Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Tatizo lako ni kumtoa wapi Maria au ni hiyo "m" wa mwisho kwenye Mariam?
 
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Kwanza kuwa mpole unapotaka kujua au kuuliza kitu usichofahamu au usichokuwa na uhakika nacho. Hilo ni jina tu halimbadilishi mtajwa kuwa mtu tofauti. Maeneo, makabila au hata mila tofauti zinaweza kutamka jina hilo hilo katika mazingira yao. Maria ni huyo huyo Mariamu, au Yosefu ni huyo huyo Yusufu, au Moses ni huyo huyo Musa. Abdul ndiyo huyo Abdool, Karim ndiyo huyo Kareem, Saeed ndiyo huyo Said. Inategemea wewe ni Mwarabu, au Mhindi au Mzungu au Myahudi au Mwafrika, maana hata sasa wewe unajiita Che Mittoga badala ya Mitoga!
 
Mkuu hapo ni mama au mwana?
Weka vifungu vya bible
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…