Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Ngoja na mimi nitoe mchango wangu hapa
Miaka ya 2004-2007 nilikuwa nipo vibaya sana kipesa. Nikamfuata shemeji yangu mume wa dada yangu ambae alikuwa ni Contaractor wa zege kwenye kampuni moja kubwa ya ujenzi. Yaani hiyo kampuni ilikuwa na kazi nyingi sana na tenda zote za Zege anapewa yeye. Basi nikamuambia aniunganishe kwenye kazi ya zege, mwanzoni alisita akaniambia hii kazi ngumu hautaiweza ila nilivyozidi kumlazimisha akaamua kunichukua. Mwanzoni alinipa kazi nyepesinyepesi kama kusimamia maji au kumsaidia yule operator wa Vibrator ila siku zilivyokwenda nikaona taratibu ananihamisha kwenye kazi ngumu. Kidume nikawa najitahidi kukaza ili asije kuniambia unaona nilikuambia huwezi. Siku moja nikaona ili nipate pesa nyingi nikachagua kubeba,nikapewa karai(siku hizi wanatumia ndoo) kubeba zege kupeleka ghorofa ya tisa,aisee sitasahau hiyo siku maana nilichakaa vibaya ssna. Ila baadae nikaanza kuzoea na mimi kuwa profesional wa Zege. Kazi ya zege ni mojawapo ya kazi ngumu yenye kuhitaji nguvu na uvumilivu wa matusu na kejeli kutoka kwa wazoefu hasa ukiwa mgeni. Siku moja tupo kuna jamaa alimleta Mke wake kwenye site akamuomba Shem ampe kitengo kwenye Zege akamkubalia, aisee yule dada nilimuonea huruma. Tulikuwa pamoja kwenye idara ya kubeba kokoto kuzitumbukiza kwenye mashine ya kuchanganya zege, alikuwa hawezi hata kubeba ndoo ya kokoto nikawa namsaidia. Baada ya lunch tulivyorudi akapelekwa kwenye maji.
Kazi nyingine ngumu ambayo sitaweza kuisahau ni kufanya kazi katika kiwanda cha Nondo pale Mwenge, aisee ile kazi kifo ni njenje kabisa. Mnabeba uji wa chuma ambao ni wa moto sana kwenda kuweka kwenye mifereji fulani hivi. Nilifanya kwa wiki moja tu nikasepa.
Nashukuru kwa sasa imebaki story tu maisha yanasonga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee hiyo ya kubeba uji wa zege inatisha nauonaga tu kwenye vipindu vya televisheni unavyotisha sipati picha kuubeba.
 
Aisee hiyo ya kubeba uji wa zege inatisha nauonaga tu kwenye vipindu vya televisheni unavyotisha sipati picha kuubeba.
Zile Scraper zinazokusanywa mtaani ndio zile wanaweka kwenye mtungi mkubwa ambao unaivisha mpaka unakuwa uji kabisa. Fikiria hapo moto wake ukoje halafu ndio mnabeba. Hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana mkuu... Ila umifurahisha hapo uliposema kana zima kabisa...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshenzi Sana mbwa huyo.....
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maisha haya.acheni tu.

Nilishawahi kufikiria kujiuza.
_ila namshukuru MUNGU Sana kwa kuniepusha na kikombe cha uzinzi..
Asante MUNGU kwa yotee[emoji120][emoji24]
..ila kuna mwanaume alikuwa ananitongoza mda mrefu na nlikuwa simpendi kweli.
Ila nilipitia magumu acha..nikajikuta namkubalia bila kupenda na mpaka sasa ni MUME wangu.

Baba kedoo nakupenda sana.
Umenivusha kwenye MAGUMU kutoka kusimangwa mpaka Kuheshimiwa....
[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzeebaba plse share zaidi.Jera ulitoka vip. Pia pole sana kwa mikasa mizito.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaman pole,mshenzi yule anasubir kupewa na demu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…