Kinachouma zaidi ni pale mtu ulikuwa unakusanya watu lundo kwenye kampeni, siku ya siku unakuja kupigwa na kugalagazwa vibaya, huwa inauma Sana
Kinachowafanya wanasiasa watangaze mapema eti uchaguzi utakuwa mgumu na usioeleweka na kwamba eti wanapendwa Sana, ni Kwa sababu ya watu kwenda kusikiliza kile wanasema, wengine kwenda kushangaa tu, na wengine kama mimi, kwenda kuangalia miujiza ya Mungu Kwa mgombea wa Chadema, jinsi Mungu alivyomtendea
Wanasahau kwamba Siku ya kupiga Kura inakuwa ni Siri ya mtu, hichi ndicho huwa wanajisahau hasa wajinga wachache humu, hushughurika na kusherehekea wingi wa mkusanyiko wa watu badala ya kusherehekea siku ya ushindi
Nyie sherehekeeni huo ujinga, wenzenu watasherehekea ushindi