Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Nafuatilia kila post yako. Hongera sana. Nakutakia kila la heri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp mkuu unaweza kuanzisha uzi wa stori ya kweli jinsi ulivyofanya hii ishu ya bangi, vp maslahi yake tangu umeanza mpaka ukaacha?
 
Nilikua hata sijafulia ila ilikua tamaa tu, vipato vya wazazi havikua juu ila si haba na nikagundua wanapofichaga mpunga, nilichonga ufunguo wa ziada wa mlango wao,i nikitoka shuleni namtuma house girl aende dukani kununua hata karanga za mia ilimradi nibaki peke yangu kwenye nyumba nifanye ujinga wangu wa kupiga tukio, nikiingia humo nanyooka moja kwa moja kwenye kabati kubwa la Nguo walipokuwa wameficha kibunda kama cha milioni 8 hivi katikati ya nguo, nilikua nachomoa za katikati kama elf 30 hivi nikidhani nikichomoa za kati hawatajua. Matumizi yalikuwa ya kijinga na hata sikumbuki cha maana nlichofanya.

Kuna kipindi ndugu wakaja ile mbinu ya kumtuma house girl dukani haikuwa na kazi tena, nikawa naiba kavu kavu bila kuonwa na mtu na hapa nadhani nilianza kujengeka kuwa jambazi sasa, Tabia ilidumu kwa wiki 3 nikiwa nimechomoa kama laki 2 jumla, nafsi ikanisuta niache mara moja, hadi leo ule ufunguo nimeutunza kumbukumbu ya ujinga kama sio unyama niliowahi kuwafanyia watu walionipenda na kunijali.

Mnisamehe sana wazazi wangu pengine mungu akipenda ipo siku ntawaambia huu upuuzi niliokua nawafanyia,
 
Vp mkuu unaweza kuanzisha uzi wa stori ya kweli jinsi ulivyofanya hii ishu ya bangi, vp maslahi yake tangu umeanza mpaka ukaacha?
Poua ndugu ni story ndefu ila panapomajaliwa nitatoa story yote mana mie nimesota tangu umri wa miaka 14 mpk sasa ikiwemo kuona akina mama wanabakwa pale keko mataa nk
 
Ahaa KK SECURITY niliwahi kwenda kuomba kazi wana ukiritimba sana walinipitisha kwenye ubao wao flani hivi unatakiwa uuguse sasa mimi nilikua chini ya hapo wakanikataa, daah niliuzunika sana.

Kweli kazi za Ulinzi sio za kudumu na ni hatari alafu pia unakua dormant kichwa kinalala hakifikirii maisha mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…