Wakati Tanzania ipo busy na masuala ya Simba na Yanga, Wakenya wanazidi kutupiga gap. Ujerumani imekubali kuwapokea Wakenya 250,000

Wewe gumbaru hao wakenya wamenda kama experts au vibarua?! Dereva ni expert wa nini?! Kuendesha gari la taka au?
Wewe ndo Gumburu kabisa. Kama umesikia vizuri taarifa za DW Kenya imesifiwa kwa kuwa na Best ICT Experts na Techn innovators katika bara la Africa. Nenda Kenya utaona namna Vijana wa kule walivyobuni na kuanzisha many marketable Tech related Programs na softwares ambazo zimenunuliwa na hata Makampuni makubwa katika kutoa huduma na uendeshaji wa biashara . Ni wabunifu na ni wazuri katika kubuni na kuendesha many Tech Innvoations.
 
Unawaonea bure viongozi wa Tanzania. Hivi kwa aina ya viongozi tulio nao kwa saa unaona kuna hata mmoja anaweza ku negotiate deal kama hii ya Kenya na Germany?
 
Endelea kufuatilia kina magoma na kagoma, Wakenya wanaenda kupiga pesa huko nje na kuna fursa zaidi za kujiendeleza kimasomo kupata kazi zenye mishahara mirefu zaidi, connections za kuja kununua maparachichi Tanzania kuyauza Ujerumani, n.k.
Ukishindwa kutoboa Bongo, ningumu kutoboa sehem nyingine yeyote duniani.
 
Diaspora wa Kenya wanaingiza kenya Dollar Bilioni 4.2 kwa mwaka sawa na Trilioni 10 za Kitanzania kwa mwaka. Hii ni zaidi ya mapato ya utalii ya Tanzania kwa mwaka.

Kwenye ni nchi ya Tano kwa kupata fedha nyingi sana kutoka kwa diasporas wao barani Afrika. Wakenya wengi wanapiga kazi nje ya nchi na wanapata pesa nyingi sana wanarudisha nyumbani. Hiyo hela sio muda inaenda ku Double.

Nimekutana na wakenya wengi sana kwenye taasisi ama makampuni mengi hapa Afrika lakini wabongo ni wa kuhesabu ama hakuna.

Watanzania elimu yetu ya hivyo ya kubabaisha, hakuna confidence, hatuna skills zinazohutajika Duniani.

Acha tuendelee kuwashangilia kina magoma.
 
Umeuliza swali halafu ukajijibu bila hata kunipa muda wa kuku jibu na ukaweka conclusion zako kabisa.

Mfano mzuri Tido mhando alikua BBC akaletwa TBC, akaibafili TBC wakati huo ikawa inaonesha hadi Epl na kuwa na vipindi vingine vizuri kama Ze comedy, baadae Akaenda Azam hadi leo matokeo yake tunayajua.
 
wabongo wengi wanasema diaspora wa kibono ngumu sana kutoa support tofauti na wa kikenya hili lina ukweli?
 
Haibadilishi maana kwamba nchi yao inaanguka na Talent zinaenda Nje hali ya kuwa vilaza wanabaki Nchini.

Pia Si Lazima Diaspora awe ni ku export workforce, hizo ni situation mbili tofauti.
 
Haibadilishi maana kwamba nchi yao inaanguka na Talent zinaenda Nje hali ya kuwa vilaza wanabaki Nchini.

Pia Si Lazima Diaspora awe ni ku export workforce, hizo ni situation mbili tofauti.
Inaanguka na nini? Kwa hiyo diaspora ni ku import workforce?
 
Mfano hio ikitokea huku....unahisi ni watu wa mlengo wa chama gani watakaopata hizo fursa za kuenda huko?
Ni bora tu zisije huku.
 
Nimesoma magazeti ya Kenya,habari haiko kama ulivyoiweka.

Kwanza kwenye makubaliano hayo hakuna idadi yoyote ya wanufaika iliyotajwa.
Pili,ni Mpango wa mabadilishano (Exchange program) kati ya Kenya na Ujerumani.Ni Mpango wa nipe nikupe.
 

Heri tulio busy na Yanga kuliko wewe unayeshadadia vitu usivyo na uhakika navyo...
 
VILE VILE WAKATI TANZANIA INAPUMBAZWA NA CCM WAKENYA WANATUPIGA GAP .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…