Wakati Waafrika wakiuzwa kama watumwa, Mashehe, Mapadre, wachungaji wa Ulaya, Amerika na Uarabuni walikuwa wapi?

Sote tunajua kuwa imani za dini (Ukristo na Uislam) vilikuwepo kabla ya utumwa. Umewahi kujiuliza wakati Waafrica wanauzwa kama Mbuzi kwenye masoko ya Ulaya, Marekani, Uarabuni, viongozi wa dini wa nchi hizo walikuwa wapi kupinga biashara hiyo, tena nchi kama Marekani watumwa wakilimishwa kwenye mashamba kwa uwazi kabisa? Jambo hili huwa najiuliza sipati majibu.

Kwa upande wa Tanzania, rasilimali zote nyeti zinamilikiwa na wawekezaji huku Watanzania wakibaki kama Watwana kwenye Maliasili zao. Madini yanachimbwa huku michanga ikibebwa na kupelekwa tusipojua, kilichomo humo hatujui, ndege kutoka Dubai inatua Loliondo na kuondoka, hivi tuna uhakika kama wanabeba wanyama hai? Vipi ule wimbo wa kwamba Tanzania iwe tayari kuelekea kwenye uchumi wa gesi ya Mtwara na Lindi, tena tunakaambiwa yatasambazwa mabomba ya gesi, kweli huo uchumi wa gesi tunauona?

Watanzania tusikubali kuingia kwenye mitego ya Wanasiasa, achaneni na propaganda za eti tusichanganye siasa na dini, viongozi wa dini zote, Waislam, Wakristo na dini nyingine, kemea mikataba mibovu. Tukiruhusu mikataba mibovu, vizazi vyetu bila kujali dini zetu vitaishia kuwa dereva bodaboda huku watoto wa kizungu wakitafuna urithi wetu.
Nenda basi ata Bagamoyo ukaone juhudi za kanisa kukomboa watumwa, sio mbali hapo. Unajua kuna kijiji pale kilianzishwa na kanisa na wakawa wanaishi watumwa waliokombolewa? Mpaka leo vizazi vyao vipo hapo Bagamoyo mjini?
 
Nadhani mtoa Mada hajasoma history....waliokuwa wanaendesha biashara za utumwa ni waarabu.na wamisionary na humanitarian ndio walioshinikiza kuachishwa Kwa biashara ya utumwa.kama Kuna watu wa kuwalaumu kuhusu biashara ya utumwa ni hao hao warabu.

Waarabu walikuwa wanauza wapi hao watumwa?
Wanaanunua wapi na kuuza wapi?

Biashara inahitaji sehemu ya kuchukua mzigo na sehemu ya kuuza.
 
Sote tunajua kuwa imani za dini (Ukristo na Uislam) vilikuwepo kabla ya utumwa. Umewahi kujiuliza wakati Waafrica wanauzwa kama Mbuzi kwenye masoko ya Ulaya, Marekani, Uarabuni, viongozi wa dini wa nchi hizo walikuwa wapi kupinga biashara hiyo, tena nchi kama Marekani watumwa wakilimishwa kwenye mashamba kwa uwazi kabisa? Jambo hili huwa najiuliza sipati majibu.

Kwa upande wa Tanzania, rasilimali zote nyeti zinamilikiwa na wawekezaji huku Watanzania wakibaki kama Watwana kwenye Maliasili zao. Madini yanachimbwa huku michanga ikibebwa na kupelekwa tusipojua, kilichomo humo hatujui, ndege kutoka Dubai inatua Loliondo na kuondoka, hivi tuna uhakika kama wanabeba wanyama hai? Vipi ule wimbo wa kwamba Tanzania iwe tayari kuelekea kwenye uchumi wa gesi ya Mtwara na Lindi, tena tunakaambiwa yatasambazwa mabomba ya gesi, kweli huo uchumi wa gesi tunauona?

Watanzania tusikubali kuingia kwenye mitego ya Wanasiasa, achaneni na propaganda za eti tusichanganye siasa na dini, viongozi wa dini zote, Waislam, Wakristo na dini nyingine, kemea mikataba mibovu. Tukiruhusu mikataba mibovu, vizazi vyetu bila kujali dini zetu vitaishia kuwa dereva bodaboda huku watoto wa kizungu wakitafuna urithi wetu.
Hatuna uwezo wa kukwepa kuingia mikataba, tunaishi tukihitaji uwekezaji wa kila aina.

Ulishauona mkataba wa bomba la mafuta upo vipi?. Ulishaiona mikataba iliyonunua ndege tisa zilizopo hivi sasa?

Hizi anga za mikataba ni za juu sana sio kila mtu mwenye uelewa wa kuweza kuongelea mikataba akaeleweka, hii ni fani ya watu inayosomewa vyuoni miaka na miaka.

