ni kweli?

Bado tu huamini kwamba Mungu yupo?
 
Mimi nani hata ni Katae?

Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Biblia ni kitabu cha kweli na YESU KRISTO ni BWANA na Mwokozi.
Na yeye ndiye njia, kweli na uzima.
Amen, una heri wewe usiyeionea haya Injili ya Kristo.
“Maana kila mtu atakayenionea haya mimi na maneno yangu... Mwana wa Adamu naye atamwonea haya mtu huyo...” (Marko 8:38)
 
OK, ngoja nikupe points chache. Nimeishashuhudia humu sio mara moja jinsi nilivyopona magonjwa mengi kwa muujiza baada ya kutamka jina la Yesu Kristo ambaye ni Mungu pamoja nasi.

Nimeshuhudia sio mara moja jinsi ambavyo niliwasambaratisha majambazi waliokuwa wanataka kunidhuru, just by rebuking them in Jesus name. Nimeishashuhudia humu jinsi nilivyopata miujiza ya pesa baada ya kumuomba Mungu. Yote hayo yamefanyika baada ya kusoma na kuiamini Biblia hii hii iliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu.

Nimeeleza katika huo uzi wa dalili za kuja kwa Yesu, kuwa dalili alizozitaja Yesu za kuja kwake zinatimia. Na dalili zote hizo zilitajwa na Yesu mwenyewe, ambaye ni Mungu, miaka zaidi ya 2000 iliyopita.

Bado tu huamini kwamba Mungu yupo?


Bado hathibitishi, kwangu Mimi sijaona uthibitisho hapo. Vp kama nipo India nikitoa dai Krishna amenibariki pesa nilimuomba pesa.

Labda Yoda uje umskilize huyu dada kama unamuelewa embu. Sijui samahani lakini ila Setfree unaonekan una IQ ndogo mno.
 
Back
Top Bottom