Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Nilipigika kudadeki mpaka nikasepa bongo maana ilikuwa mikosi tupu,ikabd nipige deal hatari za kuvuka boda ,one day Nakonde Boarder (Zambia) another day Msumbuji sijakaa vizuri KwaZulu biashara za kuuza roho mixer kukamatana na migration kulala lockup mambo ya illegal business .

Uwoga wako ndio umasikini wako coz million moja nilikuwa natengeneza ndani ya siku moja yaani go and return I can make a million.

Now days najihisi nimerogwa sina harakati kabisa kama nimewekwa Karantini coz nishakuwa mzee inabdi nitulie tu.
 
Aisee nilipomaliza tu form 4 nilikuwa sina mbele wala nyuma,nikaingia kubeba mkaa kwa baiskeli toka shamba kuja mjini ,nilifanya siku mbili tu,nilikuwa nanunua gunia 8000 naenda kuuza 17,000. Ukianza kusukuma ukisimama huwezi kuinama kinauma,kuna siku nikifika usiku nikakuta mama ntilie washafunga nikakuta ugali tu hamna mboga,kwa njaa niliyonayo nilikula ugali bila mboga nikashiba fresh tu...namshukuru Mungu leo nimetoka huko
Mwaka 2018 nilipigika sana nilibuni biashara ya kuuza mkaa siku nzima inaweza kupita hakuna mtu anayekuja kununua mkaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nakonde Boarder ilikuwa mishe gan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kichwa cha habari tu.

Nauliza?

Hivi kuna kazi ya ajabu?
 
mkuu mi mwenyew nishaapa kufanya kazi kampuni ya wahindi.wale ni mashetani
mi nakumbuka niliwahi kufanya nao Kaz ,hawataki usimame ,hawataki uguse chochote tofauti na ulichopangiwa

wanajali ratiba zao tuu.mi ilikuw ni kazi ya kushusha kokoto kwenye semi duuu ile kazi acha
nilifanya Siku 3 tuu .Siku ya mwisho nguvu ziliniishia +kuugua hapo hapo homa ikapanda ,kilichoniudh ni muhind mmoja alipomwambia mwenzake et OYA TOA HII TOTO NJE CHOKA SANA HII LETE INGINE ,SITAKI ONA TENA HII TOTO SITE.

ile kauli iliniboa nikasema fresh yote maisha ,sasa wakat naenda kuchukua mazaga yangu nisepe,,,sinikakuta huyo boya amechaji simu, hahaha nkachomoa kwenye chaja tia kwenye begi kisha huyoo mana ulinzi ulikuw hafifu sana.kufika kitaa nikaiflash na kutangaza mteja na ukawa ndo mtaji wa kuanzia.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hehehehe wabongo bhana ndo maana hatuaminiki kabsa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]kwa hyo uliunga juhudi

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hyo mkuu ulimsent na kumdeliver eksi wako akaliwe kimasihara upate ngawira[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Uko vizur mdada [emoji122][emoji122]

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Daah pole sna mkuu.Alafu utakuta kuna watu wanashabikia #Viva sijui nani Viva#Mara kidumu hoye kidum#Usijali Mungu atakuvusha katika hili

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Aisee nilifikiri kubaki DSM baada ya chuo ni lelemama. Kumbe ni mabaki ya Boom yalikuwa yananidanganya.

Nikasambaza CV mpaka na hela ya kuprint, kula na nauli zikaisha bila kupata kazi.

Nyumbani mbali na nauli sina. Kazi ikawa ni kujitetea nisife njaa. Nikaona njia pekee ya kusurvive ni kusahau kama nina Degree.

Nikafanya kazi yoyote bora mkono uende mdomoni, lakini bado Jamaa wananitenga wanahisi naigiza Maisha eti mimi ni mpelelezi!

Nikaona isiwe tabu, nikachagua Nyumba zangu Tano kupita kuomba kuwa houseboy. Nikikosa basi nabadili plan. Ya tatu nikapata ila kwa kudanganya niliishia la saba.

Nilifanya Kazi za ovyo vya kutosha, mpaka nikatamani niendelee nimalizie kuomba kazi zile nyumba nyingine zilizobaki labda ningepata yenye nafuu.

Wazo likanijia ni bora niseme ukweli nilisoma labda kazi zitabadilika. Cha ajabu majukumu yakaongezeka. On top of all, ndio kwanza nikawa mwalimu wa tuition kwa watoto wa familia ya Boss. Wadogo wa kiume wako primary mmoja wa kike alikua chuo mwaka wa pili. Usisahau mshahara ni ule ule wa hovyo.

Kwa kazi za binafsi nilizokuwa namfanyia, ilifika mahala mke wa Boss akaanza kucatch feelings za kuhitaji niwe naye. Nilikua naelekea kukubali kwa sababu Sina namna. Ghafla Boss nadhani alihisi kitu akaona ni bora anisomeshe CPA (Wahasibu wanaelewa) ili niwe busy zaidi. Nilikua busy sijawahi ona.

Baada ya yoote, Boss aliniunganisha nikapata kazi. Kutoka kwenye familia ya Boss nilipata Mke Mwema ambaye ni mwanafunzi wangu. Japo mke wa Boss bado ananisumbua.

Ila uhauseboy sitakaa nisahau! Nilikuja kuapa sitakaa nimnyanyase msaidizi wangu wa kazi kwa vyotote iwavyo. Duh, Guys hawa watu wanapitia Magumu sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Umenifunza mengi sana blaza kaka

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Ongea vizuri na hyo baka baka mkuu [emoji2][emoji2]

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Aisee nmecheka[emoji23][emoji23][emoji23] sna eti twende ukachukue charge nyumbani.Merci Le fere^ de la congole le kinshansee[emoji16][emoji16]

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…