Lakini tumeamua kuwa na taifa la wajuaji, basi tuendelee kupuyanga tu. Muuza machungwa pembeni ya barabara anamponda kocha wa kigeni aliyeletwa na uongozi wa Yanga au Simba!. Ni taifa la kijinga linalochezea elimu na sio ajabu linaendelea kukwamia katika umaskini.
 
Acha dhambi acha Rushwa utaona Matunda yake maana Mwenyezi Mungu atakulinda kila siku unapoamka,unapotembea na unapolala hatakuacha kamwe.
Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia unia isiyo na dhambi?

Mungu alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kutenda dhambi?

Je bado huoni tu, kwamba Mungu huyo hayupo?
 
Kama Mungu hayupo basi na wewe ni mzimu.
 
Umeshindwa kujenga hoja ya kuonesha uwepo wa huyo Mungu.

Sasa unafanya personal attack.

Tufanye basi mimi ni mzimu.

Mungu Mkamilifu, Alishindwaje kuumba Dunia yenye watu wakamilifu bila uwepo wa mizimu?

Kwa nini uwepo wa Mungu una utata?
 
Watu wote ni wakamilifu isipokuwa nafsi zao ndio zinazowatofautisha.
 
Halafu bado munataka waarabu warudi? Labda kama utumwa ulikuwa mzuri waleteni tu- wajukuu bado tunakimbuka historia ya slave trade hadi form six. Hatuwataki watesi wa babu zetu. Warudi tu huko zenj walipotimuliwa Kwa Mapinduzi matukufu na Akina John Okero

Sent from my Infinix X6820 using JamiiForums mobile app
 
Walioshinikiza kusitishwa kwa biashara ya utumwa ni wamishenari, na baada ya kusitishwa kwa biashara ya utumwa ni kanisa ndio liliwagomboa watumwa wote waliokuwa sokoni kwa kuwalipia!. Lile kanisa Mkunazini limejengwa mahali palipokuwa na soko la watumwa. Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama
P
Tusiwe na mahaba na dini zetu both waarabu na wazungu walishiriki vyema kabisa katika biashara ya utumwa.

Sent from my Infinix X6820 using JamiiForums mobile app
 
Ili jamii/nchi iendelee inapaswa kuendelea kwenye nyanja tatu ambazo ni Uchumi, Siasa na Utamaduni...

Hivi vitu vitatu haviwezi kutenganishwa, dini ni sehemu ya Utamaduni na zinaweza zikawa za asili au za mapokeo...
Dini sio utamaduni wetu
 
Nenda basi ata Bagamoyo ukaone juhudi za kanisa kukomboa watumwa, sio mbali hapo. Unajua kuna kijiji pale kilianzishwa na kanisa na wakawa wanaishi watumwa waliokombolewa? Mpaka leo vizazi vyao vipo hapo Bagamoyo mjini?
Utumwa umefanywa kwa miaka 400, viongozi wa dini wazungu na mashekhe wa kiarabu walikuwa wapi?
 
Kanisa limefika Bagamoyo 1800s, na wakakomboa watu mpaka Zanzibar, sasa uislamu na waarabu wapo pwani ya mashariki tangu karne ya 8!! 🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️ wanamajibu zaidi.
 
Sote tunajua kuwa imani za dini (Ukristo na Uislam) vilikuwepo kabla ya utumwa. Umewahi kujiuliza wakati Waafrica wanauzwa kama Mbuzi kwenye masoko ya Ulaya, Marekani, Uarabuni, viongozi wa dini wa nchi hizo walikuwa wapi kupinga biashara hiyo, tena nchi kama Marekani watumwa wakilimishwa kwenye mashamba kwa uwazi kabisa? Jambo hili huwa najiuliza sipati majibu.

Kwa upande wa Tanzania, rasilimali zote nyeti zinamilikiwa na wawekezaji huku Watanzania wakibaki kama Watwana kwenye Maliasili zao. Madini yanachimbwa huku michanga ikibebwa na kupelekwa tusipojua, kilichomo humo hatujui, ndege kutoka Dubai inatua Loliondo na kuondoka, hivi tuna uhakika kama wanabeba wanyama hai? Vipi ule wimbo wa kwamba Tanzania iwe tayari kuelekea kwenye uchumi wa gesi ya Mtwara na Lindi, tena tunakaambiwa yatasambazwa mabomba ya gesi, kweli huo uchumi wa gesi tunauona?

Watanzania tusikubali kuingia kwenye mitego ya Wanasiasa, achaneni na propaganda za eti tusichanganye siasa na dini, viongozi wa dini zote, Waislam, Wakristo na dini nyingine, kemea mikataba mibovu. Tukiruhusu mikataba mibovu, vizazi vyetu bila kujali dini zetu vitaishia kuwa dereva bodaboda huku watoto wa kizungu wakitafuna urithi wetu.
Watoto wa kizungu wapi? koo za, akina JK, Nauye, Malima, Samia, Mwinyi, Kinana, Lowasa, Sokoine, Makamba, n.k zina uhakika wa kula mema ya nchi milele
 
Back
Top Bottom